IGP Chonde chonde ujinga huu usitokee Mbeya!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

IGP Chonde chonde ujinga huu usitokee Mbeya!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by masopakyindi, Sep 4, 2012.

 1. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Tumeona matukio ya kusikitisha tokea mikutano ya CDM ilivyoanza kuanzia Morogoro na hata Iringa
  Serikali imetumia nguvu kubwa pasipo ulazima wowote bila kujali kuwa wanao umia ni Watanzania walipa kodi, wawe CHADEMA au vinginevyo.

  Amani tuliyozoea kuiimba kila siku haivunjwi na wananchi bali vyombo vya dola-kiashirio ambacho si kizuri kwa mustakabali wa nchi yetu.

  Mimi ni mwana CCM lakini kile ninachoona hakinipi faraja yoyote kama kuna utawala bora.Serikali nahisi imeingia kichwa kichwa katika mtego wa CDM na sidhani kama watatoka bila mikono ya baadhi ya viongozi kulowa damu.

  Ningependa kumwomba Kamanda IGP kwamba muendelezo wa kutumia maguvu bila akili sana sasa unapitiliza kuliko kiasi.

  Ni kwa nia hii hii njema ningemwomba ASITUMIE staili hii huko Mbeya maana vijana wa pale Mwanjelwa hawabipiki.
  Ukiwabipu watapiga kweli.
  Hatujasahau zile fujo za siku tatu nzima, ambazo zilizimwa na kauli tu ya Mhe Sugu.

  Sote tunapenda amani, lakini kwa mtindo huu wa Polisi amani nahisi haitachukua muda mrefu kusambaratika.
   
 2. m

  majebere JF-Expert Member

  #2
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Muhimu watu wawe na nidhamu na viongozi wao wafate sheria. Fujo hatutaki tena. Kama ni mkutano basi lazima ruhusa ya RPC, kama ni maandamano basi lazima ruhusa ya RPC na tutawachagulia maeneo ya maandamano lakini sio sokoni.
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Umechelewa sana kuliona hilo. CCM ndivyo mlivyo
   
 4. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,348
  Trophy Points: 280
  Mkuu kwa mtindo huu wa Polisi hata Mwenyekiti wa CCM sidhani kama anapata starehe moyoni kwa yanayotokea!
   
 5. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #5
  Sep 4, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Pamoja
   
 6. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #6
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kuanzia sasa hatuhitaji ruhusa ya polisi ili ikiwezekana watuue wote. Nani amewapa polisi kibali cha kuwa viranja wetu kwa kutumia risasi. Lilwalo na liwe sasa!
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Game ya sasa inahitaji mbinu za kisasa pia...bado tuko na mbinu ya zama za mawe.
   
 8. G

  Gongerfasil Member

  #8
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 96
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 25
  majebere huwa unafikiria kwa kutumia nini maana wewe ni mjinga sana vitu viko wazi wewe unaongea ujinga why killing people?hiyo kwako weweunaona sawa pumbavu saaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaana wewe
   
 9. Janjaweed

  Janjaweed JF-Expert Member

  #9
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 9,531
  Likes Received: 884
  Trophy Points: 280
  kukaa n kusononeka bila kufanya chochote ni udhaiffu
   
 10. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #10
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,333
  Likes Received: 1,796
  Trophy Points: 280
  Mkuu umesema sawa kabisa...hakuna aliyejuu ya sheria. Hata polisi wenyewe wanatakiwa kuzifuata sheria. Ipo siku tutajua kwanini kuna umuhimu wa kuhakikisha vyombo vya sheria vinakuwa sio sehemu ya siasa. Hizi za leo za kuua ni dalili zake tu ambazo kweli zinaleta huzuni.Sisi wengine hatukuzoea hayo
   
 11. m

  majebere JF-Expert Member

  #11
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  We jifariji na hayo maneno lakini utatulia tu, hii ndio bongo, Slaa alikataa kumtambua JK kama Rais,Slaa alisema hana imani na polisi na hawezi kukaa nao, Slaa alisema liwale na liwe mikutano itaendelea.
  Leo yuko wapi? Amekula matapishi yake na amefyata mkia.

  Sasa jiulize kama alie watuma amerudi rivasi je nyie mnaotumwa si mtakimbia kabisa?
   
 12. mwaJ

  mwaJ Tanzanite Member

  #12
  Sep 4, 2012
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 4,076
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Unaposema lazima rugusa ya RPC unatumia sheria gani? Hebu tuwekee hicho kifungu cha sheria kinachataka vyama vipewe ruhusa na polisi kabla ya kufanya mkutano au kuandamana!
   
 13. L

  Leodgard Member

  #13
  Sep 4, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Arusha NDIO kabisaaaa!!!! Wasijaribu!!
   
 14. m

  mamajack JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  mwenyekiti anafurahi sana,maana ndiyo ahadi aliyowaahidi wa tz wakati anaingia madarakani.
   
 15. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,986
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Kikatiba RPC hana ruhusa ya kuzuia mkutano wa chama chochote cha siasa, wanachofanya MRPC kwa kutumia sheria za kikandamizi, wanavunja katiba ya nchi hii tuipendayo ya Tanzania!!! Kama huamini ngoja wapelekwe The Hague waende wajitetee eti kuna uvunjifu wa amani tukauwa watu!!!! Kazi ya Polisi ni kulinda raia na mali zao zisiharibiwe, si kuuwa watu waliobeba mabango na matawi ya miti eti wamevunja amani!!!!

   
 16. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hee huna habari? mwenyekiti wa ccm hana hata habari ya haya matukio...yuko bize anashuhulikia trip yake ya UK hivi karibuni
   
 17. m

  mamajack JF-Expert Member

  #17
  Sep 4, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wewe kimeo,rpc anapewa taarifa ili apange watu wa kusimamia sio anaombwa ruhusa.shida yenu magamba mlikubali vyama vingi ili mpewe pesa na wazungu,hambkufikilia kuwa kuna watu watakuwa na upinzani wa kweli.chama cha siasa au watu wowote wanahaki ya kuandama au kufanya mkutano na nihaki yao kikatiba.
   
 18. m

  mgomba101 JF-Expert Member

  #18
  Sep 4, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,788
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Thubutu! chezea Mbeya wewe! kwa Mh sugu....sugu moto chini! ajaribu aone.
   
 19. m

  majebere JF-Expert Member

  #19
  Sep 4, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 4,521
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Sasa si fanyeni mambo yenu bila kupitia kwa RPC ndio mtaelewa nini nasema. Lazima ruhusa ya polisi na hilo linajulikana wazi.
   
 20. m

  mamajack JF-Expert Member

  #20
  Sep 4, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  sababu ni uchumia tumbo wa magamba kama wewe.
   
Loading...