Ife ana Frelimo - Samora Machel

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,275
24,141

Wimbo huu kwa hisani ya emwandosya wa YOUTUBE:

Inatukumbusha jinsi Tanzania ilipokuwa kimbilio la wanamapinduzi wakaweka makazi yao Tanzania mfano Samora Machel, Eduardo Mondlane n.k na wazazi wangu waliupenda sana wimbo huu naambiwa ikiwemo Mzee Moses Mnauye na watoto wa halaiki.
 
Last edited by a moderator:
I don't know. It just does

Haikutokei wewe kusikia labda ala tupu za muziki au nyimbo bila ya kujua maana na ikakufanya sad? Na mbaya yake nakuwa siwezi kuizima mpaka niisikie yote (@-@)

Mimi ni vice versa naupenda sana wimbo huu, kama wewe nikiusikia basi sitaki kuishia kati husubiri hadi uishe huwa unanikumbusha Samora Machel kiongozi ambaye nilimpenda sana baada ya Mwalimu. Kuna nyimbo hasa za ala tupu nikisikia huwa sitaki niondoke mpaka ziishe hasa za yule Andrea Bocelli.
 
Huu wimbo umeelekea kama upigwe kwenye mazishi hivi au watoto wanaokufa njaa. Hiyo ndo image nnayopata nikiusikia

Sina uhakika lakini inaweza kuwa mara ya kwanza kuniingia akilini ilikuwa alipokufa Samora Machel kwa hiyo nauhusisha na vifo na sadness
 
  • Thanks
Reactions: BAK

Sijui maana ya wimbo huu na pia sidhani kama huu ni wimbo wa Taifa la Msumbiji ila ulikuwa unawahamasisha sana Wanamsumbiji waliokuwa wanapambana ili kupata uhuru wao na pia uliwahamasisha Watanzania wengi sana katika kuwasaidia Wanamsumbiji wawe huru. Nadhani siku aliyokufa Samora vipindi vyote RTD vilisimamishwa na kukawa na nyimbo za maombolezi tu na huu wimbo nadhani ulipigwa mara nyingi sana katika kipindi chote cha maombolezi. Sijui kama kuna Rais mwingine wa Afrika ambaye Watanzania wengi walimpenda sana kama Samora.
 
[video]http://www.firstpost.com/topic/organization/frelimo-dia-de-la-independencia-de-mozambique-video-b1AUc-OGIWs-76003-1.html[/video]
Ife = sisi
ana= watoto/wana
Frelimo = Frente de Libertação de Moçambique (Mozambique[FONT=arial, sans-serif] Liberation Front).[/FONT]
Zowoona[FONT=arial, sans-serif] = Tumeona [/FONT]
[FONT=arial, sans-serif] [/FONT]
[FONT=arial, sans-serif]Frelimo, ya wina, Frelimo ya wina, Zowona, [/FONT]Tina pata ku- Mozusambiki = Frelimo imeshinda,...Frelimo, imeshinda, uhuru tumeupata Mozambigue x2.
 
Last edited by a moderator:
Huu wimbo unanikumbusha miaka ile ya wapiganaji wa ukombozi kusini mwa africa. Sweet memories
 
..duh! mmenikumbusha mbali sana.

..wa-Tanzania walimpenda sana Samora.

..nakumbuka kuna sherehe za uhuru au mei mosi alihutubia national stadium kwa zaidi ya masaa 3.

..alikuwa anapenda kutoa hotuba na kuikatisha kwa wimbo!!

..nakumbuka nyimbo nyingine za Zambia kama ule "tilute Zambezi ndi mtima umoo" na mwingine "....zambia lelo..."
 
Wimbo huu kwa hisani ya emwandosya wa YOUTUBE:

Inatukumbusha jinsi Tanzania ilipokuwa kimbilio la wanamapinduzi wakaweka makazi yao Tanzania mfano Samora Machel, Eduardo Mondlane n.k na wazazi wangu waliupenda sana wimbo huu naambiwa ikiwemo Mzee Moses Mnauye na watoto wa halaiki.

Huu wimbo unanikumbusha mbali sana wakati wa ukombozi kusini mwa Afriika.
 
masopakyindi ,

..Samora Machel alikufa October 19, 1986.

..sasa hivi kuna video clips nyingi zinazomhusu Samora Machel ziko kwenye mtandao.
Ni kweli mkuu sisi tuliosoma kitambo.
Mwaka 1970~1975, vita ya Msumbiji ilipamba moto sana, hadi Uhuru ulipopatikana 1975.
Tukiwa wanafunzi tumeimba nyimbo hizo za kimapinduzi.
 
Nikiwakumbuka hawa wazalendo wa kweli,harafu nikalingnisha na wazalendo wa mwendokasi wa sasa HV,roho yangu inapata tabu sana,wa sasa HV ni wazalendo maslahi binafsi,
 
..hivi tatizo ni macho yangu, au?

..kwamba uzi huu uko kwenye jukwaa la " "entertaiment"!!

Cc masopakyindi , Nguruvi3
Mkuu MODS watoto wa juzi.
Tunachojadili inaelekea aidha hawakijui au ni historia iliyowapita.

Sisi wengine tukisikia kina Samora Machel, Josina Machel, Eduardo Mondlane, Marcelino Dos Santos, ZJoachim Chissano, Mapande na wengine wengi, damu za kimapinduzi zinachemka tukikumbuka ujana wetu wa 60/70's.
 
..hapo naamini ulimaanisha Alberto Chipande.

..umemsahau Sabastio Mabote.

..na Raimundo Pachinuapa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom