Kutoka Bahari Beach Hotel: Yaliyojiri katika Mapokezi ya Edward Lowassa kujiunga CHADEMA

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
557
500
Habari wakuu,
Leo Jumanne, tarehe 28 Julai, 2015, chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kitampokea rasmi Edward Lowassa kuwa mwanachama wake mpya kutoka chama tawala, tukio hili pia litahudhuriwa na viongozi wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA). Tuwe sote kujuzana yanayojiri katika mapokezi haya.

=============

Updates

Waheshimiwa washaingia tayari
Shughuli imeshaanza na Salum Mwalim anawatambulisha wageni, wapo Freeman Mbowe, Ibrahim Lipumba, Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa na wengineo. Kwa leo mwenyeji kwa siku ya leo ni Mheshimiwa Mbowe. Makaidi anasubiriwa ambae ataingia muda wowote na Lowassa anakaribishwa.

Lowassa: Hizi microphone za hapa ni sawa na hirizi, ni nyingi sana. Ni muda umepita tangu yaliyotokea Dodoma, nimetumia muda huu kutafakari kwa kina yaliyotokea Dodoma na hatma yangu. Ninajua watu wengi wanaoniunga mkono wamekuwa wakinisubiri muda mrefu, wamesema nifanye maamuzi magumu. Tulipokua Arusha nilitangaza nia yangu ya kuondoa umasikini Tanzania, pamoja na yaliyotokea Dodoma, nia yangu iko palepale.

Anamshukuru mwenyezi Mungu kwa kuendelea kuwa wazima, anamshukuru kipekee mkewe Regina na watoto wake pamoja na wanafamilia, anawashukuru maefu ya wanachama wa CCM waliomuunga mkono kumpa udhamini, wakati wa ziara zangu nilikutana na umati mkubwa sana uliojitokeza kuniunga mkono. Anawashukuru viongozi wa dini zote nchini katika maombi ya kumuunga mkono.

Mchakato wa kuteua wagombea CCM ulikumbwa na mizengwe na zaidi Uchaguzi wa CCM ulifanywa kwa upendeleo na chuki iliokithiri dhidi yangu. Kilichotokea Dodma ni kupora mamlaka ya kamati kuu, watoto wa mjini wa wanasema ni kubaka demokrasia. Niliwekewa mizengwe na majungu kuhakikisha jina langu halifikishwi kamati kuu. Ni dhahiri njama dhidi yangu si jambo jipya, kumekuwa na mkakati wa siku nyingi wa kulichafua jina langu kwa uzushi na uwongo. Kwa namna ya kipekee napenda kuwapongeza Kingunge, Nchimbi, Sophia na Kimbisa waliokuwa tayari kuitetea katiba ya CCM. Viongozi walikuwa tayari kupanda mbegu ya chuki na mifarakano, yaliyotokea Dodoma yameitia dosara nchi yetu.

Kwa kifupi naamini sikutetendewa haki katika mchakato mzima wa kuteua majina. Nimenyimwa haki ya unapotuhumiwa unajitetea, natural justice. Nitakuwa naendelea kujidanganya mimi mwenyewe na kuwa mnafiki kama nitasema nina imani na CCM na kusema CCM kitakuwa chama kitakuwa ni chama kitachowaletea ukombozi wa kiuchumi na kisiasa. CCM niliyoiona Dodoma sio chama kile nilichokulia na kilichojengwa katika misingi ya haki, usawa na uadilifu, ni dhahiri CCM imepotoka na kuwa na maadili ya kuendelea kuiongoza Tanzania, nasema sasa basi, kama mwalimu Nyerere alivyosema CCM sio baba yangu na wala si mama yangu na alisema mkikosa mabadiliko ndani ya CCM, mtayapata nje ya CCM hivyo basi baada ya kutafakari kwa kina nimeamua kuanzia leo naondoka CCM na kuitikia wito wa UKAWA kupitia CHADEMA kuungana nao katika kuleta mabadiliko ya kweli. Na anawashukuru viongozi wa vyama vya upinzani kwa imani yao wa kuthamini mchango ninaoweza kutoa kufanikisha azma ya kuwaletea mabadiliko ya maendeleo ya nchi yetu.

Natoa wito kwa watanzania wenye nia njema, kujiunga nasi katika kujenga nchi yetu na kuleta maendeleo ya taifa, Nawaomba kujiunga nasi katika safari hii ya matumaini, safari inaendelea kuwepo kwa kupitia UKAWA, lakini safari hii haiwezi kukamilika bila kujiandikisha hivyo twende kujiandikisha. Nimesikia tetesi wanakaribia kufunga, naomba tume ya uchaguzi waongeze muda kama walivyoongeza Njombe ili wakazi wote wa Dar waweze kujiandikisha. Asanteni kwa kunisikiliza.

Deodatus Balie: Wapo walioanza kusema tangu zilipoanza tetesi kwamba utahamia UKAWA. Kwanza mheshimiwa Lowassa unahama kwenda kulipiza visasi endapo utashindi lakini la pili wapo wanaosema uko karibu sana na matajiri wengi katika nchi hii, kwa hio ukishinda utahamishia utajiri wa nchi hii katika mifuko ya hao matajiri, Je! Una lipi la kuzungumza katika hili?

Lowassa: Naanza na li mwisho juu ya matajiri, mimi nachukia sana umasikini, moja ya sababu ya kutafuta urais ni kuondoa umasikini, natamani watanzania wawe matajiri, wawe kama kina Mengi na mzee wa Azam. Marekani kuna matajiri wengi, wamekuwa wanafanya nini, wanawatupa chooni?

Wanaosema nalipa kisasi ni upuuzi, wewe umefanya nini mpaka uogope kulipiwa kisasi, waulizeni wamefanya nini mpaka waogope mimi kulipa kisasi. Lakini mimi ni mkristo, najua mashaka yao, samehe saba mara sabini hivyo kama wana madhambi yao wakamuombe tu Mungu wao.
====

Kadi inaanza kukabidhiwa kwa mama Lowassa, mama Regina Lowassa. Na sasa anakabidhiwa mbunge wa Monduli na mwenyekiti wa CHADEMA

Hellen(Times FM): Wakati wa kashfa Richmond ulikua na tofauti na hivi vyama, Je usipotimiza walivyotarajia, una imani upendo huu utaendelea milele?

Mwambungu (Habari cooperation): Je, Ikiwa watanzania watawapeni ridhaa, tumeshuhudia bunge letu limepisha sheria mbovu na mikataba, mtabadilisha hilo?
Lowassa: Naona hili panoge tushirikiane sote, namp
Tutumie rasilimali kwa wananchi wote, mikata na mikataba iliopitishwa itatazmwa upya ili wananchi wote tunufaike na rasilimali hizi

Makaidi: Tutaangalia sababu walizopitishia na tuone ni kwa nia njema au mbaya na ikiwa mbaya tutafumua sheria zote.

Mbowe: Kama tuna hasara moja kubwa tunaipata kama taifa, ni kuwa na bunge linalotoka kutoka chama kimoja, absolute majority. Kwa namna CCM kimekuwa na wabunge wengi, kimekuwa kinaangalia maslahi ya chama chao kuliko ilivyo kwa taifa. Bunge la kumi na moja litakuwa na uwiano wa kuridhisha hivyo watu watashindwa kufanya maamuzi kwa maslahi ya vyama vyao

Mbatia: Rasimu ya pili ya katiba yetu ambayo ndio imetufanya kuwepo UKAWA. Tunawahahakishia watanzania, tutaweka mfumo wa kikatiba kwamba serikali yoyote itayokuwa madarakani ifate maagizo ya Bunge. Nashukuru sana Lowassa kujiunga

Lowassa: Am sick of Richmond, mtu yoyote mwenye ushahidi wa mimi kuhusika Richmond aende mahakamani, kama huna just shut up. Nilichukua uamuzi kwa niaba ya serikali.

Nimeondoka madarakani miaka nane iliopita, mambo haya yameongezeka yamepungua, mikono yangu ni misafi na mtu mwenye ushahidi acha kupigapiga kelele, peleka mahakamani

MANENO KUTOKA VYAMA VINAYOUNDA UKAWA
Makaidi: Salamu zangu fupi tu, kwanza kwa bwana Mbowe nimpongeze kwa kuweza kutuletea kifaa, bwana Lowassa na nampongeza Lowassa baada ya kuona kiza mbele akaamua kuja kwetu, simfahamu sana mzee Lowassa lakini namfahamu kupitia kwa mwanangu amefanya kazi na Lowassa. Viongozi wa UKAWA tutakuwa pamoja nae kuhahakisha CCM mnaondoka, kwa pamoja tutaweza kuiondoa CCM tarehe 25 Oktoba. Nashukuru sana Lowassa kuamua, ukiona njia ina matatizo, unabadilisha. Kama amekuja kutukwamua, watu wote tutamsikiliza.

Juma Duni(CUF): Lazima niseme nimepigwa na butwaa, Lowassa karibu katika UKAWA na tumepata fahari, na kwa lugha ya kisasa tumepata jembe na Oktoba patachimbika, CCM wamesahau kabisa hata malengo ya kugombea uhuru. Tuna wajibu pamoja wewe kurudi katika misingi ya kupigania uhuru nchi hii na leo nimefurahi kusikia na wewe umasikini huupendi. Sote tuliokaa hapa ni watoto wa masikini, Lowassa tunapata fahari kubwa kuwa nawe, CUF tutashirikiana. Mkapa alisema Zanzibar hakuna mtu mwenye hatimiliki ya nchi hii, hamna kikundi chochote kina hatimiliki wa nchi hii.

Mbatia: Haki zako kama waziri mkuu ukihamia UKAWA haziondoki, UKAWA tutazilinda. Mpaka leo UKAWA tupo pamoja, watanzania wameshinda, tutahakikisha Tanzania bila CCM itawezekana. KANU iliondoka Kenya 2002 na Kenya bado ipo na tunaamini mwafaka wa kitaifa ambapo taifa letu hili lina ombwe la uongozi. Tunatoa rai kwa wale wote ambao wanaona ovu la CCM, wajiunge na UKAWA. Mzee Lowassa historia itakukumbuka kwa ujasiri wako. Wana usalama wanalipa kwa kodi za watanzania wote na sio za CCM, nawaomba wafatilie mchakato huu kwa uadilifu. Tutatumia hekima, umoja wa watanzania na tuwahahakikishia amani, hatutamwaga damu lakini wasituchokoze. Naamini hatua hii tuliofikia, mama Tanzania kwanza, vayama vya siasa baadae.

Mshehereshaji: Sasa ni wakati wa kumsikiliza mwenyeji wetu hapa, mheshimiwa Mbowe.

Mbowe: Leo kwa niaba yangu, viongozi na wanachama wote wa CHADEMA, tumependa kwa dhati kukukaribisha Lowassa na familia yako. Ujio wako umezua hofu kwani hili ni taifa la hofu. Nimesema hofu kwani imeanzia katika chama chako, wamekuwa wakinipigia simu kwa muda mrefu kuwa mnampokea huyo, atawaharibia chama na mimi nikawahahakishia kwa nguvu zote kuwa Lowassa hawezi kuhamia CHADEMA tena nikasema kwa kizungu 'over my dead body'. Nikajiuliza tangu lini wanaitakia mema CHADEMA, nikajua ni urafiki wa mashaka.

Hofu hii haijaishia kwa CCM bali imeingia hadi CHADEMA, chama hiki ni chetu sote. Chama hiki sio mahakama, simsemi Lowassa ni mtakatifu, nani mmoja wetu humu ndani ni mtakatifu achukue mawe amrushie mwenzake. Taifa hili haliwezi zaidi ya miaka 20, kulipa visasi, kumleta Lowassa katika meza hii haikuwa shughuli nyepesi, tumefanya mashauriano mengi. Eti kwa kuwa tuliwahi kumuita Lowassa mtu mchafu hatuwezi kumkarisha hasa bila ushahidi wa wazi.

Ndo mara ya kwanza mtu aliefikia waziri wa waziri mkuu kuhama CCM, nchi yetu inahitaji mkakati mpya, inahitaji fikra mpya. Watanzania wanataka umoja wetu na hawataki utengano wetu. Eti tutaacha kumpokea Lowassa kiongozi ambae anaungwa mkono na wananchi wengi wa nchi hii, anayeungwa mkono na robo tatu ya wabunge wa ccm. Kama kuna mwanachadema ambae hajatuelewa namuombea kwa Mungu aendelee kumjaza busara. Chama csha siasa ni watu, sasa nimeletewa watu milioni nitawakataa. Siwezi, mtanifukuza uenyekiti na kwa utaratibu huo sitakubali kuondoka.

Kuna wasiwasi kwa watumishi wa umma, Vyombo vya usalama vilivyopo ndio hivyo hivyo vitaendelea, watumishi wa umma ndio haohao wataendelea. Wapo wengine wengi, tutawakaribisha muda ukifika.

Tumebadilisha gia angani ili dynamics ziweze kutekelezeka, CHADEMA kinaongozwa na katiba na hii simwambii Lowassa kwa sababu tayari anayo, nawaambia watanzania wanaotaka kujiunga nasi. Tukiikiua hii tutabamizana. Kwenye chama hiki hatuji kugawana vyeo, niwashukuru sana.

Mwapokee wageni, naombeni msiwaogope wageni kwa kuogopa kuchukuliwa nafasi zenu. Kuna watu tuliwatukana sana, nawaomba na nyie mkija huku muwarushie wa upande wa pili. Tuna imani sana nguvu mpya inayokuja itakua nguvu ya neema. Niwashukuru watanzania wote, tunachopambana nacho sio mtu, tunapambana na mfumo dola. Leo hata ukamchukua malaika ukamshusha CCM na kumuacha kwa mwezi mmoja, ukimchukua tayari atakuwa Ibilisi. Huu ni mpango wa Mungu. Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipotoa shukrani za dhani kwa mtu mmoja wa kipekee sana. Namshukuru sana sana mheshimiwa Kikwete, chama chetu kina idara ya uenezi, hakijafanya kazi nzuri kama aliyofanya Kikwete. Kwa hio mheshimiwa wakati unakatwa Dodoma, wewe unalalamika sisi tunasema yes, mambo haya.

Sio kila linalotokea nia baya, mengine ni mpango wa Mungu. Mungu aliona ili muishi kwa amani na familia yako lazima mtoke CCM ila lazima ujiandae na mazoezi kidogo maana huku kuna mabomu. Waandishi wa habari tunawashukuruni sana, tunaamini ule ushirikiano mliokuwa mnampa team Lowassa mtaweza kutupa.

Kufikia hapa tumefikia hitimisho, kutakuwa na wimbo wa taifa kuhitimisha. Na mheshimiwa Mbatia anaongoza wimbo wa taifa wa mama Tanzania.

Ndugu waandishi wa habari na ndugu Watanzania wenzangu.

Yamepita majuma mawili tangu mchakato wa kuchagua mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ukamilike. Nimetumia muda huu kutafakari kwa kina yaliyotokea Dodoma na hatima yangu katika siasa nchini. Ninajua marafiki wengi na wananchi wenzangu wanaoniunga mkono wamekuwa wakisubiri kwa hamu nitoe kauli.

Nilipokuwa natangaza nia ya kugombea urais kule Arusha, nilieleza nia yangu ya kuanza mchakamchaka wa maendeleo ya nchi yetu na kuondokana na umaskini. Pamoja na yaliyotokea Dodoma, azma hii bado iko palepale.

Lakini nianze kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema aliyetupa sisi pumzi ya kuendelea kuwa wazima wa afya njema hadi hivi sasa. Nawashukuru pia mke wangu Regina, wanangu, wanafamilia na marafiki wote kwa mapenzi, msaada na uvumilivu wao wakati wa kipindi hiki kigumu tunachopitia. Nawashukuru sana pia maelfu ya wanachama wa CCM walionidhamini na mamilioni zaidi walioniunga mkono.

Katika safari zangu za mikoani wakati wa kuomba udhamini, nilitiwa hamasa na umati mkubwa wa watu waliojitokeza kuniunga mkono.Aidha, ninawashukuru sana wana kamati wangu, makundi mbalimbali na mamilioni ya vijana wakiwamo; "For You Movement", "Friends of Lowassa" "Team Lowassa", Umoja wa Bodaboda na wengine wengi ambao walijitolea kwa hali na mali katika Safari yetu ya Matumaini.

Nitakuwa sijahitimisha orodha ya shukrani iwapo nitaacha kuwashukuru viongozi wa dini zote nchini ambao waliungana na waumini wao wengi katika maombi na kwa kuniunga mkono. Najua sote tumevunjika moyo kwa yaliyotokea Dodoma na mazingira yaliyopelekea matokeo yale.

Kama ilivyokwishaelezwa, mchakato wa kuteua wagombea uligubikwa na mizengwe, ukiukwaji wa maadili, uvunjaji wa Katiba na taratibu za uchaguzi za CCM.

Zaidi ya hayo uchaguzi ulisimamiwa kwa upendeleo dhahiri na chuki iliyokithiri dhidi yangu. Kikatiba, Kamati ya Maadili si chombo rasmi na haina madaraka ya kuchuja na kupendekeza majina miongoni mwa wale wanaoomba kugombea Urais kupitia CCM.

Kilichotokea Dodoma ni kupora madaraka ya Kamati Kuu na kukiuka katiba ya CCM. Aidha, Kamati Kuu na Halmashauri Kuu viliitishwa na kuburuzwa ili vitekeleze azma ya watu binafsi pasipo kujali demokrasia, katiba, kanuni na taratibu za uchaguzi ndani ya CCM. Niliwekewa mizengwe na kuzushiwa majungu na uongo mwingi, kuhakikisha kuwa jina langu halifikishwi mbele ya Kamati Kuu na Halmashauri Kuu kujadiliwa licha ya ukweli usiopingika kuwa nilikuwa mgombea anayeungwa mkono na wananchi na wanachama wengi wa CCM kuliko wenzangu wote. Kibaya zaidi ni kile kitendo cha kuwanyima wagombea wote 38 haki ya kujieleza mbele ya Kamati Kuu.

Ni dhahiri kwamba njama dhidi yangu ndani ya CCM si jambo jipya.Kumekuwa na mkakati wa siku nyingi wa kulichafua jina langu kwa uzushi na uongo usio na kifani. Aidha, mmeshuhudia jinsi vijana kadhaa walivyotumika kunikashifu na kunitukana na bila aibu na uongozi wa CCM na Serikali kuwazawadia madaraka makubwa.

Kwa namna ya kipekee napenda kuwapongeza na kuwashukuru wazee wetu akiwamo Mzee Kingunge Ngombale Mwiru na baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu ikiwa ni pamoja na waheshimiwa Emmanuel Nchimbi, Sophia Simba na Alhaj Adam Kimbisa kwa uadilifu na ushujaa wao mkubwa wa kuisimamia katiba ya CCM na misingi ya haki na kukataa maamuzi batili ya Kamati ya Maadili na Kamati Kuu kuhusu uteuzi wa wagombea.

Cha msingi kuzingatia ni kuwa ili kuhitimisha njama za kunipora mimi na wagombea wengine haki zetu za msingi za kusikilizwa, viongozi wachache walikuwa tayari kupanda mbegu ya chuki na mfarakano ambao ni mfano mbaya kwa CCM na hata Taifa letu. Watanzania walitarajia chama kinachoongoza nchi kiwe ni mfano wa utawala wa sheria na kinara katika kutetea misingi ya haki na demokrasia na siyo kuihujumu. Yaliyotokea Dodoma yameitia dosari nchi yetu.

Kwa kifupi, ninaamini sikutendewa haki katika mchakato mzima wa kupendekeza majina na kuteua mgombea wa urais kupitia CCM. Nilinyimwa haki yangu ya msingi ya kusikilizwa na kuchaguliwa.

Kwa mantiki hii nitakuwa mnafiki kama nitaendelea kujidanganya mimi mwenyewe na umma wa Watanzania kwa kusema kuwa bado nina imani na CCM au kuwa CCM ni chama kitakachowaletea ukombozi wa kweli wa kiuchumi, kisiasa na kijamii. CCM niliyoiona Dodoma siyo tena kile chama nilichokulia na kilichonipa malezi na maadili ya siasa yaliyojengwa kwenye misingi ya haki, usawa na uadilifu.

Ni dhahiri kwamba CCM imepotoka na kupoteza mwelekeo na sifa ya kuendelea kuiongoza Tanzania yetu. Mimi kama Mtanzania aliye na uchungu na nchi yake nasema imetosha na SASA BASI!

Kama Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyosema, CCM siyo baba yangu wala mama yangu na kwamba kama Watanzania hawapati mabadiliko ndani ya CCM watayatafuta nje ya CCM. Sasa tuyatafute mabadiliko nje ya CCM.

Hivyo basi, baada ya kutafakari kwa kina nimeamua kuwa kuanzia leo ninaondoka CCM na kuitikia wito wa Ukawa kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuungana nao katika kuleta mabadiliko ya kweli ya nchi yetu. Navishukuru vyama vyote vya siasa chini ya Ukawa, yaani Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kwa mwaliko wao na imani yao na kuthamini mchango ninaoweza kutoa kufanikisha azma ya kuleta mabadiliko na maendeleo ya kweli ya Taifa letu. Waheshimiwa Freeman Mbowe, Profesa Ibrahim Lipumba, Mheshimiwa James Mbatia na Emmanuel Makaidi asanteni sana.

Ndugu zangu, sikuufanya uamuzi huu kwa pupa, lakini unafika wakati wa kuchukua maamuzi hata kama ni magumu kwa kuamini fika kuwa ni kwa masilahi ya Taifa letu.

Nimejiridhisha kuwa ndani ya Ukawa Taifa letu linayo fursa ya pekee na ya kihistoria kushinda Uchaguzi Mkuu ujao na ya kuleta mabadiliko ya msingi katika nchi yetu. Kwa uamuzi na ushiriki wangu huu, ninaamini kwa dhati kuwa tutaondoa uhodhi wa madaraka wa chama kimoja na kujenga demokrasia yenye ushindani wa kweli kisiasa.

Namalizia kwa kutoa wito kwa Watanzania wenye nia njema na nchi yetu na wanaotaka kujenga demokrasia na kuleta mageuzi na maendeleo ya kweli, kujiunga nasi katika safari hii mpya ya kuinusuru nchi yetu.

Safari ya Matumaini inaendelea kupitia Ukawa lakini haitafanikiwa iwapo sote hatutajiandisha kupiga kura. Natoa wito kwa wakazi wa Dar es salaam, kutumia fursa iliyopo kujiandikisha kwa wingi.

Aidha, nawakumbusha Watanzania kote nchini waliojiandikisha kutunza shahada zao na kukumbushana kupiga kura ili ifikapo Oktoba mwaka huu tupate ushindi wa kishindo.

Ndugu zangu Watanzania, tuungane pamoja kuuondoa umaskini na kuleta mabadiliko ya kweli.

NARUDIA CCM SIYO MAMA YANGU
 

Attachments

Last edited by a moderator:

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
6,443
2,000
1. Mwalimu aliitazama zaidi Tanzania kuliko chama alichokiongoza yaani TANU na baadaye CCM. Na kuna wakati, kwa
maneno yake mwenyewe, Nyerere alitamka; “CCM si baba wala mama yangu.” Mwalimu alikuwa tayari kuikana
CCM, lakini si kuikana Tanzania. Alidhamiria kuwakomboa Watanzania kifikra ili waondokane na unyonge
na umaskini wao.
- Mwaka 1987 akihojiwa na waandishi wa habari. katika kuadhimisha miaka kumi ya kuzaliwa
kwa CCM na miaka 20 ya Azimio la Arusha.


2. "Nimeiasisi CCM, kadi yangu ni namba 7. Hata hivyo kufukuzwa uanachama sio tatizo kwa sababu CCM si mama
yangu wala sio baba yangu
. Sitobadilisha msimamo wangu wa kuitetea Zanzibar. Nimefanya hivyo tokea ASP na
CCM hazijaasisiwa. Muungano na Katiba ni masuala ya NCHI sio MALI YA CCM. CCM sijaikosoa hadharani bali
nimeieleza ukweli, UAMUZI WAO WA KUNIFUKUZA HAUNISHUGHULISHI" Alisema mzee Hassan Nassor Moyo. 2015

EL AMETHIBITISHA KWA MATENDO.
 

babumapunda

JF-Expert Member
Dec 21, 2012
4,581
2,000
Mda mfupi ujao mh.Lowassa atakaribishwa rasmi ndani ya chadema ni kisha kuwa mwana ukawa

Huu ni uzi maalum wa ukaribisho huo japokuwa Tanesco Wamekata umeme na nahisi ni maeneo mengi nchini yatakuwa hayana umeme kwa wale wenye kuweza kuwa karibu na redio ukaribisho huu utakuwepo ndani ya radio one sterio kwahiyo mnaweza fatilia huko


Sisiwengine ngoma itanoga humu humu jf

Huwezi zuia mafuriko kwa mkono hata kama ipo laki moja wao wametangulia na kufuli sisi tunakuja na funguo
 

Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,698
1,195
Habari wakuu,
Leo Jumanne, tarehe 28 Julai, 2015
, chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kitampokea rasmi Edward Lowassa kuwa mwanachama wake mpya kutoka chama tawala, tukio hili pia litahudhuria na viongozi wa vyama vinavyounda umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA). Tuwe sote kujuzana yanayojiri katika mapokezi haya.
==================
Tuko pamoja....
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,942
2,000
Sio nawe usikie raha na kusaha u kuripoti. Jua kuwa maeneo mengi nchini hakuna Umeme sasa hivi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom