i Yoh! Siyelele Mama! ( u helele!) Wimbo Tanzania inaouhitaji kwa sasa!

Paul Alex

JF-Expert Member
Jul 14, 2012
4,342
9,824
Wengi, weusi kwa weupe walipigana dhidi ya ubaguzi wa rangi Afrika kusini! Kama leo tunavyopaswa watanzania kupigana dhidi ya dharau na dhihaka za kiongozi wetu kwetu!

Moja kati ya nyimbo za ukombozi, nyimbo ambayo natamaani Tanzania iiimbe leo ni ' Siyalele Mama'
Angalia inavyokwenda nyimbo hii!
Japo sitaifikisha mwisho lakini si vibaya tukijikumbusha kidogo.
ANGALIZO - tafsiri ya kiswahili imetoholewa kulingana na mazingira ya Tanzania yetu leo.

i You! Siyelele Mama! (u helele!)
Oh Mother, we are under attack! (u helele!)
Oh mama, tumevamiwa (u helele!)

Siyalila Sichaba, dikgomo difedile - (u helele!)
The nation is crying, our cattle are gone (u helele!)
Taifa linalia, tumekumbwa na njaa (u helele!)

Bafedile li bopapa, batsware tsi dipasa - u helele!
And the men are gone, they were caught without passes /dompas
Na watetezi wetu kama Lema wanaumizwa jela, kwasababu za kijinga - u helele!

Tlang li boneng matata a - Afrika - u helele!
Come and see the troubles of Afrika ( u helele!)
Njoo uone matatizo ya Tanzania - u helele!

Mus' ukukhulum ' amanganyana!
Don't lie to us!
Magufuli acha kutudanganya!

Sesizwid ukuthi usebenzel '
We heard that you are helping the enemy - u helele!
Tumesikia kama unamsaidia adui - u helele!

Idlozi livukile! Masibuyel emakhaya! - u helele!
The spirits of our ancestors have awakened!
Mizimu ya wazee wetu imefufuka, hatumtaki Magufuli!

U - helele!

Sio mwisho, hivyo endelea kuiimbia Tanzania.

Aluta continua
Victoria ascerta.
 
Tatizo lipo tena kubwa ila wakubwa wanachekelea maana mnalazimishwa kulipa kodi ambazo wao ndio wanazotumia kula mkate. .
 
Sawa nitachangia

Kwa sisi wakulima unaona tunazika mbegu haimkini inaoza na kuchipua hadi kuzaa hata mara kumi mia nk.

Hapo siri ipo kwenye kuoza kwa nini zioze ndipo zichipue?

Kisayansi unaweza kutafisiri kuwa kuoza kunasababisha uhai kuchipua na miche kujishibisha na uozo.

Pengine chukulia uzazi inasermekana mfupa ya kichanga ni laini inapopita kwenye nyonga za uzazi na mara baada ya kupita na kuzaliwa kiumbe? mifupa yake hukomaa na kuchukua majukumu yake.

Vivyo hivyo kwa serikali zetu hususan Tanzania na chama dola tumejaliwa uvumilivu na Mungu ametuchagulia njia ya mkondo wa maisha ya kuibuka na elimu kwa vitendo na ushuhuda, yaani uozo wa utawala ni chanzo cha miche kuchipua.

Mambo yamejikoroga kiasi yanaoza. Sasa mtanzania haambiwi ona maana amejionea. Mungu naye hajalala anatoa kibano watawala lugha gongana kero tupu. Tunashuhudia elimu ya bure ya matokeo ya kupigia kura ahadi zisizotekelezeka na mabao ya mkono.

Watawala wamepigwa upofu hawajitambui kuwa wamejiweka utupu hadharani.

Ndiko kuoza kwenyewe na inachipuka miche kutokana na uozo huo. Kama ilivyokuwa MANAZI Ujerumani Umoja wa Urusi Makaburu kusini na Makaburu wetu wamesaidia sana miche ichipue. Kwa bahati hapa kwetu wamekufa akina Alphonse Mawazo na akina Lema wako mahabusu kutubebea mateso yetu.

Huo wimbo au shairi limetulia na limemaliza kila kitu.

Ongezea na

Freedom is coming tomorrow yaani
Kumepambazuka kwa kushuhudia ukombozi
 
Asante sana kiongozi, mchango mzuri!
 
Back
Top Bottom