Ifahamu nguvu ya kisayansi 'inayoikinga' Pwani ya Afrika Mashariki na vimbunga

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Kwanini ni nadra vimbunga kutokea Afrika Mashariki?

Mwishoni mwa wiki kulikuwa na tahadhari kubwa nchini Tanzania kutokana na uwezekano wa kupigwa na kimbunga Jobo. Hata hivyo, kimbunga hicho kilipungua nguvu na kutokuwa na athari kabisa nchini humo.

Hiki kilikuwa ni kimbunga cha pili kwa miaka ya hivi karibuni kutishia kupiga Tanzania, mwaka 2019 Kimbunga Kenneth kilichokuwa kinatazamiwa kupiga Tanzania na Msumbiji kikitokea baharini, lakini mwishowe kikatua Msumbiji karibu na mpaka wa Tanzania.

Jumla ya watu 52 walipoteza maisha, saba katika visiwa vya Comoro na 45 nchini Msumbiji.

Wakati sehemu mbalimbali duniani ambazo zipo katika upwa ama karibu na bahari kubwa huathirika na misimu ya vimbunga, baadhi ya watu wanaweza kujiuliza kwa nini Tanzania na upwa wa Afrika Mashariki (Kenya na Somalia) haziathiriwi na vimbunga.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya masuala ya hali ya hewa, kimbunga cha mwisho kuipiga Tanzania ilikuwa Aprili 14 mwaka 1952 mkoani Lindi, kipindi hicho bado ikiwa ni koloni la Tanganyika chini ya utawala wa Mwingereza.

Miaka 80 nyuma, yaani Aprili 15, 1872 kimbunga cha mwisho kiliipiga Zanzibar, na kwa mujibu wa maelezo yaliyorekodiwa ya Balozi wa Uingereza visiwani Zanzibar wa miaka hiyo Bw. John Kirk theluthi mbili ya mashamba ya minazi na karafuu visiwani humo yaliharibiwa vibaya.

Hivyo, laiti Jobo kingetua na nguvu, basi kingekuwa kimbunga cha kwanza kurekodiwa kupiga jiji la Dar es Salaam na cha pili kuipiga Zanzibar baada ya takriban miaka 149.

Msimu wa vimbunga
Eneo la Bahari ya Hindi, kuanzia kusini magharibi ya India mpaka upwa wa mashariki na kusini ya Afrika una msimu wake wa vimbunga ambao huanza mwezi wa Novemba na kuishia mwezi wa Aprili.

Vimbunga vya Zanzibar na Lindi vyote vilitokea mwezi wa nne, hata kwa upande wa Jobo pia huu ni mwezi wa Aprili.

Kimbunga Kenneth kilipiga mwezi wa Aprili 2019 na mwezi mmoja nyuma yake kimbunga kibaya zaidi cha Idai kiliipiga Msumbiji na athari zake kufika mpaka nchi jirani za Malawi na Zimbabwe. Zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha katika kipindi hicho.

Kwa msimu wa mwaka huu (2020/21) ambao unaelekea mwisho zaidi ya vimbunga vikubwa na hafifu 16 vimejitengeneza na kuathiri baadhi ya nchi katika ukanda huo, Jobo ikiwa ni kimoja wapo.

Katikati ya dunia
Suali linalosalia ni kwa nini vimbunga hivyo havianzii ama kuathiri pwani ya Afrika Mashariki? Jibu ni kuwa eneo hilo lipo 'kati kati ya dunia'.

Kimbunga Jobo kilipokuwa kikikaribia pwani ya Afrika Mashariki wikendi iliopita

Dunia imegawanyika katika mihimili miwili, mhimili wa kusini na mhimili wa kaskazini. Kilichogawanyisha dunia katika mihimili hiyo ni mstari dhahania wa Ikweta. Mstari huo unapita kwenye nchi 13 duniani zikiwemo Somalia, Kenya na Uganda.

"Vimbunga husukumwa na nguvu iitwayo Kani ya Coriolis. Kani hiyo haina nguvu kabisa katika eneo la Ikweta kwa kuwa ndipo mhimili wa Kaskazini na Kusini huapaka, na upepo katika mihimili hiyo huenda katika njia tofauti upande mmoja kushoto upande mwengine kulia," anaeleza Profesa Marshall Shepherd, rais wa zamani wa Jumuiya ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Marekani.

Mtaalamu huyo anaeleza katika makala ya mwaka 2018 iliyochapishwa na jarida la Forbes kuwa nguvu hiyo kinzani ndio huua nguvu ya vimbunga katika eneo hilo.

Japo Tanzania haijapitiwa na mstari wa Ikweta lakini ipo katika ukanda wa Ikweta, masafa machache kusini mwa mstari huo uliopita katika nchi jirani za Kenya, Uganda na hata DR Congo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Prof Shepherd endapo kimbunga kikali kitajitengeneza mbali na eneo hilo kinaweza kuathiri moja kwa moja eneo hilo, "japo kutokea kwa hali hiyo ingali bado ni jambo la nadra."

Hata hivyo, hali ya mvua kubwa na mafuriko huukumba ukanda wa Ikweta kutokana na athari ya vimbunga vinavyopiga maeneo ya karibu katika msimu wake.
___________________________
Rejea hapa
 
tanzania kama tungekuwa na uongozi ulio mzuri ni taifa ambalo lingekuwa moja ya maifa super, lakini bahati mbaya ndio hivyo tena
tanzania kama tungekuwa na uongozi ulio mzuri ni taifa ambalo lingekuwa moja ya maifa super, lakini bahati mbaya ndio hivyo tena!

Lakini uongozi mzuri si kwamba ndo tutakuwa super power
 
"Miaka 80 nyuma, yaani Aprili 15, 1872 kimbunga cha mwisho kiliipiga Zanzibar, na kwa mujibu wa maelezo yaliyorekodiwa ya Balozi wa Uingereza visiwani Zanzibar wa miaka hiyo Bw. John Kirk theluthi mbili ya mashamba ya minazi na karafuu visiwani humo yaliharibiwa vibaya."

Naam!!!!!!!!!🤔🤔🤔🤔🤔
 
Lakini kwa sasa Tanzania ni kama tunabahati hivi
 
Tz kama tunalindwa hivi
... sio Tanzania tu wala tusijisifie kwamba tunamjua sana Mungu au kwamba tunajua kuomba sana kuliko wengine; la hasha! Ni nguvu za asili zinafanya kazi yake; kama Brazil ambayo nayo iko ukanda wa Ikweta iko exempted kwenye vimbunga kutokana na nguvu hizo za asili.
 
🙏🙏🙏
 
Kwanini ni nadra vimbunga kutokea Afrika Mashariki?

Mwishoni mwa wiki kulikuwa na tahadhari kubwa nchini Tanzania kutokana na uwezekano wa kupigwa na kimbunga Jobo. Hata hivyo, kimbunga hicho kilipungua nguvu na kutokuwa na athari kabisa nchini humo.

Hiki kilikuwa ni kimbunga cha pili kwa miaka ya hivi karibuni kutishia kupiga Tanzania, mwaka 2019 Kimbunga Kenneth kilichokuwa kinatazamiwa kupiga Tanzania na Msumbiji kikitokea baharini, lakini mwishowe kikatua Msumbiji karibu na mpaka wa Tanzania.

Jumla ya watu 52 walipoteza maisha, saba katika visiwa vya Comoro na 45 nchini Msumbiji.

Wakati sehemu mbalimbali duniani ambazo zipo katika upwa ama karibu na bahari kubwa huathirika na misimu ya vimbunga, baadhi ya watu wanaweza kujiuliza kwa nini Tanzania na upwa wa Afrika Mashariki (Kenya na Somalia) haziathiriwi na vimbunga.

Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vya masuala ya hali ya hewa, kimbunga cha mwisho kuipiga Tanzania ilikuwa Aprili 14 mwaka 1952 mkoani Lindi, kipindi hicho bado ikiwa ni koloni la Tanganyika chini ya utawala wa Mwingereza.

Miaka 80 nyuma, yaani Aprili 15, 1872 kimbunga cha mwisho kiliipiga Zanzibar, na kwa mujibu wa maelezo yaliyorekodiwa ya Balozi wa Uingereza visiwani Zanzibar wa miaka hiyo Bw. John Kirk theluthi mbili ya mashamba ya minazi na karafuu visiwani humo yaliharibiwa vibaya.

Hivyo, laiti Jobo kingetua na nguvu, basi kingekuwa kimbunga cha kwanza kurekodiwa kupiga jiji la Dar es Salaam na cha pili kuipiga Zanzibar baada ya takriban miaka 149.

Msimu wa vimbunga
Eneo la Bahari ya Hindi, kuanzia kusini magharibi ya India mpaka upwa wa mashariki na kusini ya Afrika una msimu wake wa vimbunga ambao huanza mwezi wa Novemba na kuishia mwezi wa Aprili.

Vimbunga vya Zanzibar na Lindi vyote vilitokea mwezi wa nne, hata kwa upande wa Jobo pia huu ni mwezi wa Aprili.

Kimbunga Kenneth kilipiga mwezi wa Aprili 2019 na mwezi mmoja nyuma yake kimbunga kibaya zaidi cha Idai kiliipiga Msumbiji na athari zake kufika mpaka nchi jirani za Malawi na Zimbabwe. Zaidi ya watu 1,000 walipoteza maisha katika kipindi hicho.

Kwa msimu wa mwaka huu (2020/21) ambao unaelekea mwisho zaidi ya vimbunga vikubwa na hafifu 16 vimejitengeneza na kuathiri baadhi ya nchi katika ukanda huo, Jobo ikiwa ni kimoja wapo.

Katikati ya dunia
Suali linalosalia ni kwa nini vimbunga hivyo havianzii ama kuathiri pwani ya Afrika Mashariki? Jibu ni kuwa eneo hilo lipo 'kati kati ya dunia'.

Kimbunga Jobo kilipokuwa kikikaribia pwani ya Afrika Mashariki wikendi iliopita
Kimbunga Jobo kilipokuwa kikikaribia pwani ya Afrika Mashariki wikendi iliopita

Dunia imegawanyika katika mihimili miwili, mhimili wa kusini na mhimili wa kaskazini. Kilichogawanyisha dunia katika mihimili hiyo ni mstari dhahania wa Ikweta. Mstari huo unapita kwenye nchi 13 duniani zikiwemo Somalia, Kenya na Uganda.

"Vimbunga husukumwa na nguvu iitwayo Kani ya Coriolis. Kani hiyo haina nguvu kabisa katika eneo la Ikweta kwa kuwa ndipo mhimili wa Kaskazini na Kusini huapaka, na upepo katika mihimili hiyo huenda katika njia tofauti upande mmoja kushoto upande mwengine kulia," anaeleza Profesa Marshall Shepherd, rais wa zamani wa Jumuiya ya Utabiri wa Hali ya Hewa ya Marekani.

Mtaalamu huyo anaeleza katika makala ya mwaka 2018 iliyochapishwa na jarida la Forbes kuwa nguvu hiyo kinzani ndio huua nguvu ya vimbunga katika eneo hilo.

Japo Tanzania haijapitiwa na mstari wa Ikweta lakini ipo katika ukanda wa Ikweta, masafa machache kusini mwa mstari huo uliopita katika nchi jirani za Kenya, Uganda na hata DR Congo.

Hata hivyo, kwa mujibu wa Prof Shepherd endapo kimbunga kikali kitajitengeneza mbali na eneo hilo kinaweza kuathiri moja kwa moja eneo hilo, "japo kutokea kwa hali hiyo ingali bado ni jambo la nadra."

Hata hivyo, hali ya mvua kubwa na mafuriko huukumba ukanda wa Ikweta kutokana na athari ya vimbunga vinavyopiga maeneo ya karibu katika msimu wake.
___________________________
Rejea hapa

Umenikumbusha Coriolis force au Fictitious force ndio kwenye Geograph ikaja Ferrel's lawa.Nimemkumbuka lecture wangu wa Physics Dr S P Kashinje baada ya kuitaja Coriolis force
 
Wabongo bana!! kwanza mjue tuna bahati mbaya kutopitiwa na hiki kimbunga kwa sababu hiki kimbunga kimoja kikipita kwa nguvu ile ile inaweza zalisha umeme wenye Mega watts nyingi mno! na

ukasambazwa kwa nchi zote za kusini mwa Africa, ukatusadia Viwandani na shughuli za kilimo! na yale maji yanayotokana na kimbunga bado yakahifadhiwa vizuri tu! ajili ya matumizi mbalimbali km ya umwagiliaji kipindi cha baadaye sana! yale maji yana beba rutuba sana si kitoto, tukiya hifadhi tunatunza rutuba!

KIla kitu kinacho ambatana na kimbunga ni faida kubwa mno! ajabu waafrica tunaona ni karma! wapo waafrica wana jua kujenga nyumba zenye uwezo wa kukabiliana na dhoruba ya kimbunga kabisa!! kule Msumbiji lkn sasa wali/wanahujumiwa! Maksudi kwa sababu mbalimbali.

wana uwezo wa kuzuia yale maji yasipotelee baharini! ghafla hivi kwa kutumia njia za wenyeji tangu mababu badala yake yataenda kidogo kidogo, baada ya kuwa yametumika miaka kadhaa kulingana na ukubwa wa dhoruba ya wkt husika!

Kitendo cha kuiweka Msumbiji kwenye Vita ya wenyewe kwa wenyewe kwa mda mrefu! imechangia pa kubwa kudhoofisha tech. hii ya kale na wakoloni walijua hasa!! hasara wanayo ifanya! lkn haikupotea jumla!
 
Faida ya kimbuka kwa Bongo ni ndogo sana ukilinganisha na Athari ambazo tungepata.
Hivyo bora tukose hizo watts
 
Back
Top Bottom