..Baada ya miezi 6 ya mahusiano nilishtuka kajihamishia kwangu......
[emoji115][emoji115][emoji115] Hapo umedanganya. Kuna vitu vilivyokufanya umpende mpaka ukakubali ahamie kwako. Pengine vitu hivyo kwa sasa havipo au vimebadilika. Au pengine ulitaka tu akusaidie katika hayo mambo ya rent na mengineyo na sasa umefikia melengo yako unamwona hafai. Kizungumkuti cha dunia: wenzio wanahaha kutafuta waume wa kuwaoa.
Ili kuzuia mikanganyiko jikaze tu umwambie ukweli. Toa sababu zako. Hata kama umepata mwanaume mwingine unayedhani anakufaa zaidi we mwambie tu. Hii ni bora kuliko kuanza kumfanyia visa na mambo mengine ya kitoto. Kama anakupenda kikweli atakuelewa na hatakulazimisha lakini lifanye hili kwa heshima, utashi mwema, uwazi na unyenyekevu. Kama unaona ni vyema unaweza kumwambia mbele ya mchungaji wenu au mtu mwingine mwenye mamlaka kama mama yako...Ukifanya vinginevyo si ajabu tutakuja kukusoma ukiwa kama mwathirika wa hawa wanaocharangwa mapanga na kuchomwa visu na wapenzi wao baada ya wapenzi wao kuwekeza sana tena kwa muda mrefu halafu wanakuja kuwafanyia visa vya kijinga mwishoni mwishoni huku...