Idea ya Bodaboda Forums - Njoo Tuzungumze

Idea ya Bodaboda Forums - Njoo Tuzungumze

Amba Samedi

Senior Member
Joined
Apr 5, 2024
Posts
193
Reaction score
326
Habari wanadau,

Naandika kwa tumaini kubwa kuwa wote tunaendelea vizuri. Ni mchana na kuna kajoto hapa Morogoro. Nashukuru Mola kwa nafasi nyingine ya kupigana. Tuendelee kupambana, kwani iko siku.

Mwezi Mei mwaka 2018, nilikaribishwa na mwandishi mmoja maarufu ambaye alikuwa ameombwa na baadhi ya viongozi wa bodaboda jijini Dar es Salaam waliokuwa wanatafuta njia ya kidigitali itakayowasaidia kusimamia taarifa zao.

Kwa bahati mbaya, mpango huo haukukamilika. Lakini wazo hilo halijawahi kunitoka.

Binafsi ni bodaboda. Huwa nabeba abiria mara moja moja. Nilichokiona, huduma nyingi za kisasa bado hazijawafikia madereva wengi, hasa waliopo mikoani.

Ndiposa kujiuliza: Je, tunawezaje kutumia teknolojia kugusa bodaboda wengi kuliko ilivyo sasa?

2. Nini Kinakosekana?
Bodaboda wengi bado wanapata changamoto
  • Kupata wateja ni kwa kubahatisha.
  • Hakuna mfumo rasmi wa kupata taarifa muhimu kuhusu usalama barabarani, sheria mpya, au huduma zinazopatikana (labda whatsapp na taariza za IG/FB, kwa walio na simu janja na wana moyo wa kufuatilia).
  • Kuanza maisha upya wanapohamia mji mwingine.

3. Huduma Zilizopo na Mapungufu Yake

Ni kweli, kuna baadhi ya mifumo tayari inasaidia. Boda mmoja hapa Morogoro ailisifia app ya Bolt. SIku moja, alikuwa home, akapata order ya mteja kupitia app—safari ya kutoka mjini Morogoro hadi Mzumbe.

Bei ilikuwa nzuri, akakubali, akamsafirisha mteja, na akapata hela. Wakati huo, wenzake walikuwa bado wanangoja abiria kijiweni.

Huo ni mfano halisi wa jinsi teknolojia inavyorahisisha maisha—unapata mteja bila maneno mengi.

Lakini sio kila boda ana simu janja. Na hata kwa wanaotumia Bolt, changamoto bado hazikosekani (sio kila mkoa Tanzania ina ride hailing app kama Bolt).

4. Pendekezo

Nina wazo: Jukwaa la kidijitali maalum kwa ajili ya waendesha bodaboda.
Sehemu ambayo wao wenyewe wanaweza:
  • Kujiandikisha na kufahamika rasmi.
  • Kujadiliana kwa uhuru kuhusu kazi zao
  • Kushirikiana taarifa kuhusu vituo, changamoto, na fursa
  • Kupata mafunzo kuhusu usalama, sheria na haki zao
  • Kujifunza kuhusu maeneo mengine wanapohamia
Tuliite Bodaboda Forums. Kitovu cha taarifa, mawasiliano na huduma. Inayoleta pamoja Bodaboda, mafundi, wauzaji, bima, shule za udereva na watoa huduma wengine.

Kwa ufupi, linaweza kufungua milango kwa:
  • Wauzaji wa pikipiki mpya au za mtumba. Mtu anatafuta tu chombo, analipia linasafirishwa hadi aliko.
  • Kampuni za bima na watoa msaada wa kisheria
  • Shule za udereva na taasisi za elimu ya usalama
  • Vikundi vya kuweka na kukopa (vikoba), SACCOs, na taasisi za mikopo
  • NGOs au taasisi za serikali zinazotaka kuwafikia bodaboda moja kwa moja
Na kila bodaboda atapata taarifa zinazohusu utendakazi wake kwa wakati na kwa uhakika.

Tujadiliane Sasa​

Haya ni baadhi tu ya mawazo niliyonayo. Sina majibu yote—lakini naamini hii inaweza kuwa hatua ya kwanza kujenga kitu cha maana.

Kama wewe ni dereva wa bodaboda, mmiliki wa pikipiki, unatoa huduma kwa bodaboda, au una interest yoyote kwenye sekta hii—hebu tuongee.

Kuna teknolojia/mfumo wowote wa Bodaboda humu Tanzania niliousahau?

Tutumiaje teknolojia kurahisisha maisha ya waendesha bodaboda Tanzania?
 
Kuhusu kupata wateja app kama Uber Bolt Farasi zingesaidia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom