IGP Mangu hawa ndo 'askari' wako!!

IGP Mangu hawa ndo 'askari' wako!!

Tazama vizuri mkuu, yupo askari mmoja tu hapo lakini kutokana na matukio ya hivi karibuni, hawa askari wa Mangu wanauwawa kirahisi rahisi, wananyag'anywa silaha kirahisi na wako nyoroyoro zaidi.
Halafu aliyebebwa hapo mtu mzima ni huyo askari , wengi neni wote watoto wa shule
Tazama vizuri picha.

Askari haimaniishi kila kitu anaweza askari wa kwenye movie sio wa kwenye maisha halisi msikurupuke tu mbona makomando wanauwawa sembuse polisi?
 
Ukiangalia picha unaona watoto tu na askari mmoja ndo kabebwa!
Ukweli ni nyoronyoro sana na aibu kwa geshi la polish.
Mbebaji alitakiwa kuangukia majini tu.
 
Sasa mkuu unataka aingie na viatu vya ngozi kwenye maji? Hayo maji unayajua yametoka wapi,una uhakika wa usalama wa hayo maji kwa afya ya ngozi? Huyo raia aliyembeba labda haijali afya yake....
 
Askari haimaniishi kila kitu anaweza askari wa kwenye movie sio wa kwenye maisha halisi msikurupuke tu mbona makomando wanauwawa sembuse polisi?

Askari polisi wamenyang'ang'anywa silaha tumebaki vinywa wazi!
Wameuwawa tuashangaa shangaa!
Sasa wanabebwa migingoni wewe hulioni tatizo.
Hivi wataka mpaka wavalishwe nepi hadharani ndo utaliona tatizo?
 
View attachment 249858
Malamiko ya askari nyoronyoro sasa yamejitokeza kuliko wakati mwingine wowote.

Pichani tujionee wenyewe somo la ukakamavu kama linavyotolewa CCP Moshi![/QUOTE

Mimi sioni kosa la huyo askari kwa kuwa alikua anakwenda ofisini.
Hakuja eneo hilo kufanya kazi ya uokoaji.

Ni vyema tufahamu kuwa kila sekta ina majukumu tofauti. Huyo askari anaweza akawa anafanya kazi za ofisini kama kuchapa barua na kuhifadhi mafaili.
Hawezi kujidumbukiza kwenye maji machafu wakati kuna kivuko cha sh.500/=.Akifika ofisini ananuka maji ya chooni ataonekana pia ni mtu wa ajabu.

Hata enzi za mababu zetu huo ndio uliokua usafiri.
Na watu waliajiriwa kwa ajili hiyo. Alipanda mgongoni kama usafiri mwengine wowote ambao ungekuwepo.
Hapo hakuna mtu aliyekua anaokolewa bali wote walikua wanalipa hela ili kukwepa kukanyaga maji machafu na kuharibu viatu.

Huyu askari analaumiwa bure wakati wamepita labda eneo hilo wamepita askari wengi wakiwa ndani ya magari yao huku wakiwa wamefunika vioo na hawakubeba mtu.

Au kosa la huyo askari ni kuwa na mshahara mdogo unaomfanya ashindwe kumiliki gari kama watu wengine au wezi,wala rushwa na mafisadi?
Kwa nini tusiangalie mazingira ya ulazima wa Yeye kuingia kwenye maji kama kweli ulikuwepo.

Hivi kama kweli tunaangalia maadiili ya polisi tungeanza na huyo aliyebebwa au tungeanza na wala rushwa ambao kulingana na jamii kuoza ndio wanaopata heshima kubwa huko uraiani kutokana na kuwa na hela za kufanya matanuzi.
Hivi askari kama amebebwa kama njia mojawapo ya usafiri anakuwa ameshirikije kwenye uhalifu mpaka IGP amfukuze kazi?
Hivi ni askari wangapi wanaotuhumiwa kwa vitendo vya rushwa na uhalifu na hata mali wanazomiliki haziendani na mishahara yao kabisa lakini bado wapo kazini na wengine ni viongozi wao wakubwa? Kwa nini tusiweke picha ya askari anayemiliki ghorofa ya milioni 800 wakati mshahara wake unajulikana kuwa ni mdogo ili tujadili badala yake tunahangaika na yule askari msafi wa unifom?
Je,tumewaandaaje askari wa nchi hii kwenye majanga ya mvua hasa kwenye sare zao ambazo mara nyingine wanavaa viatu vya kununua kwenye mitumba?

Hata mimi nimejibanza hapa karibu na mto mbezi nasubiri ili ajitokeze askari hasa mwanamke mzuri ili nimbebe nipate maujiko. Siwezi kumwacha askari mtanashati aingie kwenye maji wakati ninauwezo wa kumbeba ,tena nitambeba bure.
 
Kukubaliana na kuporomoka maadili ya kijeshi na laisszes faire katika jeshi la polisi ni dalili mbaya zaidi kwa vyombo vyetu vya ulinzi na usalama.
Kimsingi sina haja ya kubishana na mtu anayeridhika na uozo kama huu, maana ndo kiwango cha upeo waje maishani.
 
Wengine hawa hawa hapa
 
Attachments

  • 1431095384740.jpg
    1431095384740.jpg
    34.4 KB · Views: 101
Kuna ajenda gani,mbona multiple threads za mtu mmoja,na nyuzi haziungwi?
 
Back
Top Bottom