Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,484
- 30,160
Vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa, vimetoa taarifa ya kufungwa jela, kwa miaka 15, kwa aliyekuwa mkuu wa polisi, wa jimbo la Chongquing, nchini China, Kwa makosa kadhaa, likiwemo la kutumia vibaya madaraka yake, kwa lengo la kumlinda mtuhumiwa wa mauaji. Mkasa wenyewe uko hivi, mwaka jana, mwezi Novemba, mwaka jana,mfanyibiashara mmoja, anayeitwa Neil Heywood, alifariki kwenye hoteli moja, kwenye jiji la Chongquing, nchini China, katika mazingira ya kutatanisha. Akalazimika mkuu wa polisi wa jimbo hilo, Wang Lijun, aunde Tume ya kipolisi, kuchunguza kifo hicho.
Matokeo ya uchunguzi wa kifo hicho yalipotoka, yakaeleza kuwa mtu huyo alikufa kutokana na kunywa pombe kupita kiasi. Hata hivyo, ukweli wa mambo ni kuwa mtu huyo, aliwekewa sumu, na mfanyakazi wa ndani, wa kiongozi mmoja wa juu kabisa wa chama cha kikomunisti nchini humo, Bo Xilai, kwa maelekezo ya mke wa huyo wa Kigogo, aliyetambulika kwa jina la Gu Kailai, Habari hizo alizitoa mkuu wa polisi mwenyewe, Wang Lijuan, baada ya kutokea kutoelewana, kati yake na huyo mwanasiasa kigogo, wa jimbo hilo la Chongquing. Alieleza kuwa njama hizo za mke wa kigogo wa chama cha kikomunisti wa nchi hiyo, zilifanywa kutokana, na mtoto wa kigogo huyo, ambaye ni mshirika kibiashana na huyo Neil Heywood, kutofautiana katika mambo ya biashara zao. Kutokana na taarifa hizo toka China, tunaweza kufananisha na matokeo ya mauaji mengi ya kutatanisha ambayo yamekuwa yakitokea nchini mwetu, na kuishia uundwaji wa Tume za kipolisi, ambazo mara nyingi, hutuletea matokeo ya marehemu aliuawa na kitu kizito, ambacho hakijajulikana, kililurushwa na nani! Lakini kama imetokea China kwa mkuu wa polisi kujisalimisha ubalozini, na kueleza kinagaubaga kuhusu kigogo wa chama cha kikomunisti, alivyohusika katika kuamrisha mauaji, na kumuelekeza kigogo wa polisi, alifukiefukie hilo jambo, lisijulikane, hadi pale kigogo huyo wa polisi, alipoamua kupasua jipu.
Naamini, hata hapa TZ, hawa maaskari wetu wa vyeo vya chini, wanaopokea maelekezo ya kuua raia wasio na hatia toka kwa mabosi wao, akina Mwema, Chagonja, Kamuhanda, Shilogile na wengine, ipo siku maaskari hao wa vyeo vya chini, wataamua kufunguka na kueleza ukweli wote. Hapo ndipo tutakaposhudia kigogo mmoja baada ya mwingine, wakipandishwa kizimbani, na hatimaye,kuhukumiwa kwenda jela kwa miaka kadhaa! kipindi hicho kimekaribia sana nchini mwetu, maana damu za wanyonge wengi, zimemwagika bila sababu ya msingi, kwa ajili tu ya kulinda maslahi ya wakubwa!!!!