Idadi ya wapiga kura Tujulishwe Watanzania Mapema!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Idadi ya wapiga kura Tujulishwe Watanzania Mapema!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by RedDevil, Aug 6, 2010.

 1. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #1
  Aug 6, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  WanaJF, nimeamua kuanzisha hii thread kwa lengo la kupata takwimu kamili ya idadi ya wapiga kura waliojiandikisha kwa kila mkoa na wilaya zake na kwa kila wilaya na tarafa zake na kwa kila tarafa na kata zake nk. Naimani siyo siri kutupa hata nyaraka zake ili ijulikane mapema nani anatakiwa apige kura hapa na si kule.

  Tunataka mwaka huu demokrasia ya kweli, walimu wanaosimamia hivyo vituo nawatu wengine, natoa wito tuache sasa tamaa za kifisadi tukomae, kwani hata ukifa kwa kulinda haki tutakukumbuka daima.

  Hii itasaidia kujua wapi kuna idadi hii na kule idadi hii. Itasaidia kuwafunga watu baadae, na hata kutoa ushahidi pindi mambo yatakapokuwa yamekwenda sivyo, pili tutakuwa tunafanya mambo kiuwazi zaidi. Naomba kama kuna mwanaJF au wanaJF wanatakwimu watuwekee hapa ili tujue wapi kuna population ya kutosha na kuanza mikakati ya kutosha kulikomboa taifa letu.

  Dr Slaa, twende kazi mkuu hakuna kulala.

  Naomba kuwasilisha hoja.
   
 2. payuka

  payuka JF-Expert Member

  #2
  Aug 6, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 832
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mzee kwanza bigup sana kwa kuleta mada hii.....ni jambo ambalo nimekuwa nikifikiria kwa muda mrefu sasa ...hii serikali ya ccm ina mambo ya ajabu sana na inatupia loop holes nyingi kucheza rafu kipindi cha uchaguzi. Sasa basi ninaomba nipewe nafasi ya Ku-ilink hii topic na Changa la macho La "National Identity Cards".
  Mi nahisi ( Sina Uhakika) hata hizi delays za Ku-issue National IDs zinatokana na politics ikiwamo suala la uchaguzi.......sababu Info zote Za Kuhusu Idadi kamili ya watu ....umri wao na sehemu wanazoishi ( Biometric information) can be easily retrieved! endapo kunatokea utata baada ya Uchaguzi. Hili CCM walishaliona siku nyingi ...sababu wanajua ambacho huwa wanakifanya kwenye kura wakati wa uchaguzi
   
 3. RedDevil

  RedDevil JF-Expert Member

  #3
  Aug 6, 2010
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 2,287
  Likes Received: 903
  Trophy Points: 280
  Mzee Payuka pamoja kaka!

  NEC wamekula kodi yangu siku nyingi kwa kuliboresha daftari mkoa hadi mkoa lakini mimi mlipa kodi sijajua idadi kamili ya wapiga kura hadi leo, sioni shida hata wakinipatia wapiga kura mtaa kwa mtaa nitafurahi/watanzania wote tutajua sasa wapi na nani anatudanganya/kutuibia na nitapenda zaidi kulipa kodi kwani najua sasa hawa NEC wanafanya kazi nzuri nasiyo mazingaombwe.

  Hata wapiga kura watakuwa na hamasa zaidi ya kupiga kura kuliko kusubiri hadi siku mbili kabla then tuanze kuambiwa jina lako halipo.

  wanaJF hatua ni sasa, tutanataka takwimu za wapiga kura kila sehemu hata kama itachukua mwezi lakini zijulikane mapema.

  Mwaka huu hakuna kuibiana wala ujanja ujanja hatukubali.
   
Loading...