NANCA
Member
- Jun 23, 2023
- 92
- 100
Haiwezekani yani haiwezekani, haiwezekani wazanzibar wawe na haki ya kutawala kote, Tanganyika na Zanzibar afu watanganyika tusiwe na haki ya kutawala Zanzibar, sa huo ndo muungano gani wa kinyonyaji, hiyo hapana na hatutaki tena.
Leo hii watanganyika tunapigwa mande, kule kwao visiwani ni mzanzibar na huku tanganyika ni mzanzibar kwa kivuli cha Tanzania, Kiasi kwamba Kama Rais anakasumba ya udokozi na ujanjaujanja kwa katiba hii inayompa umungu si anaweza kuiba Tanganyika na akapeleka kwao Zanzibar kwa kigezo cha muungano na utanzania?
Kama Hayati Magufuli aliweza kupeleka chato kwa kigezo cha kote ni Tanzania, huyu anashindwaje kufanya hvyo kwa kigezo cha Tanzania na utetezi wa chawa wake?
-Kama mnautaka muungano basi tukubaliane yafuatayo:
1. Kwa muundo huu tulionao wa bila Tanganyika, basi Rais wa Zanzibar atoke popote, yaani awe mtanganyika au mzanzibar na rais wa Tanzania iwe kama ilivyo sasa.
2. Watanganyika wawe na haki sawa katika umiliki wa ardhi kama ilivyo kwa wazanzibar huku bara.
3. Au Zanzibar ifutwe Kama ilivyofutwa tanganyika na ibaki Tanzania na Rais awe mmoja ambae atapigiwa kura na watu wote wenye sifa nchi nzima.
Kwa tafsiri kwamba Zanzibar iwe Kama mkoa au kitongoji cha Tanzania, isiwe na serikali yake yenyewe.
4. Kama hamtaki vyote basi muungano katika mambo ya kisiasa ikiwemo kushea marais na mawaziri ufe, hivyo Tanganyika iwe na Rais wake na Zanzibar iwe na Rais wake na tushirikiane kwa kuunda jumuiya ambayo itaainisha mambo ya kushirikiana.
NOTE: Ni unyonge na ujinga kwa watanganyika kukubali kutawaliwa na mzanzibar ili hali wazanzibar hawataki kutawaliwa na watanganyika.
Haikubaliki Rais wa Zanzibar awe mzanzibar tu afu Rais wa tanganyika awe yeyote kwa kivuli cha Tanzania. Katika hili Nyerere alitukosea sana hasa kwa kuwadekeza wazanzibar, kuwaonea aibu na kudhani mfumo utakua vilevile Kama alivyoufikiria yeye.