Kaptula la Marx
JF-Expert Member
- May 10, 2015
- 981
- 449
Ndugu wanajamvi kuanzia sasa tutaanza kukichambua chama cha ACT-TANZANIA/WAZALENDO kwa kujadili mambo kadhaa yanayohusiana na chama hicho. Katika mfululizo wa mabandiko yetu pamoja na mambo mengine, duru ya siasa hapa jamvini itaangazia mambo yafuatayo:-
a) Nini maana ya ACT-TANZANIA/WAZALENDO? Jina lake, maana yake, nembo zake; kutoka ACT-TANZANIA hadi ACT-WAZALENDO, kunani? ACT TANZANIA vs ACT WAZALENDO nini tofauti? Ushahidi kutoka jikoni
b) Chimbuko la ACT-TANZANIA/WAZALENDO mfano, chanzo chake, waasisi/waanzishi wake, lini chama kilianza; ACT-TANZANIA / WAZALENDO na dhana ya usaliti kwa upinzani nchini Tanzania; Ujio wa ACT-TANZANIA / WAZALENDO unafuu kwa CCM au upinzani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu? Ushahidi wa nyaraka na mawasiliano kutoka jikoni.
c) Misingi, Itikadi na Falsafa ya chama cha ACT-TANZANIA/ WAZALENDO; Misingi hiyo ni ipi? Itikadi ya ujamaa wa kidemokrasia ikoje; itikadi au falsafa? Uhalisia au njozi?
d) Mfumo na muundo wa uongozi ndani ya ACT-TANZANIA/ WAZALENDO; dhana ya Kiongozi Mkuu wa chama (Supreme Leader of the Party) na Kiongozi wa chama (Leader of the party); Kiongozi wa chama vs Mwenyekiti wa chama; mifano kutoka nchi mbalimbali duniani; Chama dola au si chama dola?
e) Dhana ya waasisi na wavamizi ndani ya ACT-TANZANIA/WAZALENDO; Je ni kweli kuna waasisi na wavamizi ndani ya ACT-TANZANIA / WAZALENDO? Nani walivamia na nani walivamiwa? ACT na msajili wa vyama kunani? Kwa nini maamuzi yale kutoka kwa msajili? Nini kiko nyuma ya pazia? Ushahidi kutoka jikoni
f) Uzinduzi wa ACT-TANZANIA / WAZALENDO; Kwa nini uzinduzi wa chama ulichelewa? Nini kilichelewesha uzinduzi na kwa nini? Mkutano mkuu wa chama; washiriki wa mkutano mkuu wa chama, washiriki au kiinimacho? Wapi walitoka? Ushahidi kutoka jikoni
g) Mapato na matumizi ndani ya ACT-TANZANIA/WAZALENDO; Tutaangazia vyanzo vya mapato ya chama hiki tangu kianze mwaka jana hadi hii leo; gharama za mkutano mkuu wa ACT-TANZANIA / WAZALENDO, nani alilipa gharama na kwa nini? Gharama za ziara ya kwanza ya kutambulisha chama mikoani (mikoa 10/11?) nani aligharimia ziara hizo na kwa nini? Je ziara awamu ya pili inaanza lini? Kwa nini ziara ya kutambulisha chama mikoani awamu ya pili imechelewa? Je tatizo ni gharama au kujipanga? Nani anakusudia kugharamia ziara awamu ya pili? Ushahidi kutoka jikoni.
Hili ni eneo ambalo limekuwa na maswali mengi kiasi kwamba hata wahusika wenyewe wamekuwa wakiulizwa vyanzo vya mapato wamekuwa ama wakikwepa kujibu au wanatoa visingizio. Duru tunasema sasa kila kitu kitawekwa wazi na ushahidi wa nyaraka zote na miamala, mawasliano ya barua, mazungumzo, minutes za vikao n.k vitawekwa hapa kwa ajili ya kuhakiki. Habari zote zinatoka jikoni na katika vyanzo vya uhakika.
f) Tutaangalia kuhusu mengineyo mfano katiba ya ACT-TANZANIA / WAZALENDO; Mabadiliko iliyopitia; Ushiriki wa ACT-TANZANIA / WAZALENDO katika uchaguzi wa serikali za mitaa, 2014; ushiriki wa ACT-TANZANIA / WAZALENDO katika Uchaguzi mkuu mwaka huu; uhusiano wa ACT-TANZANIA / WAZALENDO na vyama vingine vya upinzani hususani vyama vinavyounda UKAWA; uhusiano wa ACT-TANZANIA / WAZALENDO na CCM na mambo mengine mengi kama muda utaturuhusu duruni.
Uwazi na ukweli ndio dira yetu katika duru; unafiki kwetu mwiko. Tutasema kweli daima kwa ajili ya maslahi ya taifa, na sio kwa ajili ya maslahi binafsi ya genge la watu wachache au wachumia tumbo. Kila mnafiki tutamuumbua, na mkweli tutamuenzi katika duru zetu hizi.
Tusemezane; stay tuned, coming up soon! Tafadhali usiache kuchungulia humu JF mara kwa mara