Tuko
JF-Expert Member
- Jul 29, 2010
- 11,180
- 7,354
Kwa wale ambao walishasafiri kwenda nchi ambazo unahitaji visa wanafahamu kuwa balozi zinazotoa visa hizo zinafahamu vyema sheria ya nchi zao juu ya visa.
Kwa Tanzania hali ni tofauti sana kwani balozi nyingi huko ughaibuni ama hazijua taratibu, au zimepewa taratibu feki kwa maslahi fulani.
Mara kadhaa maofisa wa uhamiaji hasa hapa Morogoro wamekuwa wakiwakamata wageni mbalimbali wanaokuwepo nchini kwa maelezo kuwa hawana ruhusa ya kufanya yale wanayoyafanya. Imefahamika kuwa pale wageni wanapoomba visa katika balozi za Tanzania huko kwao, kwa ajili ya shughuli kama kushiriki mafunzo au makongamano, balozi hizo huwapa tourist visa na kuambia kuwa hawahitaji business visa. Mbaya zaidi ni kuwa baadhi ya wageni hao wamekuwa wakijaza fomu zinazohitaji kupata business visa lakini balozi 'kwa nia njema' zimekuwa zikiwakatalia na kuwapa tu tourist visa.
Maofisa wa uhamiaji, (hasa hapa Morogoro), kwa kujua udhaifu huo wa kimawasiliano wamekuwa waki-sneak sehemu tofauti hapa mjini na wanapobaini kuwa kuna mgeni kafikia sehemu, wanamfuatilia kujua kama anafanya tu utalii au kuna kitu kingine na ikibainika anafanya zaidi ya utalii, humkamata na kumpiga fine ya hadi dola 400 (badala ya 100 ambazo angelipa kama angepewa visa sahihi). Mbaya zaidi ni kuwa maofisa hawa hupenda malipo hayo yafanyike 'nje ya ofisi'. Kwa kweli hali hii naamini inabugudhi na pia inaidhalilisha nchi machoni pa wageni.