ICTR yaanza mchakato wa kufunga shughuli zake

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
ICTR yaanza mchakato wa kufunga shughuli zake
Send to a friend
Friday, 07 October 2011 19:40


Peter Saramba, Arusha
MAHAKAMA ya Kimataifa ya Mauaji ya Rwanda(ICTR), imeanza mchakato wa kufunga shughuli zake hapa nchini kwa kuwaanda wafanyakazi wake kisaikolijia ili waweze kukabliana na changamoto za maisha mapya baada
ya hatua hiyo.

Maandalizi hayo yanahusisha kuwatafutia kazi katika sehemu nyingine na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa watakaojiingiza katika shughuli za kibiashara.

Mkuu wa Utawala wa ICTR, Sarah Kilemi, aliwaambia waandishi wa habari mjini Arusha jana kuwa hadi kufikia Desemba mwaka huu, idadi kubwa ya wafanyakazi watakuwa wamepunguzwa.

Kwa mujibu wa Kilemi, itakapofika Julai mwakani, shughuli nyingi za mahakama hiyo zitawekwa chini cha usimamizi wa chombo maalumu kitakachopokea kazi za
ICTR na ile ya mauaji ya halaiki ya Yugoslavia (ICTY).

Alisema katika kipindi hicho, wafanyakazi wanaohusika na kesi mbili zinazoedndelea kushughulikiwa na mahakama hiyo, watabakia kwa ajili ya kumalizia shughuli hizo kabla ya kufungwa kwa mahakama zote mbili mwaka 2014.

Alisema wafanyakazi hao ni pamoja na wakalimani, makarani, walinzi, majaji na wa kada nyingine.

“Kuanzia Novemba mwaka huu, tutaanza kutoa barua za notisi ya mwezi mmoja kwa watumishi watakaopunguzwa kazi. Hata hivyo tayari baadhi ya wafanyakazi wameondoka kwa hiari yao baada ya kupata ajira sehemu zingine zenye mikataba ya muda mrefu ikilinganishwa na ile ya ICTR ambayo ni miezi sita, mwaka mmoja au zaidi kulingana na mahitaji yaliyopo,” alisema Kilemi.

Alisema chombo kipya kitachoundwa kurithi kazi za mahakama,kitashughulikia utekelezaji wa maamuzi, hukumu mbalimbali na utunzaji wa kumbukumbu (maktaba) za kesi zilizoendeshwa na mahakama.

“Wale wenye nia ya kujiingiza kwenye biashara tunawapa elimu ya ujasiriamali ili waweze kuanzisha na kumudu kuendesha biashara zao.Lengo ni kuwawezesha kumudu maisha baada ya kutoka ICTR,” alisema Kilemi.

Kuhusu athari za kiuchumi baada ya ICTR kufunga shughuli zake, Kilemi alisema athari hizo zinaweza kufidiwa na kuwapo kwa ofisi na taasisi zingine za kimataifa zinazoendesha shughuli zake mjini Arusha.

Hata hivyo alikiri kuwa baadhi ya watu waliokuwa wakipata faida ya moja kwa moja au kupitia kwa wafanyakazi wa mahakama hiyo watayumba kiuchumi.


 
waliokuwa wanaishi kwa kutegemea ajira za ICTR...........................wana wakati mgumu wa kuanza kutafuta ajira mpya ambazo hazipo...............wapo watakaokumbuka ajira zao za zamani walizoziacha kwa kutafuta ugali mkubwa............
 
Back
Top Bottom