Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,933
- 34,912
Hamjambo wanaJF.............Kwa wale na wanachama wa chama cha MABADILIKO na UWAZI(ACT-Wazalendo) Tusemezane hapa...............
UTANGULIZI
Kuhusu ACT
Itikadi
ACT-Tanzania ni chama cha siasa nchini Tanzania kinachoamini katika misingi ya Ujamaa Demokrasia (Democratic Socialism).
Misingi mikuu ya ujamaa wa kidemokrasia ni undugu, usawa, uhuru, heshima kwa kila mtu na demokrasia.
ACT-Tanzania inatambua kuwa sisi wananchi wa Tanzania ndiyo raslimali kubwa ya nchi, na kwamba nchi yetu imejaliwa raslimali nyingi ambazo zikivunwa na kutumika vizuri
zinaweza kuboresha maisha na kuchangia katika maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.
Hivyo basi, shabaha kuu ya ACT-Tanzania ni kuhakikisha kuwa utajiri wa nchi unatumika kuboresha maisha ya watu na kuchochea uwezo wao katika kuchangia kujenga
uchumi shirikishi ambapo kila mtu ana fursa sawa za maendeleo.
Ngao za Ujamaa wa Kidemokrasia
Ngao tatu za Ujamaa wa kidemokrasia (Democratic Socialism) kwa mujibu wa ACT-Wazalendo ni:
I) Undugu ni hifadhi ya jamii ya asili kwa Afrika, na hivyo kila mtanzania na kila mwafrika ana jukumu la kumsaidia mwenzake anayekabiliwa na tatizo au janga popote alipo
bila kutarajia malipo ya aina yeyote
II) Serikali ina haki na wajibu wa kutengeneza sheria na kanuni zenye kulenga kuleta usawa wa kibinadamu katika jamii. Aidha, Serikali ina haki na wajibu wa kusimamia
moja kwa moja sekta nyeti katika jamii zenye maslahi mapana ya kiusalama na kiuchumi kwa nchi
III) Viongozi na watumishi wa umma wana wajibu wa kuhakikisha kwamba wanaishi na kuenenda katika misingi inayalinda heshima ya ofisi za umma na kwamba hawatumii
nafasi zao kwa manufaa yao binafsi na jamaa zao.
Ili kuwasaidia na kuwawezesha viongozi na watumishi wa umma kuenenda katika misingi ya uadilifu, kuna haja ya kuwekewa miiko na maadili maalumu ya viongozi
Falsafa
Falsafa ya ACT Tanzania ni UNYERERE, ikiwa ni dhamira ya kurudisha, kuhuisha na kupigania misingi mama iliyoasisi Taifa la Tanzania, kama ilivyoanishwa katika Azimio la
Arusha na kwa mazingira ya Tanzania ya sasa.
A) Bendera ya Chama yenye rangi ya Zambarau, ambayo ndio alama kuu ya Chama. Rangi hii inawakilisha taswira ya mchanganyiko wa wanachama kutoka kona na pembe
zote za nchi; utambuzi wa umuhimu wa wanawake na familia katika jamii; na alama ya kujali makundi yenye mahitaji maalum katika jamii wakiwemo watu wenye ulemavu,
watoto na wazee.
B) Bendera ya Taifa ikiashiria uzalendo, upendo na utayari wa kulilinda na kulitumikia Taifa la Tanzania.
C) Mkono uliofunguka ukiashiria Uwazi.