Ianzishwe Chemba ya pili ya Bunge(Senate) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ianzishwe Chemba ya pili ya Bunge(Senate)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by fmesanga, Jul 30, 2009.

 1. f

  fmesanga Member

  #1
  Jul 30, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 14
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Demokrasia na uwajibikaji vinaongezeka panapokuwa na udhibiti mzuri wa utungaji sheria na maamuzi. Utungaji sheria hufanywa na Bunge. Kuna uwezekano mkubwa kabisa kwamba bunge linaweza kutunga sheria zinazotokana na jazba au kukokomoa. Hivyo zitakuwa kandamizi au sisizo na tija kwa jamii. Ndiyo maana nchi nyingi zina zina chemba mbili za bunge, kwa mfano: Marekani ina Congress na Senate, Japan ina chemba mbili, Uingereza (Commons na Lords), hata Zimbabwe ina chemba mbili.

  Kifupi utendaji kazi wa chemba hizi ni kwamba ile ya chini (parliament au congress) ndiyo yenye wabunge au wawakilishi wengi na ile ya juu (senate) inakuwa na wawakilishi wachache. Mswaada wa sheria hupelekwa bungeni au chemba ya chini, hujadiliwa na hupitishwa uwe sheria. Lakini kabla Rais au Mfalme au Mkuu wa nchi hajatia saini yake ili huo mswaada uliopitishwa uwe sheria unapelekwa katika chemba ya juu (Senate) ambapo hujadiliwa na ikibidi kufanyiwa mabadiliko kabla ya kupelekwa kwa Mkuu wa nchi kutia saini uwe sheria kamili.
  Huwa wakati mwingine wawakilishi wa chemba ya chini hukataa mabadiliko yanayotakiwa na chemba ya juu. Ikitokea hivyo hubidi chemba zote mbili zikutane na kufanya mabadiliko ya pamoja. Hii haitokei mara nyingi.

  Kwa hiyo utaona hapa chemba hizo mbili huafikiana sheria ambazo ni nzuri (reasonable) tofauti inapokuwa chemba moja tu kama ilivyo hapa Tanzania. Zipo sheria nyingi (zaidi ya 40) kandamizi zilizopendekezwa ziondolewe lakini bado zipo tu.

  Sherai nzuri hurahisisha uwajibikaji na utoaji haki kwa raia. Napendekeza hii chemba ya pili (Senate) ianzishwe mara moja kwa mategemoe kwamba itasaidia kuimarisha demokrasia nchini. Napendekeza pia wale watakaochaguliwa kwenye chemba hii (maseneta) wawe watu wenye umri usiopungua miaka 40 na wenye elimu nzuri na uzoefu wa kutosha katika eneo lolote. Ili kuwa na uwakilishi mzuri katika senate itabidi kila mkoa uwe na maseneta wawili. Majiji kila moja uwe na seneta mmoja mmoja. Hii itafanya idadi ya maseneta isiyozidi sitini, 60. Hapa tusiwe na maseneta wa kuteuliwa, wote wachaguliwe na wanachi, uswahiba usije ukaharibu mantiki nzima ya chemba ya pili.
   
 2. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #2
  Jul 30, 2009
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Hiyo chemba ya pili ita tawaliwa na CCM tu kwa hiyo hiyo checks and balance itakua theory tu while in practicaly utakua ume kipa chama tawala viti zaidi katika uongozi. Chemba mbili za bunge hazita badalisha chochote mpaka pale ambapo angalau chama kingine kita kuwa na uwezo wa kupata majority kwenye chemba moja.
   
 3. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #3
  Jul 30, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mosi, Kwa Tanzania, itakuwa upotezaji wa pesa ya mlipakodi. Kwanza tunahitaji mapinduzi ya kifikra na kisiasa kisha ndo tukimbilie kutengeneza hayo 'machemba'. Pili, Chemba moja tuliyonayo haina jipya zaidi ya kuwa 'muhuri' wa kuwatumikia zaidi watawala zaidi ya 'watwana.
   
Loading...