Idara ya Uhamiaji inaidharirisha Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idara ya Uhamiaji inaidharirisha Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tuko, Aug 11, 2010.

 1. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #1
  Aug 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Kwa wale ambao walishasafiri kwenda nchi ambazo unahitaji visa wanafahamu kuwa balozi zinazotoa visa hizo zinafahamu vyema sheria ya nchi zao juu ya visa.

  Kwa Tanzania hali ni tofauti sana kwani balozi nyingi huko ughaibuni ama hazijua taratibu, au zimepewa taratibu feki kwa maslahi fulani.

  Mara kadhaa maofisa wa uhamiaji hasa hapa Morogoro wamekuwa wakiwakamata wageni mbalimbali wanaokuwepo nchini kwa maelezo kuwa hawana ruhusa ya kufanya yale wanayoyafanya. Imefahamika kuwa pale wageni wanapoomba visa katika balozi za Tanzania huko kwao, kwa ajili ya shughuli kama kushiriki mafunzo au makongamano, balozi hizo huwapa tourist visa na kuambia kuwa hawahitaji business visa. Mbaya zaidi ni kuwa baadhi ya wageni hao wamekuwa wakijaza fomu zinazohitaji kupata business visa lakini balozi 'kwa nia njema' zimekuwa zikiwakatalia na kuwapa tu tourist visa.

  Maofisa wa uhamiaji, (hasa hapa Morogoro), kwa kujua udhaifu huo wa kimawasiliano wamekuwa waki-sneak sehemu tofauti hapa mjini na wanapobaini kuwa kuna mgeni kafikia sehemu, wanamfuatilia kujua kama anafanya tu utalii au kuna kitu kingine na ikibainika anafanya zaidi ya utalii, humkamata na kumpiga fine ya hadi dola 400 (badala ya 100 ambazo angelipa kama angepewa visa sahihi). Mbaya zaidi ni kuwa maofisa hawa hupenda malipo hayo yafanyike 'nje ya ofisi'. Kwa kweli hali hii naamini inabugudhi na pia inaidhalilisha nchi machoni pa wageni.
   
 2. The Quonquerer

  The Quonquerer JF-Expert Member

  #2
  Aug 11, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 781
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona wafanyakazi haramu wa Kikenya wameshindwa kuwakamata. Hao wa kuja na kuondoka wawaache, kuna wengine ni rubi, wang'ang'ania hapa hapa, kwao whawataki kurudi, hao nndio wa kuwashukia na kuwavurumisha!
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Aug 11, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  Nadhani ni wizara nzima ya mambo ya ndani iko hovyo, lakini hii ya uhamiaji inatia kichefuchefu, kwa nchi kama south africa ni ngumu sana kupata Permit ya kufanya kazi na wanapita kwenye industries zote kukagua wageni na permit zao, lakini kwa Tanzania ni ajabu sana, wageni wamekuwa wengi na wanafanya kazi ambazo watanzania wanaweza kabisa kuzifanya na wataalam wapo tele, ukifika migodini ndio utashangaa, Mzungu anatoka Australia kuja Tanzania kuoperate Dozer ama Grader
   
 4. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #4
  Aug 11, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  jamani kila idara ndani ya nchi hii 'imeoza'
  mabadiliko ya kina yanahitajika.
   
 5. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #5
  Aug 11, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Hapa ndiyo utashangaa, ukifika Immigration HQ DAR utakuta afisa wa uhamiaji ambaye mshahara wake ni TGSD C or D ambao hauzidi tsh 450,000 gross.
  Anaendesha gari yenye thamani ya zaidi ya tsh 12ml
  anatumia simu mbili both blackberry original worthy tsh 850,000 na hana biashara nyingine zaidi ajira
   
 6. K

  Kalyosi Member

  #6
  Aug 16, 2012
  Joined: Apr 7, 2012
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Fanyeni uchunguzi wa kina kwa hayo mnayoyasema, kwa mfano kuhusu kumiliki gari na cmu, je, unafahamu vyanzo vyote vya mapato vya huyo mtu?

  Msiwaonee uhamiaji jamani haya mapungufu yapo kila idara hapo tz, hata ikulu wapo watu wa aina hiyo.
   
Loading...