Ifaham CCM mpya, chama cha wanachama, chama cha watu

Jan 23, 2017
10
10
Mwandishi, Shabani Shabani.

Shabanishabani3@gmail.com/0758321964.

CCM ILIPOTOKA (HISTORIA).

Kikao cha pamoja cha Halmashauri Kuu ya Tanganyika African Nation Union (TANU) chama cha siasa kutoka Tanganyika na Afro Shirazi Party (ASP) Chama cha siasa kutoka Zanzibar, Kikao kilichoketi Dar es salaam Tarehe 21/01/1977, Kilichoongozwa na uenyekiti wa pamoja Rais wa TANU Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa ASP Ndugu Alhaji Aboud Jumbe.Kikao hicho cha kihistoria ndicho kikao kilichokubaliana rasmi kuvunja vyama vya ASP na TANU na kuunda Chama kimoja kiitwacho Chama Cha Mapinduzi.

Chama Cha TANU kilishiriki sana katika kuleta Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Muingereza. Na ASP imeshiriki kikamilifu katika kufanikisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar 1964 na kuhakikisha uhuru kwa watu wote unapatika visiwani Zanzibar. Hivyo vyama hivi vilivyounda Chama Cha Mapinduzi vinahistoria ya kipekee katika ukombozi wa Tanzania kutoka katika makucha ya wabepari.

Ndugu Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi na kikao kilichofanyika tarehe 21/01/1977 wakati akitoa neno la shukrani kwa wajumbe Ndugu Alhaji Aboud Jumbe alisema “ Chama kinachoanzishwa ni Chama Cha Mapinduzi maana ya mapinduzi ni mabadiliko makubwa hivyo utekelezaji wa majukum tunayokabidhiwa lazima uwe katika kiwango cha juu, mapinduzi siyo lelemama na wala siyo mchezo isipokuwa ni mapambano ya hali ya juu ya kugeuza mambo ili yawe mazuri na bora zaidi”. Nukuu hii inaonyesha umuhimu wa kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi na kazi kubwa ambayo chama kinatakiwa kuifanya kwa manufaa ya watanzania wote ili kubadili maisha ya wananchi yawe bora zaidi.

Siku ya Sherehe za kuundwa kwa Chama Cha Mapinduzi 05/02/1977 ambazo zilifanyika katika uwanja wa Amani Mjini Zanzibar mwenyekiti wa kwanza wa CCM Mwalimu Julius Nyerere alisema yafatayo; “Vilevile lazima Chama Cha Mapinduzi kiwaongoze wananchi katika kazi ngumu kuliko zote; Mapambano yatakayoleta uhuru wa ndani; uhuru wa kila mwananchi binafsi,siyo uhuru wa nchi tu. Chama chetu kipya kinapaswa kuongoza katika juhudi za maendeleo ya kiuchumi, na ya uhuru wa kweli wa kila binaadamu, ndani ya misingi ya nchi ambayo imani yake ni usawa, heshima na ushirikiano wa binaadamu.”

Nukuu hizo za waasisi wa Chama Cha Mapinduzi zinafanana kimaana na lengo nikuonyesha uzito na umuhimu wa CCM katika kufanikisha maendeleo ya watanzania.

CCMMPYA.

Maono ya waasisi wakati wa kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwa sasa yameonyesha kuishi kwa vitendo chini ya mwenyekiti wa CCM Dk John Pombe Magufuli na ndio msingi na maana halisi ya CCM MPYA katika nyakati hizi.

CCM MPYA ni kauli mbiu inayotumiwa na CCM katika kuelezea dhana ya Mageuzi makubwa yanayofanywa na CCM wakati huu msingi mkubwa wa mageuzi yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha kila mwanachama na mwananchi anahisi Chama Cha Mapinduzi ni Chake. Wale wasio na sauti na wanyonge waone Chama Cha Mapinduzi kuwa kimbilio lao na ndio kuirejesha CCM katika misingi ilivyokusudiwa na waasisi wake.

Chama Cha Mapinduzi kimefanya mageuzi makubwa ya kimuundo, Kiuongozi na Kiutendaji na hayo yameenda sambamba na mabadiliko ya katiba ya CCM tarehe 12/03/2017.
Katika eneo la mfumo au muundo wa CCM. CCM imepunguza idadi ya vikao. imepunguza idadi ya wajumbe wa vikao, Jumuiya zote za CCM uendeshaji wake na mali zake zitasimamiwa na CCM lakini kubwa zaidi uzito mkubwa umewekwa katika kuimarisha mashina ya CCM, eneo hili ndio kuna wapiga kura na wanachama wa msingi, kwa kufanya hivyo CCM inakuwa karibu na watu na watahisi kiuhalisia kuwa ni chama chao na siyo chama cha viongozi au kikundi kidogo cha watu.

Katika eneo la uongozi wa CCM. CCM imesisitiza kuwa na viongozi waadilifu, waaminifu, wachapakazi, wanaochukia rushwa na wapenda watu.Lakini kubwa zaidi CCM imesisitiza cheo kimoja mtu mmoja mfano ukiwa mbunge huwezi kuwa Mwenyekiti wa Chama wilaya kwa wakati mmoja.Eneo lingine kwenye uongozi, CCM imesisitiza kila mwanachama ana haki sawa ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yoyote ya uongozi ambayo anazosifa zinazostahili, Katika hili CCM imeonya msisitizo mkali katika suala la viongozi kupanga safu zao za uongozi kwa manufaa yao, Katibu wa Halmashauri kuu Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole amenukuliwa maeneo mbalimbali akisema “Atakayepanga (Safu za viongozi) na atakayepangwa (kwenye nafasi za uongozi) wote watakula panga”. Nukuu hii ya Ndugu Humphrey Polepole inatafsiri kuwa wanachama wa CCM wanatakiwa waachwe uhuru wachague viongozi wanaowataka na kuwakubali bila kupangiwa na mtu yoyote.

Katika eneo la utendaji wa CCM. CCM imesisitiza kuwa na watendaji wevye vigezo vya kiutendaji kama vile uweledi wa kutosha, uzoefu ikiwa na maana kwamba kwa kushiriki kwa muda mrefu katika siasa za Chama Cha Mapinduzi au kwa kushiriki mara nyingi katika siasa za CCM na kujitoa au kujidhatiti katika shughuli za Chama.

Mageuzi haya makubwa yanayofanywa na CCM yamelenga kuongeza tija, ufanisi. uwajibikaji, kupunguza gharama za uendeshaji, kupiga vita rushwa, ubadhirifu wa mali za chama na umma,Kuimarisha chama kiuchumi kiweze kujitegemea, kudumisha umoja, kuongeza na kutoa viongozi wa mfano na wenye sifa zinazotosheleza.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dk.John Pombe Joseph Magufuli katika kuwekea msisito Mageuzi ya CCM alisema tarehe 13/12/2016 kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM “Napenda tuwe na chama kinachoongozwa na wanachama na sio chama kuongozwa na mtu chama ni mali ya wanachama”.

Mwisho mageuzi makubwa yanayofanywa na CCM siyo nadharia au maneno yasiyo na vitendo hapana ni jambo ambalo ni kweli na wala siyo la mzaha au ubazazi. Hatuwezi kukataa kwamba mageuzi haya kuwa hayata kumbana na changamoto kwa asili mageuzi yanaugumu wake ila ni marahisi kama wanachama wengi wa CCM pamoja na wananchi wengi wataendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM). Naamini kwamba CCM ambayo imepewa ridhaa ya kuongoza nchi ikiwa katika mstari sahihi na kuimarika basi haitachukua muda mrefu Tanzania itaimarika, na watanzania wataimarika katika nyanja zote kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni. Mageuzi makubwa ya CCM ni muhimu kwa wanaCCM na wananchi wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
CCM YA SAHIVI NI CCM YA MTU MMOJA...km huamini angalia uteuzi wa wagombea wa ccm ktk nafasi zote za udiwani na ubunge wote ni agizo.sahv hakuna neno ccm hata mkapa mwenyewe aliona hlo akaonya serikali ijitambulishe km serikal ya ccm c ya mtu fulani
 
Ama kweli Akutukanaye hakuchagulii tusi ! chama cha wanachama kinawezaje kupitisha wasaliti kugombea ubunge na udiwani bila kufuata mchakato wa chama ?
IMG-20180811-WA0018.jpg
 
Ama kweli Akutukanaye hakuchagulii tusi ! chama cha wanachama kinawezaje kupitisha wasaliti kugombea ubunge na udiwani bila kufuata mchakato wa chama ?
View attachment 847245
Hata mimi nashangaa hawa wanasiasa!!! Ama kweli nyani haoni kundule!!! Lowassa wenu alipita kw mchakato gani??? Tena mkamwamini kabsa mkampa nafas nyet hvyo kuongoza nchi leo wewe unashangaa nini??? Acha unafk!!!
Mlifurahia kipind hcho leo mapovu ya nini???? What goes around comes around!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa sijaona faida ya hii CCM unayo ipamba humu.
Imetuletea all types of criminals.
Imetuzalishia mapunguani chungu mzima mitaani huku.
Malimbukeni kibao...
Sijui unajaribu kum brainwash nani na hizi nonsense ulizo bandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hauwezi kuiona kweli kabisa dogo. CCM hii hii inatupeleka Kilimanjaro kwa shilingi elfu tisini, CCM hii hii imetutoa kwenye kusafiri kwenda Mwanza kwa kupitia Nchi jirani na sasa tunakwenda kwa kuteleza kupitia singida. CCM hii hii imewafanya muweze kushinda kwenye mitandao siku nzima kwa maana ya masaa 24 na kazi hamtaki kufanya. CCM ndiyo chama pekee Nchi hii kamq hufahamu. Leo hii CDM au hata chama cha Zitto tukakipa uongozi itakuwaje? Nani atakuwa nani? Kwa TZ hakuna kama CCM mkuu wangu. Ni kujidanganya tuu. Hatuna upinzani madhubuti.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwandishi, Shabani Shabani.

Shabanishabani3@gmail.com/0758321964.

CCM ILIPOTOKA (HISTORIA).

Kikao cha pamoja cha Halmashauri Kuu ya Tanganyika African Nation Union (TANU) chama cha siasa kutoka Tanganyika na Afro Shirazi Party (ASP) Chama cha siasa kutoka Zanzibar, Kikao kilichoketi Dar es salaam Tarehe 21/01/1977, Kilichoongozwa na uenyekiti wa pamoja Rais wa TANU Mwalimu Julius Nyerere na Rais wa ASP Ndugu Alhaji Aboud Jumbe.Kikao hicho cha kihistoria ndicho kikao kilichokubaliana rasmi kuvunja vyama vya ASP na TANU na kuunda Chama kimoja kiitwacho Chama Cha Mapinduzi.

Chama Cha TANU kilishiriki sana katika kuleta Uhuru wa Tanganyika kutoka kwa Muingereza. Na ASP imeshiriki kikamilifu katika kufanikisha Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar 1964 na kuhakikisha uhuru kwa watu wote unapatika visiwani Zanzibar. Hivyo vyama hivi vilivyounda Chama Cha Mapinduzi vinahistoria ya kipekee katika ukombozi wa Tanzania kutoka katika makucha ya wabepari.

Ndugu Alhaji Aboud Jumbe Mwinyi baada ya kuchaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi na kikao kilichofanyika tarehe 21/01/1977 wakati akitoa neno la shukrani kwa wajumbe Ndugu Alhaji Aboud Jumbe alisema “ Chama kinachoanzishwa ni Chama Cha Mapinduzi maana ya mapinduzi ni mabadiliko makubwa hivyo utekelezaji wa majukum tunayokabidhiwa lazima uwe katika kiwango cha juu, mapinduzi siyo lelemama na wala siyo mchezo isipokuwa ni mapambano ya hali ya juu ya kugeuza mambo ili yawe mazuri na bora zaidi”. Nukuu hii inaonyesha umuhimu wa kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi na kazi kubwa ambayo chama kinatakiwa kuifanya kwa manufaa ya watanzania wote ili kubadili maisha ya wananchi yawe bora zaidi.

Siku ya Sherehe za kuundwa kwa Chama Cha Mapinduzi 05/02/1977 ambazo zilifanyika katika uwanja wa Amani Mjini Zanzibar mwenyekiti wa kwanza wa CCM Mwalimu Julius Nyerere alisema yafatayo; “Vilevile lazima Chama Cha Mapinduzi kiwaongoze wananchi katika kazi ngumu kuliko zote; Mapambano yatakayoleta uhuru wa ndani; uhuru wa kila mwananchi binafsi,siyo uhuru wa nchi tu. Chama chetu kipya kinapaswa kuongoza katika juhudi za maendeleo ya kiuchumi, na ya uhuru wa kweli wa kila binaadamu, ndani ya misingi ya nchi ambayo imani yake ni usawa, heshima na ushirikiano wa binaadamu.”

Nukuu hizo za waasisi wa Chama Cha Mapinduzi zinafanana kimaana na lengo nikuonyesha uzito na umuhimu wa CCM katika kufanikisha maendeleo ya watanzania.

CCMMPYA.

Maono ya waasisi wakati wa kuanzishwa kwa Chama Cha Mapinduzi kwa sasa yameonyesha kuishi kwa vitendo chini ya mwenyekiti wa CCM Dk John Pombe Magufuli na ndio msingi na maana halisi ya CCM MPYA katika nyakati hizi.

CCM MPYA ni kauli mbiu inayotumiwa na CCM katika kuelezea dhana ya Mageuzi makubwa yanayofanywa na CCM wakati huu msingi mkubwa wa mageuzi yanayofanywa na Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha kila mwanachama na mwananchi anahisi Chama Cha Mapinduzi ni Chake. Wale wasio na sauti na wanyonge waone Chama Cha Mapinduzi kuwa kimbilio lao na ndio kuirejesha CCM katika misingi ilivyokusudiwa na waasisi wake.

Chama Cha Mapinduzi kimefanya mageuzi makubwa ya kimuundo, Kiuongozi na Kiutendaji na hayo yameenda sambamba na mabadiliko ya katiba ya CCM tarehe 12/03/2017.
Katika eneo la mfumo au muundo wa CCM. CCM imepunguza idadi ya vikao. imepunguza idadi ya wajumbe wa vikao, Jumuiya zote za CCM uendeshaji wake na mali zake zitasimamiwa na CCM lakini kubwa zaidi uzito mkubwa umewekwa katika kuimarisha mashina ya CCM, eneo hili ndio kuna wapiga kura na wanachama wa msingi, kwa kufanya hivyo CCM inakuwa karibu na watu na watahisi kiuhalisia kuwa ni chama chao na siyo chama cha viongozi au kikundi kidogo cha watu.

Katika eneo la uongozi wa CCM. CCM imesisitiza kuwa na viongozi waadilifu, waaminifu, wachapakazi, wanaochukia rushwa na wapenda watu.Lakini kubwa zaidi CCM imesisitiza cheo kimoja mtu mmoja mfano ukiwa mbunge huwezi kuwa Mwenyekiti wa Chama wilaya kwa wakati mmoja.Eneo lingine kwenye uongozi, CCM imesisitiza kila mwanachama ana haki sawa ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yoyote ya uongozi ambayo anazosifa zinazostahili, Katika hili CCM imeonya msisitizo mkali katika suala la viongozi kupanga safu zao za uongozi kwa manufaa yao, Katibu wa Halmashauri kuu Itikadi na Uenezi Ndugu Humphrey Polepole amenukuliwa maeneo mbalimbali akisema “Atakayepanga (Safu za viongozi) na atakayepangwa (kwenye nafasi za uongozi) wote watakula panga”. Nukuu hii ya Ndugu Humphrey Polepole inatafsiri kuwa wanachama wa CCM wanatakiwa waachwe uhuru wachague viongozi wanaowataka na kuwakubali bila kupangiwa na mtu yoyote.

Katika eneo la utendaji wa CCM. CCM imesisitiza kuwa na watendaji wevye vigezo vya kiutendaji kama vile uweledi wa kutosha, uzoefu ikiwa na maana kwamba kwa kushiriki kwa muda mrefu katika siasa za Chama Cha Mapinduzi au kwa kushiriki mara nyingi katika siasa za CCM na kujitoa au kujidhatiti katika shughuli za Chama.

Mageuzi haya makubwa yanayofanywa na CCM yamelenga kuongeza tija, ufanisi. uwajibikaji, kupunguza gharama za uendeshaji, kupiga vita rushwa, ubadhirifu wa mali za chama na umma,Kuimarisha chama kiuchumi kiweze kujitegemea, kudumisha umoja, kuongeza na kutoa viongozi wa mfano na wenye sifa zinazotosheleza.

Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Dk.John Pombe Joseph Magufuli katika kuwekea msisito Mageuzi ya CCM alisema tarehe 13/12/2016 kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM “Napenda tuwe na chama kinachoongozwa na wanachama na sio chama kuongozwa na mtu chama ni mali ya wanachama”.

Mwisho mageuzi makubwa yanayofanywa na CCM siyo nadharia au maneno yasiyo na vitendo hapana ni jambo ambalo ni kweli na wala siyo la mzaha au ubazazi. Hatuwezi kukataa kwamba mageuzi haya kuwa hayata kumbana na changamoto kwa asili mageuzi yanaugumu wake ila ni marahisi kama wanachama wengi wa CCM pamoja na wananchi wengi wataendelea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi (CCM). Naamini kwamba CCM ambayo imepewa ridhaa ya kuongoza nchi ikiwa katika mstari sahihi na kuimarika basi haitachukua muda mrefu Tanzania itaimarika, na watanzania wataimarika katika nyanja zote kiuchumi, kisiasa, kijamii na kiutamaduni. Mageuzi makubwa ya CCM ni muhimu kwa wanaCCM na wananchi wote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siioni CCM mpya kwa matendo, hiyo slogan ni yakutafutia kura lakini watu ni walewale na hivyo Chama ni kilekile

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tujitadhimini! Huyu bwana kadhibiti chama,mihimili yote,katiba na Uhuru binafsi,haki za binadamu.Amejipa u mungu Tanzania. Hatuna alie salama, tudai kwa pamoja katiba mpya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom