I Miss: Alikiba anavyomsaidia Marioo Kulamba matapishi yake

Brother Wako

Member
Mar 18, 2017
21
19
“The Kid You Know” albamu ipo masikioni mwa mashabiki wa Marioo tangu December 9. Albamu hii yenye nyimbo 17 imepambwa na kolabo 12 za Afrika, miongoni mwa kolabo kubwa zinazopatikana humu ni I Miss.

I Miss ni wimbo namba 10 alioshirikishwa King Kiba, Alikiba na Marioo wameutendea haki mdundo wa Abbah kwenye hii love song.

Ni Stori ya mtu anaekumbuka penzi lake la zamani. Wimbo unatupa hadithi ya mtu anayeteseka kumuona Ex wake akifurahia maisha.

Stori inatuonyesha namna gani mwamba anatamani kumrudisha mrembokwenye himaya yake, lakini inaonekana tayari mrembo alisha'move on. Mwamba anajuta kupoteza mtu wa thamani kwenye maisha yake.

Wimbo huu unaweza kuwa miongoni mwa nyimbo zinazopendwa na watu wanaotamani kurudi kwenye mahusiano yao yaliyovunjika.

Ikumbukwe Marioo amewahi kutamba na Dear Ex, wimbo meutumia kumkataa vibaya Ex wake. Kwenye Dear Ex Marioo alionyesha msimamo wake wa kutolamba mapishi (kurudi kwenye penzi lililokufa). Stori imebadilika kwenye I Miss ambapo tunamuona mwamba anataka kupasha makabichi.

Ingekuwa ni maisha ya kawaida, tungesema Marioo, amelamba matapishi yake kwa kutamani kurudi kwa mwanamke aliyewahi kumkejeli kupitia Dear Ex.

Inafurahisha kuona kanuni ya muziki inavyofurahisha, muimbaji anaweza kukisifia na kukikosoa kitu kimoja katika nyimbo mbili tofauti.

Dear Ex na I Miss zina uhalisia kwenye maisha yetu ya mapenzi. Tukiachana na watu na tukawaona hatuwahitaji, tunakuwa Marioo wa Dear Ex, lakini dunia ikitufundisha kuwa tulioachana walikuwa wa thamani tunageuka kuwa Marioo wa kwenye I Miss.
 
Mapenzi hatari sana yaani King kiba anamlilia mke wake kwenye nyimbo zote alizotoa baada ya kuachana na amina kama mpaka King analia hakuna aliyesalama maana yule ni mr don't care kama mpaka yeye analia basi mapenzi ni nyoko kwenye I miss you kuanzia kipande cha marioo mpaka anakuja kuimba yeye bado analia na kujuta kuachana na amina mapenzi shikamoo
 
Dear x na i miss ni mademu tofauti usichanganye
 
Mapenzi hatari sana yaani King kiba anamlilia mke wake kwenye nyimbo zote alizotoa baada ya kuachana na amina kama mpaka King analia hakuna aliyesalama maana yule ni mr don't care kama mpaka yeye analia basi mapenzi ni nyoko kwenye I miss you kuanzia kipande cha marioo mpaka anakuja kuimba yeye bado analia na kujuta kuachana na amina mapenzi shikamoo
Duh yaani huyo kiba ndio umeona ndio kipimo sahihi cha wanaume wote? Halafu ulivyo kuku bila aibu eti unadai kama kiba kalia basi hakuna aliyesalama......hizi shule za kata ningeweza ningezibomoa kwakuwa athari yake ni kubwa mno
 
Ali kiba ameuiba wimbo kama wake vile 😂😂 sema album ni yamoto Sana 👊👊👊👊👊
 
Back
Top Bottom