Ifahamu Scandal ya IPTL na namna Singasinga, CCM na Serikali walivyoliibia taifa

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
1.Ifahamike kwamba ufisadi wa escrow akaunti msingi wake ni mkataba wa kifisadi wa IPTL uliosainiwa mwaka 1995 kufuatia tatizo la umeme mwaka1994 ambapo ilitakiwa umeme wa dharula ndipo IPTL ikasaini mkataba wa miaka20(1995-2015)..na wamiliki wa kampuni hiyo ya IPTL walikuwa Mechmar ya malaysia mwenye 70% na VIP ya Tz yenye 30% na kwa mujibu wa mkataba tanesco na IPTL walikubaliana kuwa muamuzi wa mwisho kuhusu mgogoro baina yao ni baraza la usuluhishi la migogoro ya kiuwekezaji (international centre for settlement of investment disputes-ICSID)

2. Kosa la kwanza IPTL haikuweza kukamilisha mradi wake 1995 kwenye kipindi cha dharula na badala yake ikakamilisha mwaka 1998. Hii ilikuwa kosa

2. Baada ya kumaliza mwaka1998 IPTL ililalamikiwa na tanesco ICSID kwamba imekuza gharama za uwekezaji na hivyo kukuza gharama za umeme.mwaka 2001 uamuzi wa ICSID ukatoka ikabainika ni kweli IPTL ilikuza gharama kwa kiasi cha dola 27milioni. Hili ni kosa kubwa.

3. Mwaka 2002 IPTL ikanza kuuzia umeme tanesco lakn mwaka 2004 tanesco ikabaini kuwa IPTL ilidanganya kuhusu mtaji. IPTL ilisema 30% ya mtaji ilikuwa nao kama equity sawa na dola 36milion na kwamba 70% ilikopa. Lakn bada ya ukaguzi ikabainika kuwa IPTL haikuweka dola 36milion kama equity bali dola 50 ambapo kwa exchange rate ya wakati huo ya 1:1000, dola50 ilikuwa sawa na tsh elfu50 ambazo hata fundi baiskeli angeweza kuwekeza. Hili ni kosa.

4. Kutokana na kasoro iyo tanesco ikataka gharama ya umeme (tarrif) ishuke kwasababu bei ilizingatia equity ya dola 36milioni kumbe ni sh50000. Mabishano yakaendelea mpaka 2006.

5. Mwaka 2006 serikali na tanesco ikashinikiza ifunguliwe akaunt maalumu (escrow)ili malipo yawekwe huko mpaka mgogoro utapokwisha kuhusu bei sahh ndipo pesa hiyo igawanywe kwa kuzingatia bei sahh baina ya pande mbili ndio mana ilikuwa kosa Pinda kusema pesa yote ya escrow eti ni ya IPTL kabla ya uamuzi kuhusu bei haujafikiwa

6.mwaka 2008 IPTL iliposhindwa kujiendesha ikawekwa chini ya receivership chini ya RITA ambapo ni RITA ikawa inasimamia gharama za uendeshaji

7.mwaka 2013 September ikatoka hukumu ya mahakama kuu chini ya Jaji Utamwa ilojichanganya baada ya VIP mwenye 30% kushtaki na kutaka IPTL iondolewe chini ya receivership na mali zote za IPTL ipewe kampuni ya PAP ya singasinga anaitwa Sethi.hukumu iyo ikaenda mbali na kusema singasinga huyo mwenye rekodi mbaya ya ufisadi tangu Kenya aliposhiriki ufisadi mkubwa mwaka 2002 wa Goldenberg scandal ilokiangusha chama cha KANU chini ya Moi na asiye na rekodi yoyote ya uwekezaji ktk umeme eti mahakama ikasema atazalisha 500MW na kwamba atauzia umeme tanesco kwa bei nafuu ya dola cent6 mpaka8 kwa unit.hukumu iyo inamua ivyo wakati ikijua kuwa mmiliki wa asilimia70 ya IPTL yuko chini ya liquadation Malaysia na zaidi ICSID kuna kesi inayohusu mgogoro wa IPTL na serikali uliofunguliwa na standard chartered bank ambayo ilinunua deni la IPTL mwaka 2005 na ikaruhusiwa kuishtaki serikali ya Tanzania kwenye baraza hilo lenye mamlaka ya mwisho.

8.Hukumu ya Jaji utamwa haikujua kuwa hoja ya biashara kwa maana ya bei na kiasi cha umeme ambao tanesco itanunua kwa IPTL sio kazi ya mahakama bali ni makubaliano ya tanesco kwa kutegemea mahitaji..na zaidi mwanahisa mkubwa alikuwa under liquidation malaysia na zaidi kulikuwa na kesi ICSID

9.pamoja ya Jaji Utamwa kudai mali zote za IPTL ipewe kampuni ya singasinga ya PAP bado ieleweke kuwa pesa za escrow hazikuwa mali ya IPTL kwakua uamuzi kuhusu mgogoro wa bei haukuwa umefanywa kokote na zaidi ulikuwa unasubilia hukumu ya ICSID

10. Mwaka 2014 Feb, ICSID ilifanya uamuzi wa awali kwamba ni kweli IPTL ina overcharge tanesco na kuelekeza pande mbili zikafanye hesabu upya ndani ya siku90 zilizoisha may2014.

11. Msingi wa hukumu ile ungesaidia kujua ni kwa kiasi gani iptl imeibia tanesco tangu 2002 mpaka 2013 katika bei.. (overcharge)

12. Tanesco na serikali hawakutoa ushirikiano ndani ya siku90 kutekeleza uamuzi huo ambao una faida kwa nchi kwasababu tayari tangu sept2013 pesa ya escrow imeshaliwa. Huu ndio uzalendo?

12. Kwanini serikali imekosea kufanya malipo haya kwa haraka?;

a. Kipindi malipo haya yanasukumwa kwa nguvu BOT itoe waziri wa fedha alikuwa anaumwa na wakati malipo yanafanyika nov2013 tayari waziri mgimwa alikuwa amekata kauli hospital afrika kusini

b. Kampuni ya singasinga ya PAP ilokomba fedha hiyo sio mmiliki halali wa IPTL ndio mana mpaka sasa hakutoa share certificate ya yeye kuuziwa 70% za Iptl ambazo ziko chini ya Mechmar. Kwann serikali imemuamini bila uthibitisho huo?

C.kama kweli alinunua asilimia 70 ya share za mechamar zilizo iptl angelipa capital gain tax lakn hakuna ushahidi huo kama alivo na ushahidi wa kununua hisa 30 za VIP

d.ushahidi mwingine ni kwamba wakati PAP inasema ilinunua IPTL tangu 2010 ukweli ni kwamba tangu 2008 mpaka 2013 IPTL ilikuwa under receivership chini ya RITA na hivyo isingewezekana kisheria share zake iuze

E. Ushahidi mwingine kampuni yenyewe ya mechmar imeandika barua gazeti la citizen na kwa wakili wake Tanzania asyla attorney kupinga kuwa haijauza hisa zake za IPTL kwakuwa ilikuwa under kiquidation na ikielekeza kuwa huyo PAP anaedai kuwa alinunua hisa hizo awaoneshe share certificate.

F. Hakuna ushahidi wa malipo ambayo PAP ameonesha alifanya kununua share za VIP kabla ya kupata pesa za escrow. .ndio mana mmiliki wa PAP aliandika barua BOT kulalamika kuwa kampuni ya PAP ni ya kitapeli isilipwe kwakua ilikuwa haijamlipa wakati huo ilikuwa novemba mwanzoni kabla pesa haijatoka escrow..hii maana yake PAP alilipa VIP bada ya kuchota pesa za escrow. Kwamba alinunua hisa bada ya kufaidi hisa. Hii haikubaliki kisheria

Kwa ujumla suala hili ni aibu nyingine kwa taifa ambalo Tanesco inadaiwa zaidi ya 400bn leo inatapanya 200bn kizembe namna hii. Lakn zaidi liquidator wa mechmar ataidai serikali na kulipwa...standard chartered ambae alikuwa anaidai serikali na kesi haijafika mwisho nae tutamlipa..huyu singasinga atabaki na mitambo ya iptl na ametudhulumu hizo 200bn za escrow pamoja na gharama ambazo iptl ilikuwa ina overcharge ambazo ilipaswa turejeshewe zaidi ya 150m dola za tangu 2002 mpaka 2013.

Ni aibu watu wanaosema ni wazalendo leo wanashabikia nchi kuporwa 200bn na singasinga mwenye rekodi mbaya. Ushahidi wote nitauweka wazi bungeni na nitahakikisha ninauweka wazi kwenye mitandao yote y kijamii ili kila mtanzania aelewe huu mzima wa IPTL ulioshindikana tangu awamu ya pili mpaka leo.

Na nitaandika kitabu kuhusu sakata hili ambalo kabla ya mwalimu Nyerere hajatuacha duniani alitaja kama mfano wa ufisadi mbaya africa.


(imetolewa na David Kafulila)
 
Suala hili lilishatolewa maelezo na Waziri Mkuu. Wewe kiherehere cha nini? Najua chama chako kimepewa fedha na Reginald Mengi lakini mbele ya Prof hamtaambulia kitu. Hoja zenuzote zina majibu
 
Hakuna wizara nisiyoipenda kama hii ya nishati na madini. Madini mengi Tanzania na nchi bado maskini, umeme wa mgawo kila mwaka aaahhh nisije tukana bure
 
Suala hili lilishatolewa maelezo na Waziri Mkuu. Wewe kiherehere cha nini? Najua chama chako kimepewa fedha na Reginald Mengi lakini mbele ya Prof hamtaambulia kitu. Hoja zenuzote zina majibu
Wewe ni Me au Ke? Nataka kukushauri kuhusu maradhi yako ...
 
Suala hili lilishatolewa maelezo na Waziri Mkuu. Wewe kiherehere cha nini? Najua chama chako kimepewa fedha na Reginald Mengi lakini mbele ya Prof hamtaambulia kitu. Hoja zenuzote zina majibu

Mbona unataka kuwatoa watu kwenye mjadala? Mengi anaingiaje hapa kwenye maswala nchi kama aya?? Nchi inaibiwa kijinga namna hii ila unaona ni sawa tu kutetea ukifikiri unaitetea ccm..Laana uwa zinapenya tu haijarishi unatumia fake id...
 
Kama hujaelewa maelezo haya ya Waziri Mkuu basi utakuwa na utindio wa Ubongo

KAULI YA SERIKALI KUHUSU FEDHA KATIKA AKAUNTI YA ESCROW KUHUSIANA NA MKATABA WA IPTL
HISTORIA YA MRADI WA IPTL


Mheshimiwa Spika, katika mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, baadhi ya Waheshimiwa wabunge wamehoji utoaji wa fedha kwenye Escrow Account baada ya Hukumu ya Mahakama Kuu ya Tanzania.


Mheshimiwa Spika, Makubaliano kati ya Serikali na Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kuanzisha mradi wa kufua umeme wenye uwezo wa kuzalisha MW 100, yalifikiwa ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa umeme katika miaka ya 90. Serikali ilialika sekta binafsi kuwekeza katika uzalishaji umeme kwa vile haikuwa na fedha za kugharimia miradi ya umeme. Kampuni ya VIP Engineering and Marketing Ltd ya Tanzania (VIP) iliweza kuishawishi Serikali kualika Kampuni ya Mechmar Corporation ya Malasyia (MECHMAR), na baada ya MECHMAR kuonyesha kuwa inaweza kuzalisha MW 100 katika mji wa Dar es Salaam ilisaini MoU na Serikali. Mwaka 1994 Kampuni ya MECHMAR na Kampuni ya VIP kwa pamoja zilianzisha Kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kama kampuni binafsi iliyokuwa inamilikiwa na MECHMAR kwa asilimia 70 na VIP kwa asilimia 30. Kampuni ya IPTL ilipewa leseni ya kujenga, kumiliki na kuendesha (Build-Own-Operate) mtambo wa kuzalisha MW 100 za umeme wa mafuta mazito katika eneo la Tegeta-Salasala.


Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Kununua Umeme kati ya TANESCO na IPTL, (Power Purchase Agreement-PPA) ulisainiwa tarehe 26 Mei, 1995 kwa kipindi cha miaka 20, ingawa utekelezaji wake ulianza 2002. Katika Mkataba wa PPA, TANESCO ndiye mnunuzi pekee wa umeme toka mtambo wa IPTL. Kulingana na IPTL inatakiwa kuiuzia TANESCO umeme usiopungua asilimia 85% ya umeme unaozalishwa kila siku. Pamoja na mkataba huo, Serikali ilisaini mikataba miwili ambayo ni Mkataba wa Utekelezaji (Implementation Agreement) na Mkataba wa Dhamana (Guarantee Agreement) ambapo ilikusudiwa kuwa, endapo TANESCO itashindwa kulipa gharama za kununua umeme, Serikali ichukue dhamana ya kulipa gharama hizo kwa niaba ya TANESCO.


Mheshimiwa Spika, Gharama za uwekezaji wa mradi huo zilikadiriwa kuwa Dola za Marekani milioni 150. IPTL walitakiwa kutoa asilimia 30 kama mtaji na asilimia 70 kama mkopo. Makubaliano kati ya wanahisa hao ni kwamba MECHMAR watoe fedha za mtaji na mchango wa VIP uwe huduma muhimu za kuwezesha kuanzishwa kwa IPTL na eneo la kiwanja kitakachojengwa mtambo wa kuzalisha umeme huko Tegeta Salasala. Kwa maelezo yote hayo, utaona kuwa Serikali na TANESCO siyo wabia bali wateja wa Kampuni ya IPTL. Hata hivyo, Wanahisa wa IPTL (MECHMAR na VIP) hawakutoa asilimia 30 ya mtaji kama walivyotakiwa ila waligeuza fedha za mkopo kuwa mtaji.Kwa lugha nyingine wanahisa hao walidanganyana wenyewe.


Mheshimiwa Spika, Baada ya mkataba huo kutiwa saini, tarehe 4 Februari, 1997 IPTL iliingia mkataba wa ujenzi (EPC Contract) na Kampuni ya Wartsila ya Uholanzi. Tarehe 28 Juni, 1997, IPTL iliingia mkataba wa mkopo (Syndication Loan Agreement) na umoja wa mabenki ya Malaysia kwa ajili ya mkopo wa Dola za Marekani milioni 105 ikiwa ni asilimia 70 ya mtaji wa IPTL.


Mheshimiwa Spika, Hata hivyo, IPTL walitakiwa kuchukua Dola za Marekani 85,862,022.08 kutoka Dola za Marekani milioni 105 zilizotolewa kama mkopo. Serikali wala TANESCO hawakuwa sehemu ya Mkataba huo. Mkopo huo ulitakiwa kurudishwa katika kipindi cha miaka nane (8) na riba ilikuwa asilimia 2.5 kwa mwaka. Grace period ya mkopo huo ilikuwa miezi 18. Dhamana ya mkopo huo ilikuwa kiwanja cha Tegeta ambapo mtambo wa kuzalisha umeme utawekwa pamoja na mtambo wa kuzalisha umeme. Mradi wa IPTL ulianza uzalishaji umeme mwezi Januari, 2002 na ndiyo utekelezaji wa mkataba ulpoanza.


Mheshimiwa Spika, Kulingana na PPA, malipo ya gharama za umeme ambazo TANESCO inatakiwa kulipa ni ya aina mbili energy na capacity charges. Capacity charge ni gharama za uendeshaji na matengenezo (O&M) pamoja na vilainishi, ambazo zinalipwa hata kama TANESCO haitumii umeme unaozalishwa na IPTL. Energy charges ni gharama za kuzalisha umeme ambazo TANESCO inalipa ikitumia umeme wa IPTL.


Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa mtambo ulianza mwaka 1997 na kukamilika mwaka1998, lakini uzalishaji ulianza tarehe 15 Februari, 2002 (Commercial Operational Date). Mtambo ulichelewa kuanza uzalishaji kutokana na mgogoro kati ya TANESCO na IPTL katika Mahakama ya Usuluhishi ya Kimataifa (ICSID).


AKAUNTI YA ESCROW


Mheshimiwa Spika, Akaunti ya Escrow ilifunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania baada ya Mkataba wa Escrow kusainiwa na Serikali (kwa niaba ya TANESCO), Independent Power Tanzania Limited (IPTL) na Benki Kuu ya Tanzania, tarehe 5 Julai, 2006. (Kiambatisho Na. 1)


Mheshimiwa Spika, Kufunguliwa kwa akaunti ya Escrow kulitokana na ushauri wa Mkono and & Co. Advocates in association with Denton Wilde Sapte wa tarehe 30 Juni, 2004. Ushauri huo upo kwenye kifungu cha 10.1 na 10.2. (Kiambatisho Na. 2)


Mheshimiwa Spika, Mkataba wa Escrow ulitokana na Mkataba wa Ununuzi wa Umeme kati ya TANESCO na IPTL uliosainiwa tarehe 26 Mei, 1995. Kulingana na kifungu Na. 6.8 cha PPA, kinachoeleza kuwa, iwapo pande mbili za mkataba hazikubaliani na gharama za umeme, fedha za gharama za umeme zilipwe kwenye akaunti ya Escrow hadi hapo mgogoro wa malipo utakapotatuliwa. (Kiambatisho Na. 3)


Mheshimiwa Spika, Fedha zilizokuwa kwenye akaunti ya Escrow zilikuwa zinalipwa na TANESCO kutokana na mgogoro wa gharama za malipo kati ya TANESCO na IPTL. TANESCO ilidai kuwa inalipa gharama za juu kutokana na IPTL kutumia fedha za mkopo kama mtaji, kukokotoa gharama za umeme wakati fedha halisi za mtaji wa IPTL si zaidi ya Dola za Marekani 1,000. IPTL walikuwa wakidai kuwa fedha za mkopo zihesabiwe kama mtaji kukokotoa gharama za umeme. Aidha, TANESCO walikuwa wakilipa fedha kwenye akaunti ya Escrow kuanzia tarehe 22 Septemba, 2006 hadi Agosti 2009 walipoacha kuweka fedha kwenye akaunti hiyo. (Kiambatisho Na. 4) kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo IPTL kuwa kwenye ufilisi na kuendelea kutoa dispute notice kwa ushauri wa Wakili wao.


Mheshimiwa Spika, kulingana na kifungu cha XXII cha "Implementation Agreement" ya tarehe 8 Julai, 1995 kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na IPTL, Serikali ilitoa dhamana (Guarantee) kulipa fedha yoyote ambayo TANESCO itashindwa kulipa kama itatokea hivyo na siyo kama IPTL itakopa au mtu yeyote atakopa kwa niaba ya IPTL. Dhamana ya Serikali ilihusu "Capacity Charge" na si vinginevyo. Mkopeshaji yeyote ambaye siyo sehemu ya PPA hawezi kujigeuza na kudai ni sehemu ya mkataba huu. Mawakili (Mkono & Company Advocates) wetu wanaelewa hivyo lakini hawataki kusema kwa kuwa watapoteza au kuacha kulipwa na Serikali pamoja na TANESCO.


Mheshimiwa Spika, Kwa maelezo hayo, na kwa mtazamo wangu, kampuni pekee inayonufaika na dhamana ya Serikali ni IPTL au yeyote atakayekuwa anamiliki IPTL na Serikali pia ilikubali kulingana na sheria za nchi.


Mheshimiwa Spika, Ni vizuri ikaeleweka kuwa, akaunti ya Escrow ilifunguliwa kutokana na "Dispute" iliyotolewa na TANESCO na sasa, "Dispute" haipo, na hivyo Serikali yeyote makini haina sababu ya kuzuia fedha ambazo zipo kwenye akaunti ya Escrow kwa sababu yoyote ile.


Mheshimiwa Spika, IPTL ni Kampuni binafsi na siyo kampuni ya Serikali, na TANESCO kama Mnunuzi wa umeme, wajibu wake ni kununua umeme na siyo kuingilia masuala ya ndani ya Kampuni. Kama "dispute" imeisha sasa fedha hizo zinazuiwa ili ziende wapi na zifanye nini?


Mheshimiwa Spika, Katika hukumu yake, ya tarehe 5 Septemba, 2013 na pia "consent order" iliyotolewa na Judge Utamwa J, tarehe 17 Januari, 2014, katika kesi yake Misc. Civil Case No.49/2002 and Misc. Civil Case No.254/2003 states "among other prayers that, by this settlement order, parties have discharged all of their respective outstanding performance obligations required in completion of execution of the contract". (Kiambatisho Na. 5 )


Mheshimiwa Spika, Siamini kama Bunge letu tukufu lingependa kuhoji maamuzi ya Mahakama. Ninaamini Mahakama zetu zina-uhuru wa kutoa uamuzi wowote na kulinda haki za Wananchi. Vyama vya upinzani wakifukuzana kwenye Ubunge (kama ilivyo kwa Mhe. Zitto Kabwe na Mhe. David Kafulila) hukimbilia mahakamani na wanapopewa haki hawalalamiki na huona ni sawa, lakini katika kesi hii kati ya VIP na IPTL imeisha na mahakama imeamua hatutaki kukubali. Tumefikia mahali hatuiamini Mahakama kama chombo cha kutoa haki? Kwa nini hakuna aliyekata rufaa kupinga maamzi ya Mahakama?


Mheshimiwa Spika, Kwa mujibu wa Hati ya Makabidhiano (Handing Over Note) ya tarehe 5 Septemba, 2013 (Kiambatisho Na. 6), IPTL inaonyesha inaidai TANESCO jumla ya Tshs.370,738,773,651.09 sawa na Dola za Marekani milioni 227.45 kufikia tarehe 5 Septemba, 2013.


Mheshimiwa Spika, Kutokana na hukumu ya Mhe. Jaji Utamwa ya tarehe 05 Septemba, 2013 kuondoa IPTL kwenye ufilisi na kutambua PAP kama mmiliki kwa asilimia 100 wa IPTL, TANESCO ilifanya mazungumzo na IPTL kwa ajili usuluhisho wa hesabu ya fedha ambazo TANESCO ilikuwa haijaweka kwenye Akaunti ya Escrow na kukubaliana jinsi ya kulipa fedha hizo.


Mheshimiwa Spika, Aidha, kwa mujibu wa barua ya IPTL ya tarehe 20 Septemba 2013, IPTL wanadai TANESCO jumla ya Dola za Marekani milioni 239.6 na Tshs. 33,370,147,675.88/- kama Capacity Charges. Hata hivyo, baada ya TANESCO kukaa na kufanya hesabu upya na IPTL; walikubaliana kuwa madai halali ya IPTL ni Dola za Kimarekani 79.05 milioni. (Kiambatisho Na. 7)


Mheshimiwa Spika, Wakati wa kufunga akaunti ya Escrow Desemba, 2013 kulikuwa na jumla ya Dola za Marekani 22,198,544.60 na Shilingi za Tanzania 161,359,686,585.34 (sawa na Dola za Marekani milioni 122). Baada ya makubaliano kati ya TANESCO na IPTL, Serikali ilisaini makubaliano na IPTL ya kuruhusu fedha za Escrow zilipwe kwa IPTL na kuagiza Benki Kuu ya Tanzania kulipa fedha hizo kwa IPTL na kufunga akaunti hiyo. (Kiambatisho Na. 8).


Mheshimiwa Spika, Pamoja na maelezo ya hapo juu, napenda kusistiza kuwa IPTL ni Kampuni binafsi ya kuzalisha umeme kama ilivyo Kampuni ya Symbion na Songas, Serikali haijihusihi na masuala binafsi ya Makampuni hayo. Mgogoro iliyopo ni kati ya Benki ya Standard Charterd Hong Kong na IPTL, Serikali si sehemu ya mgogoro huo.


Mheshimiwa Spika, ni vizuri sisi kama viongozi wa wananchi tukaheshimu Mahakama zetu na tusipende kuwa wasemaji tu bila uhakika baada ya kupata habari za mitaani.


Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja
 
Suala hili lilishatolewa maelezo na Waziri Mkuu. Wewe kiherehere cha nini? Najua chama chako kimepewa fedha na Reginald Mengi lakini mbele ya Prof hamtaambulia kitu. Hoja zenuzote zina majibu

Hivi Pinda anaweza kufafanua nini katika hili la IPTL?
 
Kwanini hawaruhusu kampuni binafsi kuzarisha umeme?
Kampuni zinaruhusiwa kuzalisha umeme na kuiuzia TANESCO. hata hiyo IPTL ni kampuni binafsi na si ya TANESCO. Mwambie tu Mengi azalishe umeme na kuusambaza badala ya kulialia kwa Prof
 
Mbona unataka kuwatoa watu kwenye mjadala? Mengi anaingiaje hapa kwenye maswala nchi kama aya?? Nchi inaibiwa kijinga namna hii ila unaona ni sawa tu kutetea ukifikiri unaitetea ccm..Laana uwa zinapenya tu haijarishi unatumia fake id...
Mengi ndiye anayefadhili kundi la wapinga maendeleo
 
Wamechota hela kwa kuwa awamu yao inaisha ili pia waweze kufadhili Wabunge vibaraka watakaokuja kuwa mawaziri wao wa kuwaibia na pia kuweka mgombea wao!!!
 
Hakuna wizara nisiyoipenda kama hii ya nishati na madini. Madini mengi Tanzania na nchi bado maskini, umeme wa mgawo kila mwaka aaahhh nisije tukana bure
Mie nilijua kuwa utaipenda kwa vile boss wako Mengi anamiliki vitalu kadhaa vyenye ukubwa sawa na Jiji la Dar es Salaam!
 
Wamechota hela kwa kuwa awamu yao inaisha ili pia waweze kufadhili Wabunge vibaraka watakaokuja kuwa mawaziri wao wa kuwaibia na pia kuweka mgombea wao!!!
Kakudanganya nani kama awamu ya CCM inaishia?
 
Back
Top Bottom