I am single now, she left yesterday!

I am single now, she left yesterday!

Zinduna

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2011
Posts
2,377
Reaction score
3,394
Wana jamii kichwa cha habari kinahusika hapo juu.

Kuna kaka mmoja tulikutana online mwishoni mwa mwaka juzi, (siyo Jamii Forum lakini) sasa katika ku-chat akaanza kunieleza matatizo ya mke wake kuwa yuko hivi yuko vile yaani alikuwa ananieleza mpaka udhaifu wa ndani wa huyo mke wake kitu ambacho nilikuwa sikifurahii kabisa.

Kwa upande wangu nilikuwa najaribu kumshauri hivi na vile kulingana na ufahamu wangu kwa hiyo akawa anawasiliana na mimi pale anapokuwa amekwazwa na huyo mkewe. Kuna wakati alinitaka tukutane ili kujuana zaidi nikaweka ngumu na nikamweleza kwamba siko tayari kuonana uso kwa uso na mtu tuliyekutana mtandaoni na nikamsisistiza ajitahidi kukarabati ndoa yake ili amani irejee nyumbani kwake maana hazipiti siku mbili nyumbani hakulaliki.

Hata hivyo mwanzoni mwa mwaka huu alinikera pale aliponieleza kwamba, angependa kunioa niwe mkewe wa pili, (Kwa huku visiwani ndoa ya mke zaidi ya mmoja kwa wanaume siyo jambo la kustaajabisha) nikamwambia siko tayari kuolewa mke wa pili nataka mume wa peke yangu.

Tukaweka nukta, na mawasiliano yakawa ni yale ya kawaida tu ya ku chat kiurafiki.

Sasa jana ndiyo kanitumia huo ujumbe mfupi wa simu ya mkononi hapo juu na akasisistiza sasa kwamba kwa kuwa nilikuwa ninataka mume wa peke yangu sasa mambo yamekuwa safi kwa sababu yule aliyekuwa kikwazo kajiondokea zake sasa yupo single na yuko tayari kuleta posa nyumbani ili tuoane.

Kwa kifupi ni kwamba nimepinga sana wazo lake hilo la kitoto na nimem delete kabisa kwenye mawasiliano yangu maana naona huyu mwanaume hazimtoshi.

Naomba kuuliza, hivi wanaume wa aina hii huwa wanafikiria kwa kutumia bongo zao au makalio, yaani ushindwe kuilinda ndoa yako hadi ikuponyoke halafu ukurupuke kutangaza ndoa kwa mtu usiyemfahamu!

Wanawake wenzangu hebu nipeni uzoefu wenu.
 
nanyie wanawake huwa mnatumia makalio kuchati na kila mwanaume na kuwakukubali?
 
mmh yani huyo ni muongo muongo muongo kimbia mbio za farasi loh, hapo hajaachana na mkewe wala nini ukimkubali tu imekula kwako utakuwa mke wa pili, na hayo matatzo aliyokuwa anakwambia hamna lolote alikuwa anakutafutia sababu ya kukupata, wanaume wa online wengi wao ni OGOPA
 
Inaonekana unaushauri mzuri sana jamaa ulikuwa unampa dawa akaona ili akufaidi vizuri daktari hana budi akuoe ili uwezi kumtibu zaidi, hebu ngoja na mim siku nikufuate PM nione kama tunaweza kuyajenga, na hiyo avatar yako hapo hebu mwambie huyo dada akae vizuri
 
Ww ulimuonyesha kama unataka kumpa tunda umepewa chance unazingua?...kwann mnawapa watu matumaini wakat hampo serious
 
Wana jamii kichwa cha habari kinahusika hapo juu.

Kuna kaka mmoja tulikutana online mwishoni mwa mwaka juzi, (siyo Jamii Forum lakini) sasa katika ku-chat akaanza kunieleza matatizo ya mke wake kuwa yuko hivi yuko vile yaani alikuwa ananieleza mpaka udhaifu wa ndani wa huyo mke wake kitu ambacho nilikuwa sikifurahii kabisa.

Kwa upande wangu nilikuwa najaribu kumshauri hivi na vile kulingana na ufahamu wangu kwa hiyo akawa anawasiliana na mimi pale anapokuwa amekwazwa na huyo mkewe. Kuna wakati alinitaka tukutane ili kujuana zaidi nikaweka ngumu na nikamweleza kwamba siko tayari kuonana uso kwa uso na mtu tuliyekutana mtandaoni na nikamsisistiza ajitahidi kukarabati ndoa yake ili amani irejee nyumbani kwake maana hazipiti siku mbili nyumbani hakulaliki.

Hata hivyo mwanzoni mwa mwaka huu alinikera pale aliponieleza kwamba, angependa kunioa niwe mkewe wa pili, (Kwa huku visiwani ndoa ya mke zaidi ya mmoja kwa wanaume siyo jambo la kustaajabisha) nikamwambia siko tayari kuolewa mke wa pili nataka mume wa peke yangu.

Tukaweka nukta, na mawasiliano yakawa ni yale ya kawaida tu ya ku chat kiurafiki.

Sasa jana ndiyo kanitumia huo ujumbe mfupi wa simu ya mkononi hapo juu na akasisistiza sasa kwamba kwa kuwa nilikuwa ninataka mume wa peke yangu sasa mambo yamekuwa safi kwa sababu yule aliyekuwa kikwazo kajiondokea zake sasa yupo single na yuko tayari kuleta posa nyumbani ili tuoane.

Kwa kifupi ni kwamba nimepinga sana wazo lake hilo la kitoto na nimem delete kabisa kwenye mawasiliano yangu maana naona huyu mwanaume hazimtoshi.

Naomba kuuliza, hivi wanaume wa aina hii huwa wanafikiria kwa kutumia bongo zao au makalio, yaani ushindwe kuilinda ndoa yako hadi ikuponyoke halafu ukurupuke kutangaza ndoa kwa mtu usiyemfahamu!

Wanawake wenzangu hebu nipeni uzoefu wenu.

Mwambie poa, posa atume kwa M-pesa afu ndoa mfungie kupitia Skype. Anajifanya hamnazo nawe jifanye chizi!
 
Indeed, alimchoka mkewe.. yani ameondoka jana tu... leo anakuhitaji wewe..... ya visiwani... siyawezi!!
 
Tunaomba 'behind the scene' special edition...JF release due to viewers' demand!!!
 
mambo ya facebuk muwe mnamalizana huko huko,huku kwa watu wazima huwa tunatongozana kimya kimya tunatafunana kimya kimya na tunatosana kimya kimya
 
Back
Top Bottom