.IDD SIMBA CHADEMA HAWEZI KUKUBALIWA KAMWEEEEEEEEEE
Nakataa, nakataa, nakataa japokuwa mimi ni kidampa tu CDM, lakini ninaamini kabisa Idd Simba akiomba kuhamia CDM atakataliwa kama vile mtu anayeumwa kichaa cha mbwa anavyoyakataa maji.
Ikumbukwe kwamba CCM imezalaurika mbele ya jamii kwa mtindo huo huo wa kukiuka maadili yake iliyojiwekea kwamba uadilifu ni moja ya vigezo vya watu kukubalika kukiongoza. Baada ya waasisi wa chama hicho kutangulia kwenye haki, basi wahuni wakakivamia chama chetu tunachokipenda matokeo yake sisi wakulima , wafanya kazi, wavuvi na wakwea minazi tukawa siyo kitu mbele ya chama cha CCM.
Baada ya matajiri kukivamia chama hicho ndipo kimepoteza mvuto kabisa na sasa kinakufa pole pole, wakati ule watu kama hao walikuwa hawakubaliki kamwe, sasa Idd Simba aende CHADEMA akafanye nini?
Watu wafuatao kwa tabia zao hawafai kabisa kuwa viongozi wa chama chochote iwe CCM, CHADEMA CUF n,kna wakiwa viongozi wa vyama kati ya hivyo nilivyovitaja basi chama hicho kitakufa polepole kama mtu afae kwa corbon monoxide poisoning.
I. IDD SIMBA
II. ROSTAM AZIZ
III. ADEN RAGE
IV. ANDREW CHENGE
V. KARAMAGI
Na wengine ongezea. ( muliokaribu na Nape Nnawie mwonyesheni asome haya.)