Naona ndoto yako haina kipingamizi, chamsingi ni kwamba support yetu italeta ushindi wenye Manufaa kwa Taifa letu kwa ujumla. Jambo lingine ni kwamba ili kumuongezea nguvu Dr Slaa kwa kuenzi kazi anayoifanya kwa maslahi ya watanzania, tuiulize serikali iliyopo madarakani na inayoongozwa na CCM swali hili kwenye kilele cha kuadhimisha miaka 50 ya uhuru. "je, kwa nini serikali imefanikiwa, imeweza, imethubutu na inasonga mbele kwa kuiba Rasilimali za Watanzania? Je, ufisadi unaokithiri Tanzania ni moja ya mafanikio ya uhuru? kama siyo kwa nini wahusika hawawajibishwi? Je katika awamu hii ya nne kwa nini kauli mbiu yake imewanyonya watanzania kwa Maisha Magumu kwa kila Mtanzania asiyo na nafasi ya kuiba serikalini? Je, Ari zaidi ya Ufisadi, Nguvu zaidi ya Jeshi la Polisi na Kasi zaidi ya Kuiba rasilimali za watanzania inayoendeshwa na viongozi wa juu wa serikal itakwisha lini? kama maswali haya yatakosa majibu sawia basi 2015 CCM basi na karibu Dr Slaa Ikulu utukomboe sisi wanyonge wa Tanzania.