Ifanye forex kuwa biashara yakukuingizia kipato kidogo kila siku

Moneytwister

JF-Expert Member
Jul 22, 2022
301
990
Salaam....

Baada ya utafiti wangu wa muda kwenye soko la forex nimekuja na vitu ambacho naamini vinaweza kuwa ni msaada mkubwa sana kwa wapambanaji wenzangu wanaotaka kubadilisha mifumo ya maisha yao kwa fursa mbalimbali zinazojitokeza kutokana na kukua kwa technolojia.

Asilimia 90% ya watanzania tumeishi kwa mtazamo wa kwamba ndoto kubwa tunazotakiwa kuwa nazo ni kusoma na kuja kuajiriwa hasa hasa serikalini na kwa asilimia chache wapo ndoto zao ni kuajiriwa mashirika binafsi na tunaamini mafanikio yamejificha huko hii hali imeangamiza familia nyingi sana na imezalisha watu wengi sana wasiojielewa na izo fikra zimewafanya wazee wetu waendelee kuamini kua heshima pekee na mafanikio ni mwanae kuajiriwa bila kuangalia nafasi zilizopo kwenye ajira na idadi ya wahitaji ni wengi mno.

Sasa basi kurahisisha maisha vijana wengi tumejikuta tunazivaa fursa mbali mbali tunazoamini zitatuletea unafuu wa maisha kama vile kubet football, kubashiri michezo mbalimbali mitandaoni kama biko n.k sio kwamba zilikua ndoto zetu hapana hatuna namna system imetupeleka uko.

Turudi kwa wadau wangu wa forex trading wale beginers na wale wazoefu kuna jambo nataka tuwekane sawa apa na lengo ni kusaidiana sisi sote ni wamoja tunatakiwa tuwe pamoja katika kupambana na hali ngumu za maisha, binafsi naijua hii biashara tokea 2016 mwishoni nimeshapata pesa kutokana hii biashara na nimeshapoteza pesa kutokana na hii biashara, nishagombana na watu na sio kwamba kuwepo muda mrefu kwenye soko ndo mafanikio hii kitu haifanyi kazi ivo tunakosea sana kuliendea hili soko inatakiwa tubadilishe mitazamo yetu na kikubwa ninachoamini soko lina pesa ni namna ya kuzichukua ndo inahitaji mbinu za uhalisia.

Tunachokosea sisi ni kitu kimoja tunatamani tulale masikini tuamke matajiri ndugu zangu kila kitu kina level hata kukua kiuchumi ni lazima upite level mbali mbali lazima uanzie chini ili uende juu nayasema haya sio kwamba nina mafanikio makubwa sokoni nayasema haya kwa experience ya mistake mbalimbali nilizopitia na kugundua kuwa natakiwa nifanye nini na atleast sikosi pesa ya kula kupitia hii biashara na lengo ni hilo tuanze kwanza level ya chini yani usikose pesa ya kula elfu 10, 20, 30 zisikupige chenga kwa siku au siku mbili

Huna haja ya kutamani kutengeneza kiwango kikubwa cha pesa kwa muda mfupi au kwa kumuangalia mtu aliyefanikiwa kupitia hii biashara ukalazimisha uwe kama yeye unapaswa kuiendea biashara taratibu yani ifanye kama biashara zingine kwanza mambo mazuri yatakuja yenyewe na hivi ni vitu vya msingi unapaswa kuvizingatia:-

1. UNAPASWA KUJUA LEVEL YAKO KIUCHUMI
Yani hapa unatakiwa ujijue wewe ni nani unahali gani, mambo gani yamekuzunguka, una kiasi gani cha pesa na unatakiwa kuanzia wapi jua kabisa unafanya kwaajili ya nani usimuangalie mtu yeyote na ukataka kushindana nae labda umuangalie mtu kwa lengo lakujifunza au akupe motivation na hapa kuna mambo ya saikolojia yataingia sitayagusa kwa sasa ila ntawagusa watu wenyr level ya chini kama vijana wenzangu ambao hawana kazi wala biashara yakuwaingizia kipato

Unapoingia kwenye soko la forex usilazimishe kuwa tajiri mara moja hayo mawazo yatakucost na utaiona hii biashara ni mbaya siku zote

Ingia sokoni kwa kutafuta elfu 10 tu kwa siku

Yani hakikisha kwa siku unaingia order 7 tu na kila moja ikupatie $ 0.65

$0.65 = tsh 1500

1500 × 7 = 10500

Tsh 10500/= kwa siku ni kitu rahisi sana kukipata traders mnajua ilo, so hutokua na haja yakuwa omba omba kuwapiga watu mizinga hata pesa za vocha utaanza kukua taratibu kiuchumi ukijua unaweza kuingiza hata elfu 10 kwa siku.

2. UNAPASWA KUWA NA PLAN
Hii kitu muhimu sana unatakiwa ujue namna yakuandaa plan yako kutokana na kiwango cha pesa yako na unatakiwa ujue namna gani yakuifata na kuilinda plan yako siku zote

Sitoweza kuweka plan hapa kila mtu ana uchumi wake ila unapaswa kuandaa plan hata uwe na $5

Hupaswi mtu ukae kizembe tafuta namna yakupambana na umasikini

Nitaendelea nilipoishia...
 
Order 7 0.65 sasa unatrade unacheza hata scalper hawezi trade hivyo anyway. Shusha uzi.
Om boy 0.65 unaiona ndogo sana... Yani kuingiza tsh 1500 kwa trade 1 unaona mchezo nimependa kwasababu umegundua kumbe ni kitu rahis sana ofcoz ni simple tuishi umo ukifanya 0.65x7 una tsh10000/= apo ni vichwa 10 kwa boda boda yani abiria wa buku buku utanielewa tu na kama unataka kujilipua huu uzi haukuhusu endelea na stress za kublow account ila kama unajua kufanya biashara tutaenda sawa
 
achana na iyo forex inahitaji mtaji join hapa jishighilishe online pata pesa link iyo apo
 
Sas nataka kuingia kwenye hii biashara Ila cjui chochote kuusu haya Mambo cjui mtaji kiasi gani na weza Anza Ila Kama Kuna mdau atakaye nisaidia 0627151094 hiyo kwa WhatsApp tu
 
Om boy 0.65 unaiona ndogo sana... Yani kuingiza tsh 1500 kwa trade 1 unaona mchezo nimependa kwasababu umegundua kumbe ni kitu rahis sana ofcoz ni simple tuishi umo ukifanya 0.65x7 una tsh10000/= apo ni vichwa 10 kwa boda boda yani abiria wa buku buku utanielewa tu na kama unataka kujilipua huu uzi haukuhusu endelea na stress za kublow account ila kama unajua kufanya biashara tutaenda sawa
Kama unafunga na 0.65 stop loss unaweka pips ngapi?? Nilikua nablow acc mwaka 2020 sasa hivi hata usd 10 siwezi ichoma kaka. I snipe kama jina langu.
 
Salaam....

Baada ya utafiti wangu wa muda kwenye soko la forex nimekuja na vitu ambacho naamini vinaweza kuwa ni msaada mkubwa sana kwa wapambanaji wenzangu wanaotaka kubadilisha mifumo ya maisha yao kwa fursa mbalimbali zinazojitokeza kutokana na kukua kwa technolojia.

Asilimia 90% ya watanzania tumeishi kwa mtazamo wa kwamba ndoto kubwa tunazotakiwa kuwa nazo ni kusoma na kuja kuajiriwa hasa hasa serikalini na kwa asilimia chache wapo ndoto zao ni kuajiriwa mashirika binafsi na tunaamini mafanikio yamejificha huko hii hali imeangamiza familia nyingi sana na imezalisha watu wengi sana wasiojielewa na izo fikra zimewafanya wazee wetu waendelee kuamini kua heshima pekee na mafanikio ni mwanae kuajiriwa bila kuangalia nafasi zilizopo kwenye ajira na idadi ya wahitaji ni wengi mno.

Sasa basi kurahisisha maisha vijana wengi tumejikuta tunazivaa fursa mbali mbali tunazoamini zitatuletea unafuu wa maisha kama vile kubet football, kubashiri michezo mbalimbali mitandaoni kama biko n.k sio kwamba zilikua ndoto zetu hapana hatuna namna system imetupeleka uko.

Turudi kwa wadau wangu wa forex trading wale beginers na wale wazoefu kuna jambo nataka tuwekane sawa apa na lengo ni kusaidiana sisi sote ni wamoja tunatakiwa tuwe pamoja katika kupambana na hali ngumu za maisha, binafsi naijua hii biashara tokea 2016 mwishoni nimeshapata pesa kutokana hii biashara na nimeshapoteza pesa kutokana na hii biashara, nishagombana na watu na sio kwamba kuwepo muda mrefu kwenye soko ndo mafanikio hii kitu haifanyi kazi ivo tunakosea sana kuliendea hili soko inatakiwa tubadilishe mitazamo yetu na kikubwa ninachoamini soko lina pesa ni namna ya kuzichukua ndo inahitaji mbinu za uhalisia.

Tunachokosea sisi ni kitu kimoja tunatamani tulale masikini tuamke matajiri ndugu zangu kila kitu kina level hata kukua kiuchumi ni lazima upite level mbali mbali lazima uanzie chini ili uende juu nayasema haya sio kwamba nina mafanikio makubwa sokoni nayasema haya kwa experience ya mistake mbalimbali nilizopitia na kugundua kuwa natakiwa nifanye nini na atleast sikosi pesa ya kula kupitia hii biashara na lengo ni hilo tuanze kwanza level ya chini yani usikose pesa ya kula elfu 10, 20, 30 zisikupige chenga kwa siku au siku mbili

Huna haja ya kutamani kutengeneza kiwango kikubwa cha pesa kwa muda mfupi au kwa kumuangalia mtu aliyefanikiwa kupitia hii biashara ukalazimisha uwe kama yeye unapaswa kuiendea biashara taratibu yani ifanye kama biashara zingine kwanza mambo mazuri yatakuja yenyewe na hivi ni vitu vya msingi unapaswa kuvizingatia:-

1. UNAPASWA KUJUA LEVEL YAKO KIUCHUMI
Yani hapa unatakiwa ujijue wewe ni nani unahali gani, mambo gani yamekuzunguka, una kiasi gani cha pesa na unatakiwa kuanzia wapi jua kabisa unafanya kwaajili ya nani usimuangalie mtu yeyote na ukataka kushindana nae labda umuangalie mtu kwa lengo lakujifunza au akupe motivation na hapa kuna mambo ya saikolojia yataingia sitayagusa kwa sasa ila ntawagusa watu wenyr level ya chini kama vijana wenzangu ambao hawana kazi wala biashara yakuwaingizia kipato

Unapoingia kwenye soko la forex usilazimishe kuwa tajiri mara moja hayo mawazo yatakucost na utaiona hii biashara ni mbaya siku zote

Ingia sokoni kwa kutafuta elfu 10 tu kwa siku

Yani hakikisha kwa siku unaingia order 7 tu na kila moja ikupatie $ 0.65

$0.65 = tsh 1500

1500 × 7 = 10500

Tsh 10500/= kwa siku ni kitu rahisi sana kukipata traders mnajua ilo, so hutokua na haja yakuwa omba omba kuwapiga watu mizinga hata pesa za vocha utaanza kukua taratibu kiuchumi ukijua unaweza kuingiza hata elfu 10 kwa siku.

2. UNAPASWA KUWA NA PLAN
Hii kitu muhimu sana unatakiwa ujue namna yakuandaa plan yako kutokana na kiwango cha pesa yako na unatakiwa ujue namna gani yakuifata na kuilinda plan yako siku zote

Sitoweza kuweka plan hapa kila mtu ana uchumi wake ila unapaswa kuandaa plan hata uwe na $5

Hupaswi mtu ukae kizembe tafuta namna yakupambana na umasikini

Nitaendelea nilipoishia...
Bado hujaijui Forex vizuri. How Do you get profit everyday. Huo ni uongo.

Forex watu wanatrade set up yenye entry point na exit.

Set up 7 Kwa siku unazipataje. Labda uwe scalper strategy yenye stress na utakaa Kwa PC siku nzima.

Forex ni psychology 90% ukipata strategy ambavyo itakaa siku kadhaa hata wiki bila kuclose position hapo umeshaiva.

Kusoma Forex ni rahisi Sana tatizo ni akili zetu hata strategy iwe nzuri namna gani kama akili haijakaa Sawa Tamaa na hofu lazima upate hasara.
 
Kama unafunga na 0.65 stop loss unaweka pips ngapi?? Nilikua nablow acc mwaka 2020 sasa hivi hata usd 10 siwezi ichoma kaka. I snipe kama jina langu.
sniper 0.65 rahis kupata hata kama upo wrong market is wave machine ina move up and down kama upo vizuri kweny price action (ICT) market maker method au supply and demand utajua namna yaku pull triger sio lazima uwe kwenye ratio 1:5 sometimes 1:1 ni poa chamsingi kuwa consistent.

Unaweza weka SL sehem ambayo haiwezi kufikiwa kutokana na sehemu uliyo ingia we si sniper unaelewa ila mimi hata nisipo weka SL im sure 100% sikosi 1500 kwa kila order ntakayoingia na nimeona urahisi wa biashara hata nikifunga hesabu kwa mwezi naona profit

Do not trade without stop loss
 
We jamaa wewe unataka watu waugue cataract kwa kukodolea macho maskrini ya simu
 
Acha kuwapotosha watu FX sio rahisi kiivyo braza.

Nyie ndio mnaitia nuksi hii industry.

Narudi kusema forex ni ngumu ngumu ngumu lakini inawezakana kuifanya.

Mnawaza pesa tu ila sio yaliyo kwenye hio biashara.

Mtu Hana ujuzi anaweza Hela zake Rehani anapigwa za uso na soko anakuja liialia.

Jamani eeh forex sio easy kiivyo

Kama hujadhamiria kweli kweli Hela Yako kafanye mitikasi mingine usije ukapoteza kizembe.

Forex is not for everyone.tuelewane wadau.
 
sniper 0.65 rahis kupata hata kama upo wrong market is wave machine ina move up and down kama upo vizuri kweny price action (ICT) market maker method au supply and demand utajua namna yaku pull triger sio lazima uwe kwenye ratio 1:5 sometimes 1:1 ni poa chamsingi kuwa consistent.
Unaweza weka SL sehem ambayo haiwezi kufikiwa kutokana na sehemu uliyo ingia we si sniper unaelewa ila mimi hata nisipo weka SL im sure 100% sikosi 1500 kwa kila order ntakayoingia na nimeona urahisi wa biashara hata nikifunga hesabu kwa mwezi naona profit

Do not trade without stop loss
Basi umetisha mkuu. Mimi sifiki hiyo profit trade zangu ni hapo kwa hapo sl pips 3 mpaka 10 so kama niko wrong inapigwa fasta niko nje.
Zamani yah niliwahi fanya hivyo unafika hata usd 100 kwa wiki unafunga tu na 0.50 au 60 unatoboa.
 
Forex sio ngumu na sio rahisi, Chukulia jana mfano kulikuwa na taarifa nyingi saba za Uchumi hasa Ulata maana yake walio kuwa wana sale EURO jana watakwa kwa sasa wanachekelea make Euro jana ili nyanyaswa mbaya na kibaya zaidi zile ncbi za ulaya zilikuwa zinapishana kama lisaa kutoa taarifa na mbaya taarifa zote zikawa mbaya.

Nilicho jifunza Forex pia ni kucheza na taarifa za habari zile zina impact ya kutisha make zile ndo either upige pesa au uunguze account.

Siku kama ya jana niliivulia kofia Fundamental analysisi
 
Acha kuwapotosha watu FX sio rahisi kiivyo braza.

Nyie ndio mnaitia nuksi hii industry.

Narudi kusema forex ni ngumu ngumu ngumu lakini inawezakana kuifanya.

Mnawaza pesa tu ila sio yaliyo kwenye hio biashara.

Mtu Hana ujuzi anaweza Hela zake Rehani anapigwa za uso na soko anakuja liialia.

Jamani eeh forex sio easy kiivyo

Kama hujadhamiria kweli kweli Hela Yako kafanye mitikasi mingine usije ukapoteza kizembe.

Forex is not for everyone.tuelewane wadau.
Nazani hata kama hajui soko still anaweza kula kama anaweza kuliwa hata kula inawezekana sana.
Sioni cha ajabu sana Forex tuna liwa some time kizimbe sana.

Sasa mfano una subilia taarifa my be ya hali ya Uchumi wa Ulaya taarifa ikitoka tu unaingia sokoni kwa nini usile hata kama hujui Forex?

Mimi mwanzo ndo nilivyo kuwa nafanya, nilikuwa sana si trade hadi nijue kuna nini, kuna wakati ilikuwa inatoka taarifa ndo naingia sokoni na piga hadi Dola 100 then na left hata siku mbili sionekani.
 
Sas nataka kuingia kwenye hii biashara Ila cjui chochote kuusu haya Mambo cjui mtaji kiasi gani na weza Anza Ila Kama Kuna mdau atakaye nisaidia 0627151094 hiyo kwa WhatsApp tu

Jipe muda kujifunza. Soma soma angalia YouTube video. Fungua demo Hadi ifike hatua yaani wewe na market ni rafiki.

Forex ni ngumu sana. Ukishindwa kukucontrol mind na msukumo wa kupata pesa loss zitakufata. Jifunze kwa pair 3 tuu itakupa utulivu na kuingnore kelele

Ushauri wa kijana la saba B
 
Back
Top Bottom