Mzalendo2015
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 6,704
- 9,060
Wana JF,
Kwa hali ya kisiasa,kiulinzi na kiusalama inayoendelea kwa sasa, viongozi waandamizi wa Jeshi la Polisi kwa maana ya IGP Ernest Mangu na Wasaidizi wake Kamishina Simon Ciro na wengine wanapaswa kujiuzulu!
Nasema hivi kwasababu kiukweli kabisa wameshindwa kusimamia majukumu yao.
Kitendo cha Mkuu wa wa Mkoa wa Dar Bwana Paulo Makonda kuanza kuingilia kazi za Kipolisi kiasi cha yeye Makonda kuonekana ndiye anayepanga mbinu na mikakati ya kupambana na uhalifu ikiwemo madawa ya kulevya kumelidhslilisha Jeshi hilo!
RC Makonda alianza kama utani kuwa anawajua wavutaji wa Shisha, Ugoro na Bangi na akaenda mbali zaidi kwa kuwatuhumu Jedhi la Polisi akiwemo Kamanda Ciro kuwa anawatetea watu hao kupokea dau la milioni 5 tano kutoka kila gwiji wa Shisha!
Lakini mbaya zaidi na kali kuliko ni hii ya juzi kuhsu madawa ya kulevya baada ya Makonda kuwatuhumu tena Polisi kuwa wahusika WAKUU WAKIWEMO POLISI 12!! Baada ya tamko hilo tulikna jinsi Mangu, Ciro na Polisi alivyohaha kujisafisha kwa kuwaksmata wenzao 12 harakaharaka!
Kwa kiongozi makini idara yako kutuhumiwa kuhusika na makosa makubwa ya jinai kama hili la Madawa ni aibu kubwa sana! Je, IGP na Kamanda wake wa Kanda Maalumu walikuwa wapi wakti vijana wao(askari)walipokuwa wakifanya haya madudu?
Kama Polisi wenyewe wanajihusisha na biashara hii au kuvuta tutegemee nini hapo?Jibu ni HAKUTAKUWA NA UFANISI WOWOTE!!!!!
Tunaomba JPM atengue uteuzi wa IGP Mangu na Kamanda Ciro maana tayari wamepoteza sifa za kuongoja Jesji la Polisi! Lakini pia JPM atengue uteuzi wa RC Makonda ampangie kazi nyingine kwa kutaka kuvuruga amani ya nchi kwa kuingilia mihimili isiyo muhusu. Nashauri Makonda APELEKWE CCP MOSHI AKAJIFUNZE UPOLISI KAZI INAYO ONEKANA KUMFAA NA SIYO UKUU WA MKOA!! Makonda kwa sasa ameanza kujifanya mungu mtu kwa kukashfu Jeshi la Polisi na Bunge la JMT lakini pia kuidhalilisha Ofisi ya Rais kwa kumhusisha Rais na ukiukwaji mkubwa wa Sheria na Katiba ya nchi! Rais ajue kuwa tayari Wabunge wote CCM na UKAWA wameungana Bungeni kutaka Makonda aitwe kujieleza mbele ya Kamati ya Sheria,Haki na Kinga!
Hii tayari ni kutangaza VITA KATI YA BJNGE NA SERIKALI na hii si hali nzuri kiutawala! Kama Rais atadndelea kumkingia kifua Makonda basi ajue anajiangamiza mwenyewe, CCM na Serikali yake!
Wasalaam.