IGP aunda tume sakata la utekaji nyara

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,299
33,080
MKUU WA JESHI la Polisi nchini, Saidi Mwema, ameunda tume maalum kwa ajili ya kuchunguza mauaji ya raia mmoja kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita katika tukio ambalo lilidaiwa kuwa ni jaribio la utekaji. Jeshi la Polisi lilitangaza juzi kuwa askari walimuua Octavian Kashita wakati akiwa na wenzake watatu walipokuwa wakijaribu kuwazuia polisi wasiwakamate katika jaribio lao la kumteka Bariki Minja.

Katika tukio hilo vijana watatu wengine waliokuwa pamoja na marehemu wakiwemo na aksari watano wanaendelea kushikiliwa na polisi kuhusiana na tukio hilo.

Mwema, alisema kuwa tume maalum imeundwa kuchunguza ukweli wa tukio zima la utekeji nyara na ukweli kuhusu askari wanaotuhumiwa kumuua raia huyo utajulikana mara baada ya tume hiyo kushughulikia na kutoa ripoti yake.

Tume hiyo imehusisha maofisa wa serikali wakishirikiana na Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam kuchunguza sakata zima kuhusiana na tukio hilo.

Alisema tume hiyo itachunguza “ mwananchi aliyepeleka taarifa za kutekwa kwa kaka yake zilikuwa za kweli na kama, ama alitoa taarifa za uongo? Na kama ikigundulika alitoa tarifa za uongo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake” alisema

“ Na je askari anayetuhumiwa kuua alifanya kwa bahati mbaya au la, au alitumia nguvu bila kutumia busara kufyatua risasi hiyo? Vyote vitajulikana katika uchunguzi huo” alisema.

Nae IGP Mwema hakuweza kutaja majina ya askari wanaohuska katika tukio hilo na kusema kuwa majina ya askari hao yatatolewa mara baada ya tume hiyo kukamilisha uchunguzi wake.


NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
 
Bwana, waacheni wafanye vyovyote vile alimradi wanaondoa hilo tatizo linalonyima watu usingizi, watu hata hatupati amani, haujui kama mtoto wako atarudi salama shule, kisa? kwasababu watu wanakuona kama una hela so watateka mwanao ili utoe hela, hii inakera ujue
 
Back
Top Bottom