Saidama
JF-Expert Member
- Jun 10, 2022
- 501
- 946
Vijana katika safari yetu hii ngumu tuliyonayo sasa. Cha kwanza tupunguze matarajio hivyo tutapunguza presha na tutafanya mambo kwa hatua na tutafanikiwaSalaam....
Baada ya utafiti wangu wa muda kwenye soko la forex nimekuja na vitu ambacho naamini vinaweza kuwa ni msaada mkubwa sana kwa wapambanaji wenzangu wanaotaka kubadilisha mifumo ya maisha yao kwa fursa mbalimbali zinazojitokeza kutokana na kukua kwa technolojia.
Asilimia 90% ya watanzania tumeishi kwa mtazamo wa kwamba ndoto kubwa tunazotakiwa kuwa nazo ni kusoma na kuja kuajiriwa hasa hasa serikalini na kwa asilimia chache wapo ndoto zao ni kuajiriwa mashirika binafsi na tunaamini mafanikio yamejificha huko hii hali imeangamiza familia nyingi sana na imezalisha watu wengi sana wasiojielewa na izo fikra zimewafanya wazee wetu waendelee kuamini kua heshima pekee na mafanikio ni mwanae kuajiriwa bila kuangalia nafasi zilizopo kwenye ajira na idadi ya wahitaji ni wengi mno.
Sasa basi kurahisisha maisha vijana wengi tumejikuta tunazivaa fursa mbali mbali tunazoamini zitatuletea unafuu wa maisha kama vile kubet football, kubashiri michezo mbalimbali mitandaoni kama biko n.k sio kwamba zilikua ndoto zetu hapana hatuna namna system imetupeleka uko.
Turudi kwa wadau wangu wa forex trading wale beginers na wale wazoefu kuna jambo nataka tuwekane sawa apa na lengo ni kusaidiana sisi sote ni wamoja tunatakiwa tuwe pamoja katika kupambana na hali ngumu za maisha, binafsi naijua hii biashara tokea 2016 mwishoni nimeshapata pesa kutokana hii biashara na nimeshapoteza pesa kutokana na hii biashara, nishagombana na watu na sio kwamba kuwepo muda mrefu kwenye soko ndo mafanikio hii kitu haifanyi kazi ivo tunakosea sana kuliendea hili soko inatakiwa tubadilishe mitazamo yetu na kikubwa ninachoamini soko lina pesa ni namna ya kuzichukua ndo inahitaji mbinu za uhalisia.
Tunachokosea sisi ni kitu kimoja tunatamani tulale masikini tuamke matajiri ndugu zangu kila kitu kina level hata kukua kiuchumi ni lazima upite level mbali mbali lazima uanzie chini ili uende juu nayasema haya sio kwamba nina mafanikio makubwa sokoni nayasema haya kwa experience ya mistake mbalimbali nilizopitia na kugundua kuwa natakiwa nifanye nini na atleast sikosi pesa ya kula kupitia hii biashara na lengo ni hilo tuanze kwanza level ya chini yani usikose pesa ya kula elfu 10, 20, 30 zisikupige chenga kwa siku au siku mbili
Huna haja ya kutamani kutengeneza kiwango kikubwa cha pesa kwa muda mfupi au kwa kumuangalia mtu aliyefanikiwa kupitia hii biashara ukalazimisha uwe kama yeye unapaswa kuiendea biashara taratibu yani ifanye kama biashara zingine kwanza mambo mazuri yatakuja yenyewe na hivi ni vitu vya msingi unapaswa kuvizingatia:-
1. UNAPASWA KUJUA LEVEL YAKO KIUCHUMI
Yani hapa unatakiwa ujijue wewe ni nani unahali gani, mambo gani yamekuzunguka, una kiasi gani cha pesa na unatakiwa kuanzia wapi jua kabisa unafanya kwaajili ya nani usimuangalie mtu yeyote na ukataka kushindana nae labda umuangalie mtu kwa lengo lakujifunza au akupe motivation na hapa kuna mambo ya saikolojia yataingia sitayagusa kwa sasa ila ntawagusa watu wenyr level ya chini kama vijana wenzangu ambao hawana kazi wala biashara yakuwaingizia kipato
Unapoingia kwenye soko la forex usilazimishe kuwa tajiri mara moja hayo mawazo yatakucost na utaiona hii biashara ni mbaya siku zote
Ingia sokoni kwa kutafuta elfu 10 tu kwa siku
Yani hakikisha kwa siku unaingia order 7 tu na kila moja ikupatie $ 0.65
$0.65 = tsh 1500
1500 × 7 = 10500
Tsh 10500/= kwa siku ni kitu rahisi sana kukipata traders mnajua ilo, so hutokua na haja yakuwa omba omba kuwapiga watu mizinga hata pesa za vocha utaanza kukua taratibu kiuchumi ukijua unaweza kuingiza hata elfu 10 kwa siku.
2. UNAPASWA KUWA NA PLAN
Hii kitu muhimu sana unatakiwa ujue namna yakuandaa plan yako kutokana na kiwango cha pesa yako na unatakiwa ujue namna gani yakuifata na kuilinda plan yako siku zote
Sitoweza kuweka plan hapa kila mtu ana uchumi wake ila unapaswa kuandaa plan hata uwe na $5
Hupaswi mtu ukae kizembe tafuta namna yakupambana na umasikini
Nitaendelea nilipoishia...