Ifahamu biashara ya spea za pikipiki na bajaji (Sehemu ya pili)

Jvei

Member
Joined
Jul 13, 2025
Posts
42
Reaction score
64
Sehemu Iliyopita tuliishia kwenye mjadala wa mtaji, Inaendelea...

MTAJI WA SPEA ZA PIKIPIKI NA BAJAJI KWA WAUZAJI WA REJAREJA:
Makala hii ya Pili Itaangazia zaidi bishara hii kwa wale wanaopenda kufanya rejareja.
Hakuna mtaji kamili/sahihi wakuanza nao. Mtaji hutegemea zaidi hali ya kiuchumi ya mfanya biashara mwenyewe, pamoja na malengo yake ya kibiashara.
✅Viwango mbali mbali vya mtaji.
⚙Kiwango cha milioni 3 au 4. Mtaji huu unafaa kuanzia biashara hii ya spea za pikipiki, japokuwa ni mdogo sana kwenye ushindani na soko la biashara ya spea za pikipiki na bajaji. Mtaji huu utakuwezesha kupata vitu vichache tu vya kuanza navyo, ambavyo ni muhimu sana mhusika ajikite kwenye kununua vile vitu vya msingi zaidi (sehemu ya nne tutaenleza vitu hivyo)

⁉️Je, kwanini mtaji wa milioni 3/4 hadi 6 ni mdogo?
Kwauzoefu wa Dsm, Kuna pikipiki zaidi ya aina 8, japo nyingi zaidi ni: boxer, Tvs, Hero,Yamaha, GN, CG, Houjue n.k
Kila pikipiki moja inahitaji walau spea 350 ( hizi sio zote, ni baadhi tu).
Spea hizi zipo za aina 2 yaani Original na zakawaida (copy).
👉 Spare Original huzalishwa na kampuni iliyotengeneza pikipiki/bajaji husika na huwa na Alamance zake za utambuzi, mfano spare za Boxer Original huzalishwa na Bajajibajaji.
👉Spare za kawaida (copy) wengi hupenda kuziita za kichina, spea hizi huzalishwa na kampuni mbali mbali, zipo kampuni zaidi ya 15(ninazojua).
Utofauti kati ya Original na za kawaida, ni quality na bei. Original huwa na quality kubwa na bei kubwa pia, huku copy zikiwa za bei ya chini(wateja wengi hupendelea copy, maana ni wanazimudu garama zake)
Hoja kuu ya kuelezea spea hizi ni kutaka kujenga picha ya namna ambavyo mtaji mdogo unaweza kutumika, na kutambua mahitaji yalivyo makubwa. Hivyo kwenye manunuzi utanunua kwa kuchanganya bidhaa, Original kiasi, na copy nyingj kwakua Zina wateja wengi.

⚙Mtaji wa kati chini, kundi hili huanzia mtaji wa milioni 6 hadi 10/15. Ni kundi lenye ukubwa wa fedha, kiwango hicho kitakusaidia kununua vitu vingi zaidi vya pikipiki nyingi zaidi.
Nimuhimu kuelewa kuwa kuwa na bidhaa nyingi za aina mbalimbali, kutakusaidia kujenga jina na uaminifu wa haraka. Kwani wateja wengi watapata mahitaji yao. Hii ndio faida kubwa ya mtaji mkubwa kiasi.

⚙Mtaji wa kati Juu milioni 15 had 25.
Kundi hili la mtaji limeitwa mtaji wa kati Juu, kwakua lenyewe litakuengezea nguvu ya manunuzi. Utapata bidhaa nyingi zaidi aina mbalimbali pamoja na makampuni mbalimbali (wateja baadhi wanamakampuni yao wanayoyapenda, akija anaulizia spea ya kampuni hiyo, anakutajia jina).
Hivyo basi mtaji huu utakuwezesha kuwa na duka lililosheheni, faida ya kujaza duka ni pamoja na kupata uaminifu zaidi kwa wateja, pamoja na kupunguza msuguano wa bei. Kwani mteja akikuta duka halina vitu anaona kama unamdalalia.
Faida nyingine kubwa, mtaji huu utakupunguzia safari za kila mara kwenda kutafuta bidhaa, kwani stock yako itakuwa kubwa. Hivyo garama za nauli zinapungua na usumbufu. Pia Kuna punguzo kwa watu wanaonunua bidhaa nyingi kwenye maduka ya jumla, hii pia itakusaidia sana.

⚙Mtaji wa Juu milioni 25 hadi 50 na kuendelea,
Mtaji huu ni uwekezaji mzuri zaidi na mkubwa, una faida nyingi sana na utakufanya kutanuka kibiashara kwa haraka. Huku mjini wanasema (weka pesa upate pesa).

KIVIPI YANI?
Watu wengi tunaotaka kuanza bishara tunafurahia tukiambiwa mitaji midogo, hii huchangiwa sana na hali zetu za maisha.
Hata hivyo mitaji mikubwa itakupa fursa nyingi, na muhimu. Nakukufikisha sehemu amabayo mwenye mtaji mdogo angetumia miaka kadhaa kufika.
Ipo hivi, ukiwa na mtaji mkubwa unapata nguvu kubwa ya manunuzi. Badala ya kununua kwenye Maduka ya jumla, unapata fursa ya kwenda kununua huko Maduka ya jumla nawao wanakonunulia yaani kwa Supplier wa kampuni (hii wanaita kununua jumla kwa jumla).
Suppliers wengi wana idadi/idadi ya bidhaa ambazo ni minimum. Kama huwezi kununua watakuambia uende kwa wasambazaji waliopo chini yao.
Yes, huku vitu vingi hununuliwa kwa katoni, na bei yake huwa ndogo sana. Utofauti huu humidity pale ambapo utazidisha idadi ya katoni bei nayo hushuka zaidi. Hapa ndio pale wenye mitaji mikubwa hutupiga bao.
Manunuzi haya yatakufanya uwe nanguvu ya kuuza jumla na rejareja tena kwa bei ya chini. Yaani mtu akinunua katoni moja ya bidhaa kutoka kwa agent/Supplier ana uwezo wa kuwauzia wengine jumla wakauze rejareja. Je, aliamua kuuza rejareja nayeye atapata faida kiasi gani, au ushindani wa bei utakuwaje.
Je, Kunahaja ya kwenda China ukiwa na mtaji huu? Hapana.
Kuna watu wana mtaji hadi milioni 200 wala hawajawahi kufikiri kwenda China, japo kwenda si jambo baya (faida na hasara zake tutajadili wakati mwingine).
Jambo muhimu ni kudeal na suppliers kwani mtaji wako unavyokua mkubwa, unapata nguvu yakununua zaidi na bei wanayokuuzia inashuka zaidi. Na itafika mahali watakuwa wanakuuzia bei ya kiwandani.
Je, tukiwa na mtaji mdogo tusifanye biashara hii?
Hapana. Biashara ni jambo zuri, uchumi wetu si mkubwa sana, si kila mmoja anaweza kuwa na uwezo wa kundi la pili juu, au kundi la Tatu.
Nikutie moyo Anza na ulichonacho. Kuazia ulipo si sawa na kubakia ulipo.
 
Attachments

  • IMG-20250811-WA0014.jpg
    IMG-20250811-WA0014.jpg
    690.4 KB · Views: 36

⚙JINSI YA KUFANYA BISHARA YA SPEA ZA PIKIPIKI NA BAJAJI REJAREJA, (Itaendelea Sehemu ya Tatu....)
Screenshot_20241015-085038_Instagram.jpg
Safi sana Mkuu!
 
Noma 🔥 sadly enough nyuzi kama hizi hazipati wachangiaji wa kutosha ili waweze kupata Madini

Mkuu naomba uwe unanitag ktk muendelezo
 
Milion 20 inaweza kufunga mzigo wa maana China Kwa pikipiki?
 
Shukrani sana ,ukiondoa mtaji vitu gani hasa vinahitajika ili mfanyabiashara aweze kufanikiwa katika biashara hii.
 
Kufanya biashara ya spare za pikipiki kwa rejareja ni lazima uwe na fundi mahiri wa kutengeneza pikipiki. Mengine ya mitaji ni factor ya pili.
 
Back
Top Bottom