Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,760
- 730,008
Kuna hili la kuchoma pesa kwenye imani za kibudha japo pia inaambatana na tamaduni za Kichina
Zaidi ya kuchoma pesa pia kuna kulisha mizimu (hungry ghost)
Hizi ni ibada mbili tofauti, za kuchoma moto hufanywa mara nne kwa mwaka mbili ndogo na mbili kubwa, hapa lengo ni kuongeza ngekewa bahati kismati na utajiri kwenye biashara
Hii ya pili ni ya kulisha mizimu, wakiamini kiimani kwamba mizimu hiyo ni viumbe vilivyo jaa mateso na haviwezi kula chochote kwakuwa kikipita tu kooni kinaunguzwa na moto mkali
Unaweza kuwaona wendawazimu kwa haya wanayofanya lakini ni imani na inawasaidia....wao pia wanawashangaa wale wnaomuabudu Mungu mkuu
Imagine mtu anateketeza milioni cssh motoni