Iam positive

Iam positive

I am sorry

Member
Joined
Feb 7, 2015
Posts
16
Reaction score
8
Habari.

Ukweli nilisikitika sana nilipopata majibu kuwa nimuathirika wa HIV niliamini sina jipya tena, but with hope waliniambia HIV haizuii kufikia ndoto zangu na hata kuweza kuoa na kusonga mbele na maisha ya kawaida.

Ukweli ni story ndefu mpaka kufikia hapa lakini naamini humu Jamii forums wapo ambao ni affected kama mimi but I should be the first to start.

Kwa sasa nina miaka 30 really looking for fellow positive girl to marry. Please if u think your positive and your a girl Just send me a PM (private message) thats we can contact.

Be blessed and stay safe.
 
hongera sana kwa kugundua kwamba life lazima iendelee na pia ukimwi kwa sasa sio kama zamani, bado kansa, diabetes na non communicable disease zinatisha zaidi

cha maana tu ni adherence ya nasaha za wataalam
 
kila la kheeri mkuu ni vyema hujavunjika moyo wala kukata tamaa
 
Pole kwa yaliyokukuta na Hongera kwa ujasiri
 
hongera sana kwa kugundua kwamba life lazima iendelee na pia ukimwi kwa sasa sio kama zamani, bado kansa, diabetes na non communicable disease zinatisha zaidi

cha maana tu ni adherence ya nasaha za wataalam

asante kwa ushauri wako
 
Bila shaka utampata umtafutaye...

Kutambua afya ni jambo muhimu sana...
 
aliye negative akikuridhia hutaki? hongera kwa kuwa positive na maisha ila ningekuwa positive na ninataka mume nisingeku-pm ng'o!! Historia ya MMU inaonyesha baadhi ya watu wanapiemiana, wakikutana nje ya pm wakashindwa kuelewana mambo yanakuja kuwekwa hadharani na mmoja wao. Ungeandaa mkataba wa usiri kabisaaa. Kwani huko clinics huwa hamkutani?
 
ImageUploadedByJamiiForums1423340151.965878.jpg
 
You think so? Hata ikinitokea muitikio wangu unaweza usiwe kama wako. Sijiskii pia kukuonea huruma maana huhitaji huruma - itakuharibu. Unahitaji kueleweka tu. Mi nilitaka tu uwe makini zaidi ila we umenichukulia kivingine. Nawajua watu walioamua kuwa pamoja: mmoja mwathrika

mwingine mzima na wana watoto na walijua hali zao kabla hawajaamua kuoana na yule mzima bado ni mzima. Kwamba wanafanyaje mi sijui ila ukitaka kujua utajua. Ishi maisha yako kama kawaida na wakati mwingine usubiri kupokea kile wakati unachokuletea. Ukigandisha macho yako kwa waathirika wenzio tuu utakosa fursa zingine za maana maana sasa unataka kufungua mlango wa kujitesa kwa upweke.
 
You think so? Hata ikinitokea muitikio wangu unaweza usiwe kama wako. Sijiskii pia kukuonea huruma maana huhitaji huruma - itakuharibu. Unahitaji kueleweka tu. Mi nilitaka tu uwe makini zaidi ila we umenichukulia kivingine. Nawajua watu walioamua kuwa pamoja: mmoja mwathrika, mwingine mzima na wana watoto na walijua hali zao kabla hawajaamua kuoana na yule mzima bado ni mzima. Kwamba wanafanyaje mi sijui ila ukitaka kujua utajua. Ishi maisha yako kama kawaida na wakati mwingine usubiri kupokea kile wakati unachokuletea. Ukigandisha macho yako kwa waathirika wenzio tuu utakosa fursa zingine za maana maana sasa unataka kufungua mlango wa kujitesa kwa upweke.

Nimekuelewa asante kwa ushauri wako
 
Usimdhihaki aliyeathirika maana kutoathirika si ujanja bali wote bado tunavuka mto. Kama hujaathirika leo waweza kuathirika kesho.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom