Idara ya Afya Wilaya ya Sengerema imeshindwa kuweka watumishi zaidi ya 50 kwenye orodha ya kupanda madaraja

jhohoho

Senior Member
Nov 8, 2016
154
142
Kiukweli ni hali ya kusikitisha sana idara ya afya kushindwa kuwaweka kwenye orodha ya watumishi wanaopaswa kupanda daraja zaid ya watu 50.

Dhahama hii imewakumbuka baadhi watumishi wengi walioajiriwa kuanzia miaka ya 2015 na kurudi nyuma.

Katika kufuatilia kwangu nimeona watumishi hawa sifa wanazo isipokuwa ni mizengwe tu ya baadhi ya watendaji katika idara hii juu ya watumishi hawa.

Tukumbuke watumishi hawa wamefanya kazi usiku na mchana katika kutibu wagonjwa kwa zaid ya miaka 7 na kuendelea.

Leo inapokuja suala la kupata motisha kidogo na mtendaji mmoja au wawili kwa sababu tu wanazozijua wao kuamua kuwanyima haki zao si suala sahihi na halikubaliki.

Niombe mamlaka zote zinazohuska ziliangalie hili suala kwa kina kwani huku kwenye halmashauri kuna watendaji au watumishi wanaojiona wao ni miungu watu kutaka kuendelea kumunyima mtumishi wa kawaida haki zake za msingi.

NB: Najua uandishi wangu katika hii mada yaweza kuwa usiwe mzuri Sana lakin kikubwa ujumbe umefika kwa walengwa

*Naomba kuwasilisha
 
Back
Top Bottom