I hate my wife

I hate my wife

PIMs

Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
59
Reaction score
49
Imenitokea ghafla sana kila nikikumbuka matendo yake mabaya kwangu nashindwa kumsamehe na ninamchukia kupita maelezo. Kifupi hata nikimuona hasira inanipanda na hata mawasiliano naye sitaki.

Hua napenda kua mbali na watu na kukaa alone tu. Nimebadilika sana mpaka marafiki wananishangaa kua nimepoa mno na sionekani. Ila ukweli ni kua nimeumizwa moyo mpaka basi. Sitaki kujua habari zake na sitaki ajue zangu. Mpaka sasa hua nasafiri safari nyingi but hawezi jua nipo wapi na nafanya nini.

Nimekua na relationships na wasichana wengi mpaka kichwa kinauma ila sio serious relationships just for chating. Ila wao wanajua niko serious but ukweli kua niko frustrated. Nimeamua kuaachana nao but mmoja ndio ananiumiza kichwa maana yuko serious kupita maelezo.

Hata jinsi ya kumuambia kua niko married nashindwa kupata pa kuanzia. Ki ukweli niko confused sana na sioni faida ya kuoa. Nimekua kwenye shida for a long time na nahisi nikiwa single nitakua na uhuru. Sijajua nifanyeje ila nko bored balaaa na haya maisha ya ndoa.

Ndoa ya moto balaa mpaka hamu ya kuishi inapotea. Nashindwa kufikiria kurepair my relationship kitu nachofikiria ni divorce tu. Kwa sasa nimeamua kua kimya na kuishi alone kwanza nisome mchezo unaendaje but majaribu nayo ndio yanazidi kwani naposafiri nakua tempted sana.
 
Hapo tu ndo panapofanya nijifikirie mara mbilimbili suala la kuoa....
 
Pole sana mkuu. Kama majambo yenu ni mazito kiasi hicho washirikishe watu wazima.
 
Imenitokea ghafla sana kila nikikumbuka matendo yake mabaya kwangu nashindwa kumsamehe na ninamchukia kupita maelezo. Kifupi hata nikimuona hasira inanipanda na hata mawasiliano naye sitaki. Hua napenda kua mbali na watu na kukaa alone tu. Nimebadilika sana mpaka marafiki wananishangaa kua nimepoa mno na sionekani. Ila ukweli ni kua nimeumizwa moyo mpaka basi. Sitaki kujua habari zake na sitaki ajue zangu. Mpka sasa hua nasafiri safari nyingi but hawezi jua nipo wapi na nafanya nini.

Nimekua na relationships na wasichana wengi mpaka kichwa kinauma ila sio serious relationships just for chating. Ila wao wanajua niko serious but ukweli kua niko frustrated. Nimeamua kuaachana nao but mmoja ndio ananiumiza kichwa maana yuko serious kupita maelezo. Hta jinsi ya kumuambia kua niko married nashindwa kupata pa kuanzia. Ki ukweli niko confused sana na sioni faida ya kuoa. Nimekua kwenye shida for a long time na nahisi nikiwa single nitakua na uhuru. Sijajua nifanyeje ila nko bored balaaa na haya maisha ya ndoa. Ndoa ya moto balaaa mpka hamu ya kuishi inapotea. Nashindwa kufikiria kurepair my relationship kitu nachofikiria ni divorce tu. Kwa sasa nimeamua kua kimya na kuishi alone kwanza nisome mchezo unaendaje but majaribu nayo ndio yanazidi kwani naposafiri nakua tempted sana.
Polee ila cha msingi ni kumwambiaa ukwelii kuwa im merried !!
 
Mtoa mada pole lakini bado unayo nafasi ya kutengeza uhusiano wako na mkeo.
Jifunze kusamehe.
Duniani kuna makundi yafuatayo:
1. Wanaotaka kuoa kwa hamu
2. Wanaotaka kuolewa kwa hamu
3. Wanaotaka talaka kwa hamu
4. Wanashinda kuwashawishi wenzao waolewe au waoe
5. Wanaoponda wenzao ambao hawajaoa au kuolewa
Ila yote katika yote wewe ndio muamuzi wa maisha yako, usifate mkumbo.
 
Kama hukujipanga si usinge leta huu uzii maana cjakuewa kabisa nn kimekusibu from your mke punguza hasira jipange upyaa ueleze vzuri ilitukushauriii
 
Nimesoma upesi upesi na nikaamua niisome tena kwa ukimya mzuri nikagundua mawili au matatu yafuatayo;
  • Una tatizo la kutojiamini, huamini kama umeoa, huamini kuwa uan familia bado unaamini kwenye ujana
  • Una asili ya ubinafsi kwahio inakuapa shida sana ku-share na wengine, mkeo ndio mtu wako wa ku-share naye mambo mengi sijasema mambo yote nimesema mambo mengi.
  • una kiburi na kujikweza, hutaki kushindwa, hutaki kuelewa, ndio yako ndio NDIO na hapana yako ndio Hapana, misimamo ya style hii haiwezi kamwe kukupa amani
  • Umejiingiza kwenye mahusiano mengine kwa kisingizio cha kutendwa vibaya na mkeo, japo umeshindwa kusema kosa lako at least kwa ujumla wake tu
  • Hauko tayari kushaurika, hivyo utapotea zaidi badala ya kufanikiwa.
  • Wanawake wengi watakuumiza zaidi na hakuna atakayekupa faraja.
Hao wanawake unaowadanganya nao watakuja kuumia siku moja wakiujua ukweli, kwahio na wewe jiweke kwenye nafasi yao. Kumbuka kuna ujana na kuna utu uzima. Huwezi kuwa mtu mzima kisha ukaishi maisha ya ujana....utapotea.

The way forward; jifunze kujishusha, jifunze kuzungungumza, jifunze communication skills, soma maandiko mbali mbali jinsi ya kupunguza hasira na kiburi. Jichanganye na usitake kujiona wa maaana kuliko wengine, Brother, utaishi kwa amani tele out of that ujue kisukari, cancer, presha na mengineyo yanakusubiri. Pole, njoo inbox
 
Sasa bila kuekeza chanzo cha tatizo tutakusaidieje?
 
Kwani mkuu,huyo mkeo alikufanyia yapi na yapi? Kama inawezekana, pasuka hapa ili tukupe uzoefu wa kuyatatua kutokana experiences zetu.
 
Moyo umejeruhiwa,na shetani anapitia hapohapo kwenye hilo jeraha,anakuumiza na hilo ndilo analolitaka na mwishowe ni kweli mtaachana.Wakati mwingine mkeo anatenda mambo ya kukuudhi,wewe utafikiri ni yeye kumbe shetani anamtumia ili kutonesha jeraha lako na unajikuta uko palepale kwenye huzuni na hasira zisizo isha,soon High blood pressure itaanza kukusumbua,na utajikuta ni mtu mpweke usie hata na rafiki.Mrudie Mungu aweze kukuepusha na hayo yote otherwise ndoa yako itavunjika tu kwani ndicho anachokitafuta shetani hapo.
 
Imenitokea ghafla sana kila nikikumbuka matendo yake mabaya kwangu nashindwa kumsamehe na ninamchukia kupita maelezo. Kifupi hata nikimuona hasira inanipanda na hata mawasiliano naye sitaki. Hua napenda kua mbali na watu na kukaa alone tu. Nimebadilika sana mpaka marafiki wananishangaa kua nimepoa mno na sionekani. Ila ukweli ni kua nimeumizwa moyo mpaka basi. Sitaki kujua habari zake na sitaki ajue zangu. Mpka sasa hua nasafiri safari nyingi but hawezi jua nipo wapi na nafanya nini.

Nimekua na relationships na wasichana wengi mpaka kichwa kinauma ila sio serious relationships just for chating. Ila wao wanajua niko serious but ukweli kua niko frustrated. Nimeamua kuaachana nao but mmoja ndio ananiumiza kichwa maana yuko serious kupita maelezo. Hta jinsi ya kumuambia kua niko married nashindwa kupata pa kuanzia. Ki ukweli niko confused sana na sioni faida ya kuoa. Nimekua kwenye shida for a long time na nahisi nikiwa single nitakua na uhuru. Sijajua nifanyeje ila nko bored balaaa na haya maisha ya ndoa. Ndoa ya moto balaaa mpka hamu ya kuishi inapotea. Nashindwa kufikiria kurepair my relationship kitu nachofikiria ni divorce tu. Kwa sasa nimeamua kua kimya na kuishi alone kwanza nisome mchezo unaendaje but majaribu nayo ndio yanazidi kwani naposafiri nakua tempted sana.
Poleeee mkuu but naomba muongozo wako hujaweka wazi tatizo nn mpaka uchukie shemeji yetu.... But hujawah mkosea wweee hata siku moja kama ana mchepuko tafuta njia ya kutatua kosa moja halifukuz mke mkuu
 
Ukiingia ndoani jipange na yote mkuu ndoa ni vile ambavyo utaipeleka. hakuna mkamilifu wala kila mmoja ana mapungufu yake.
 
Ebu tuambie mkeo kakufanya nini kwanza mpk umchukie ivyo kingine ao wanawake zako usiwafiche kuhusu kuoa uwa mnaona aibu au
hamna jipya ni usaliti na mauzi yenu ndo vitu vikubwa vinavyompa dume stress to the max,mengineyo ni ngumu
 
Mkuu najua how do you feel, buh hujaweka wazi matatizo yako, pengine tumeshapitia huko uliko pita wewe, tunaweza kukuongoza vizur ili usiharibikiwe zaidi.

Kuwa frustrating lazima na hili ni kutokana unaweka kwenye moyo mambo yako instead of telling someone who can help you, iwe baba mama,or kaka or rafiki ambae atakae ficha siri yako.

Unaweza kamwambia hata sheikh kama muislamu, kama christo unapajua pa kwenda, actually popote pale kwa kiongozi wa dini unayo amini, watakupa ushauri.

Kwa vile huu uzi umeleta hapa, basi pia wako tutakao kupa ushauri, pia kwa kufanya maaamuzi ya kutafuta wanawake nje ni kosa na ndio mzigo wa matatizo yako.

Njoo inbox nitaweza kukupa ushauri pia
 
Back
Top Bottom