Penda kuwa dereva na usiwe abiria.
Hiyo ndio kanuni inayoniongoza katika maisha Dadangu.
Ukitumia kanuni hii basi Sonono na hali Kama hizo huwezi kupata.
Unapoanzisha mahusiano hakikisha wewe ndio unaya-kontroli. Kwa vile u mwanamke basi use indirect way of controlling u re relationship. Hakikisha asijue kuwa wewe ndiye unayaendesha hayo mahusiano.
Utawezaje kuwa dereva wa uhusiano?
Ni hivi; hakikisha asilimia kubwa ya furaha katika uhusiano wenu wewe ndiye unachangia. Yaani hiyo huitwa hisa ya furaha katika mapenzi. Isipungue 70% ya mchango wako katika kuongeza furaha ya mapenzi. Hizo 30% mwachie huyo mwenzako.
Hii humaanisha wewe ndio utakuwa mmiliki mkubwa wa furaha katika mahusiano yenu. Halikadhalika ukiwa nyumbani, ofisini au sehemu yoyote.
Siku usipokuwepo basi kwa vile wewe ndio mwenye hisa kubwa katika mahusiano na ndio umeondoka basi pengo lako linaonekana.
Hakikisha wewe ndio unahusika kwa kuanzisha vurugu, malumbano na ugomvi ndani ya mahusiano indirect.
Ujue kufanya uwiano baina ya kuleta furaha na huzuni ndani ya mahusiano.
Hakikisha unachukua hisa kubwa sehemu yoyote ulipo. Hii haitakugharimu kwani mambo yote wewe ndiye unayeratibu.
Lazima ujue kwa mwezi huu utaleta sokomoko gani katika uhusiano wenu na namna gani ya kuimaliza. Lakini lazima utumie indirect way ili mwenzako ndio ajione mwenye hatia.
Ahsante