Ifahamu kondomu

Frumence M Kyauke

JF-Expert Member
Aug 30, 2021
630
1,245
Kondomu ni kifaa/ zana iliyotengenezwa mahususi kuvalisha uume au kuwekwa ukeni wakati wa kujamiiana.Nazo hubana kutokana na umbile la uume au uke.

Kondomu hizi zipo za aina tofauti kutokana na muda na vipindi zilipotengenezwa, nazo ni kama ifuatavyo:-

Awamu ya I – zilizotengenezwa kwa mimea.

Hizi zilitengenezwa mahususi kama kinga dhidi ya maambukizo ya vimelea vya ugonjwa wa kaswende [ugonjwa wa kifaransa]

Awamu ya II – kutokana na utumbo wa kondoo.

Dr. Condom alifahamika kama mgunduzi wa kondomu hizi, naye alikuwa ni dakatari wa Mfalme Charles II.

Alimshauri Mfalme kutumia kama kinga kutokana na magonjwa ya zinaa kutokana na tabia yake ya kuwa na wanawake wengi nje ya ndoa yake.

Awamu ya III – kutokana na mpira

Hizi zilitengenezwa kwa urahisi na kwa wingi na zikawa ndizo pekee zenye uwezo wa kudhibiti mimba hadi miaka ya 1960 vilipogunduliwa na vidonge vya majira.

Je Kondomu ni salama?

Tunaelezwa kuwa kondomu hutengenezwa kwa ustadi mkubwa kiasi kwamba haziwezi kuruhusu kitu chochote kupita.

Wengine wanadai kuwa ili kuzifanya imara, kondomu zimetengenezwa kwa kupishanisha pande mbili ili kuziba udhaifu wa kila upande.

Wasambazaji wanatueleza kuwa kondomu zilizotoka kiwandani zikiwa na ubora unaotakiwa zikitumika wakati wote na kwa usahihi zina uwezo wa kukinga kwa kiwango hadi cha asilimia 97.

Kondomu zaweza kuzuia kwa kiwango kikubwa maambukizo ya magonjwa ya zinaa yanayosafiri kwa njia ya ute, .

images - 2021-11-07T101936.607.jpeg
 
Back
Top Bottom