Idara ya Uhamiaji imulikeni Ofisi ya TRA Morogoro Mjini, kuna watu uraia wao ni wakutilia mashaka

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,628
9,175
Mimi ni Raia mwema nina nia njema wala sina kinyongo na mtu yeyote, kwa sasa naishi Mtwara lakini nimewahi kufika hapo Ofisi za TRA Morogoro mjini.

Kuna watumishi baadhi yao hapo ofisini ukiwaangalia tu lazima upate wasi wasi na uraia wao, kwa wale ambao mmewahi kuingia hapo nadhani mnaweza kuelezea zaidi.

Mimi ni raia mwema natoa tu taarifa, kama nitakuwa nimevunja sheria yeyote Mods fanyeni uhalili au chukueni umiliki wa hii post.

Nawasilisha.
 
Acha majungu wewe ni mmoja wa wafanyakazi hapo kuna watu unawachimba kabisa hapa labda kweli ama chuki Binafsi. Kuangalia pua ili kutathmini uraia ni kuishiwa.
 
Mkuu, usiwe na shaka.. Kwa sasa nchi ina makabila mengi yaliyoongezeka kutokana na kupewa uraia kwa Wahutu na Watutsi ambao walihamia nchini.. Pia kuna Wahindi na Waarabu.. So jumla nchi ina makabila kama 127 hivi.
 
Acha Majungu wewe ni mmoja wa wafanyakazi hapo kuna watu unawachimba kabisa hapa labda kweli ama chuki Binafsi. Kuangalia pua ili kutathmini uraia ni kuishiwa
Mshenga hauwawi!
 
Mtoa taarifa yuko sahihi hongera kwa kuwa mzalendo kwa Nchi yako, Vyombo vinavyohusika vikahakiki uraiya wa hao wafanyakazi, na office zingine pia.
Watahakiki nini wakati watumishi ndio tulikuwa wakwanza kupewa vitambulisho vya NIDA. Hao wana kila document inayotakiwa
 
Watahakiki nini wakati watumishi ndio tulikuwa wakwanza kupewa vitambulisho vya NIDA.
Hao wana kila document inayotakiwa
Uhakiki hauwezi kwisha, kwani inawezekana walivipata kwa makosa, kwa hio uhakiki ni lazima hata kama una document zote.
 
Back
Top Bottom