If I fail, I try again, and again, and again

If I fail, I try again, and again, and again

Mungu Mkubwa.

Natumai siku inaenda vizuri kwa kila mmoja wetu,

Nilikua napitia video moja ya huyu kaka anaitwa Nick Vujicic (Ningependa kila mmoja amtafute google au youtube). Yaani nikifika kwenye point ya kukata tama, maisha ya huyu kaka yananiinua moyo sana.

Amezaliwa bila mikono wala miguu lakini kajikubali na hajaruhusu hali yake imrudishe nyuma. Anafanya vitu ambavyo hata wengi wetu wenye viungo vyote vya mwili tunashindwa fanya.

Ata siku moja tusiruhusu madhaifu yetu yaturudishe nyuma kwenye mahusiano, familia, taaluma ata kwenye elimu na kwenye jamii. Mungu hakukosea kutuumba hivi na kamwe tusijitafutie kasoro. Badilisha unavyojiona mwenyewe na utafanikiwa sana, siri ni kujiamini, kua jasiri na usikate tamaa na zaidi mtangulize Mungu katika maisha yako.

View attachment 481536View attachment 481537View attachment 481539View attachment 481540View attachment 481541View attachment 481542View attachment 481543View attachment 481544View attachment 481545
 
Kuna kipindi cha TV kilionyesha maisha ya huyu kaka, kiliitwa 'born without limbs'

Mke wake alieleza anavyompenda mumewe pamoja na changamoto zote.

Niliamini kila mtu ana mtu wake hapa duniani na mapenzi ya kweli yapo
 
Kweli kabisa! Haijalishi unajiona una kasoro ya namna gani,! Kuna mtu yupo kwa ajili yako.
 
Kuna kipindi cha TV kilionyesha maisha ya huyu kaka, kiliitwa 'born without limbs'

Mke wake alieleza anavyompenda mumewe pamoja na changamoto zote.

Niliamini kila mtu ana mtu wake hapa duniani na mapenzi ya kweli yapo
Ata website yake inaitwa hivyo.
 
Siri ya kufanikiwa ni kuanza na kile ulichonano,hicho hicho ulichonacho
Kweli kabisa... Unakuta mtu anasubiri mpaka apate makubwa.! Unaambiwa ata ukiwa na elfu tano, anza kufanya kile elfu tano inaweza fanya... Nunua pipi panga sehemu na uuze... Polepole utajiona unapanda.
 
Great great great!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom