uttoh2002
JF-Expert Member
- Feb 3, 2012
- 14,758
- 26,669
Rais wa jamhuri ya Muungano mama Samia, alitengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi wa TTCL Maharage Chande ,muda mfupi tu baada ya kuteuliwa .
Pamoja na Track Record safi , uzalendo na uchapakazi mzuri wa Peter Ulanga Rais aliamua kumrudisha madarakani Mkurugenzi Ulanga si tu kwa weledi wake kazini na uongozi bora kabisa ,ambao umeanza kuirudisha TTCL kwenye ramani.
Jambo la pili ni umiliki wa hisa nyingi (majority share) wa bwana Maharage Chande kwenye kampuni ya softNet.
Kampuni hii ina kandarasi ya kutoa huduma kwenye mkongo wa taifa, wakishirikiana na kampuni ya Huawei tokea China.
Kuteuliwa kwa Maharage Chande si tu kungeleta mgongano wa masilahi, lakini pia TTCL ingezikwa rasmi.
Peter Ulanga ni moja ya Wakurugenzi bora kabisa kwenye mashirika ya Umma kwa sasa nchini, just to mention few , Kamishina wa TRA ni kiongozi bora kabisa, Gavana wa BOT Tutuba ni bora kabisa.
Chini ya Nape kuna Peter Ulanga wa TTCL na Bakari yupo TCRA , hawa na visionary leader, TASAC kuna Mkurugenzi kijana anapiga kazi bora sana na wakurugenzi wengine kadhaa wanaing'arisha serikali.
Nini kilitokea mpaka Ulanga akataka kuondolewa.
Kuna Watu wasiomtakia mema Ulanga wapo wizara ya TEHAMA, hawa hata Nape hawajui vyema, kwenye hili Nape amekua upande wa Ulanga, watu hawa wanataka kwa hali na mali Ulanga andoke TTCL ili mkongo wa Taifa urudi wizarani ,utoke TTCL ,kuna watu wizara ya TEHAMA wala rushwa wakubwa sana ,ndio maana walitaka kum double cross Ulanga.
Rais amekua very smart kuwa ng'amua mapema kabla hawajatimiza adhima yao.
Mkongo wa Taifa una tija gani? Nimeomba connection mwaka umeisha, umebaki kusifia tu watu pasipo sababu, badiki kichwa cha habari kiwe ccm Oyee!
Rubbish.