IGP Mangu: Trafiki wengine hawa hapa

IGP Mangu: Trafiki wengine hawa hapa

10672290_763564583705144_3787979452770158771_n.jpg


Hawa watavunja viti.

Inaonekana magari yalikuwa hayajapita kwa muda mrefu, hadi wameweka chandarua!
 
biashara mbovu ndio maana wanalala, hamuoni barabarani hakuna magari!
 
Jaribuni kufikiria kwa undani madhara ya picha hizi kabla hamjapost. Kufukuzwa kazi jamani ina athari sana jamani.
 
utetezi upo walikuwa kwenye freshers. welcome first year
 
Kama ungekuwa wewe ndo unasemwa na kisha unarushwa hewani ungefurahi, kazi za kukaa tu na kungoja magari ya watu na ya serikali sio kazi rahisi kama wanavyodhani walio wengi. Tuwapende askari wetu na kisha tuwaelekeze pale wanapokosea nao ni binadamu maana sio miungu na hivyo wanamapungufu kama uliyo nayo wewe na mimi.
Tuache unafiki na ushabiki kama ndugu yako angekuwa trafiki na kisha akafukuzwa kazi je ungefurahi? Vivyo hivyo ndugu wa hawa matrafiki mnaowasema hawafurahi kuwasema ndugu zao bali wangefurahi kama ungemweleza afanye nini ili kuboresha utendaji wake na sio kufukuzwa kazi. Maisha sasa ni magumu kwa kila mtu usipende mwenzako aharibu kazi yake maana "ukiingia kwa fitna utaondoka kwa aibu maana unataka kujionesha kuwa wewe umekamilika kuliko wengine na kama wabunge pamoja na ubaridi wa kiyoyozi wanalala (kusinzia) kwanini askari katika natural air asilale (kusinzia)". Tuache ushabiki usiokuwa na maana bali wengine waloajiriwa ni wadogo zetu tuwaelekeze wawe watumishi wazuri serikalin na pia wajiwekee akiba ya baadaye na wajifunze kutunza fedha mapema kabla ya kupata pension zao ili wazitumie vizuri na waboreshe maisha yao na familia zao mapema ili waepuke kuja kuwa walinzi wa maduka,majumba ya watu na maghala ya matajiri mara wanapostaafu tu utumishi wa umma.
 
Back
Top Bottom