Msanii wa Filamu na Mwanamitindo Maarufu Nchini Tanzania ametangaza ujio wa Tamasha la Rangi Zinaongea litakalo fanyika Tarehe 23/05/2025 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kuionesha nembo ya Tanzania nje ya mipaka ya Tanzania ambapo itakuwa ni pamoja na kuonyesha Makala fupi inayo onyesha uzuri wa Nchi ya Tanzania na Vivutio vyake ambapo wameipa jina la Tanzania ya Samia.
Msanii wa Filamu Idris Sultan ametangaza rasmi ujio wa tamasha lake la rangi zinazazoongea litakalofanyika tarehe 23/05/2025 Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Akizungumza na waandishi wa Habari, Sultani amesema uzinduzi huo utaambatana na makala fupi itakayoonyesha uzuri wa nchi ya Tanzania pamoja na vivutio vyake vyote ambapo makala hiyo ameipa jina la Tanzania ya Samia