Ninja
JF-Expert Member
- Feb 5, 2010
- 348
- 535
Niliwahi kukutana na jamaa mmoja mganda huko Kakurezato Japan, tukiwa pamoja mafunzoni na akanishangaza sana kuhusu yule aliyekuwa adui yetu watanzania miaka ya 70 nduli Idd Amin Dada.
Alisema kuwa Idd Amin pamoja na picha ya ubaya iliyokuwa ikionekana huku Tanzania kuhusu udikteta na unyanyasaji wa raia wa Uganda aliokuwa akiufanya bado alikuwa na mashabiki wengi sana Uganda ambao walimhesabu kama shujaa wao. Kilichonimaliza ni alipotamka maneno haya, naomba kuyanukuu;
"Idd Amin alikuwa na nia njema sana kwa nchi yetu Uganda na kwa Afrika nzima, alikuwa ni mzalendo wa kweli toka moyoni, aliuchukia sana ukoloni na wakoloni wa aina zote, na aliamua kuwanyanganya wageni mali zao ili kuwarudishia waganda, na hadi alifukuza jamii ya waasia na kuwarudisha kwao; kila aliyekua mpinzani wa mikakati madhubuti ya kizalendo ya rais mpendwa wa wakati huo Idd Amin basi mpinzani huyo aling'olewa duniani. Waganda wengi mwanzoni mwa miaka ya 70 waliamini Idd Amin angeifanya Uganda iwe sawa na Ulaya kiuchumi hadi kufikia mwaka 1980."
My take
Duh!