I cant get enough... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

I cant get enough...

Discussion in 'Entertainment' started by jmushi1, Dec 22, 2011.

 1. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Huu mpini wa J.Cole una beats ka za bongo flavor...


  Umetulia kiaina...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 2. Heart

  Heart JF-Expert Member

  #2
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 2,660
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  i'l search for it...na mie niusikilize..
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  HEART, Nimekuwekea linki hapo juu, ni video through youtube.
   
 4. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #4
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  It is a nice catchy song....
  Nimependa back beats and sounds zaidi... Sijui ni ladies wale or watoto.... I have added it to my recent playlist.
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Huu wimbo ni wimbo wa Ki-Africa hasa na ndiyo maana wengi wenu mmeupenda.

  Cole kafanya ku-Sample huo wimbo na kuuweka kwenye RAP na kwa hilo namsifu.

  Hata mie mwenyewe ilibidi niwaagize washikaji majuu waninunulie CD yake na wanitumie.

  Wimbo hasa unaitwa Can't Get Enough na video yake haswa hii hapa chini....  Wimbo Original uliandikwa na wanamuziki ambao kwa sasa ni Wazee sana. Hii band ya Balla et Ses Balladins ilikuwa ni band ya serikali na baadhi ya wanamuziki wa band hii walishiriki kupiga miziki ya Miriam Makeba wakati akiishi Guinea, Conacry. Baada ya serikali kushindwa kuidhamini, band ilikufa rasmi kama band ya serikali ila hadi leo wazee hawa huwa wanaonekana mara moja moja wakifanya Concert.

  Baadhi ya TV Station, wanaandika watunzi wa wimbo huo ambao ni Kouyate na mwingine simkumbuki kwa jina. Cole kwa kweli kawanyenyua hawa wazee na sasa dunia nzima imeshaanza kuwafatilia na CD zao naanza kuziona ONLINE kwa wingi sasa.

  Paullete na Balla Et Ses Balladins, kibao cha mwaka 1980, kutoka Conacry, Guinea.

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #6
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Itakuwa kawapa shavu la nguvu, imetulia kwa kweli.

  I wonder if Jigga hana mkono kwene hili since J Cole ni kijana wake.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #7
  Dec 23, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  Thanks Sikonge... I wanted the Catch! No wonder... sasa nimeipata.
   
 8. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #8
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kwanza samahani sikuweka LIKE maana Laputopu yangu ina matatizo na nashindwa kuweka LIKE.

  Jigga atakuwa na mkono wake na kumbuka hata Mkewe Beyonce, kwenye wimbo wake alitumia chezaji ya vijana wa Msumbiji waitwao Tofo Tofo Boys. Inaonekana wamekuwa na imani au upenzi na Africa kwa nguvu sana na hawaoni shida ya kuchukua vitu na kuvitangaza.

  Hawa wazee wameula uzeeni. Mie mwenyewe natamani kuwaona kwenye Concert yao wakishusha vitu vya uhakika maana uzoefu wao kwa kweli utakuwa unatisha.

  Beyonce aliposhindwa kucheza / Kujifunza uchezaji wa Tofo Tofo, aliamua kuwafuata Msumbiji na vijana wakapata VIZA na kutua USA ili kutoa shule kwa Beyonce. Vijana nasikia nao Msumbiji wapo juu sana maana News zilikuwa kila sehemu....


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 9. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #9
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Quite something! ... Ladha ya Kiafrika ... Utaitambua tu!!
   
 10. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #10
  Dec 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,569
  Likes Received: 1,936
  Trophy Points: 280
  Ndicho nachompedea Jigga, vision, kwa kweli nimefarijika licha ya mambo mabovu ya viongozi wetu...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #11
  Dec 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  AshaDii, pamoja sana. Taratibu Africa itaamka.
   
 12. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #12
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Tamu sana hii...
  Thanks Jmushi na Sikonge...!
   
 13. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #13
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Pamoja sana mkuu. Nafikiri wanaosema Waafrica hatuwezi kitu, basi inabidi wafikiri mara mbili.

  Huu ni mfano halisi wa "Tukiwezeshwa, tunaweza hata sisi......"
   
 14. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #14
  Jan 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Wala hatuitaji kuwezeshwa Mkuu....
  Hapo hujamwaga vitu vya gallery ya Femi Kuti Sr....
  Kuna mtu alikuwa anaitwa Paul Simon (sijui yupo hai??), yule mzungu msouth afrika mpinga ukaburu alipiga show ya Halale zimbabwe na kumleta Miriam Makeba baada ya kuondoka kwa miaka 27 uhamishoni, natamani nikupe Video hapa ila mautundu yananipiga chenga kuweka video ambazo haipo kwenye site, humo kuna wale "Red Smith and Black Mambazo"....
  Najiona kama nipo peponi, jigga tunamkaribisha sana

   
 15. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #15
  Jan 2, 2012
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hahahaa, Graceland Concert siyo? Pamoja na Mzee wa Stimela (Ray Phil), Hugh Masekela, Ladysmith Black Mambazo ......

  Ni moja ya DVD ambayo ninaipenda sana.

  Nilibahatika kuja kuona Live show ya Black Mambazo miaka kadha nyuma kwa kweli ilikuwa ni nzito sana.

  Zimbabwe ilikuwa nchi moja iko juu sana. Nilishawahi kununua DVD ya Don Williams (Country) alipokuwa Zimbabwe. Anasema alisita sana kwenda Africa na hasa kwa mwimbaji wa Country kama yeye. Ila alipofika huko, alishangaa kukuta hadi kuna wimbo wake wanauimba kwa Kishona. Pia wimbo wa "You are my best friend" unaanza kwa kuonyesha vipofu wawili mjini Harare, wanaimba huo wimbo. Jamaa alishangaa sana. Cha ajabu kwenye concert zake, nusu ni wazungu na nusu ni Waafrica weusi.

  Video moja nakuwekea, nyingine ziangalie kwenye youtube.....


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...