OLS
JF-Expert Member
- Oct 12, 2019
- 457
- 773
Naanza kwa kusema kuwa hii ni kama Hypothesis, yoyote anaweza aka-test kwa statistical data kujua kama ina hold au la
Kwa miezi kadhaa kulikuwa na joto kali la kisiasa, hili ndio sababu kubwa ya baadhi ya bidhaa hasa saruji kupanda bei kwa kiasi kikubwa. Imeonekana hivi karibuni kuwa viwanda vingi viliacha uzalishaji wengine wakisingizia kufanya usafi nk
Hali halisi ni kuwa yanapotokea machafuko katika nchi, matajiri ndio huwa wa kwanza kuathirika kwa kuwa wana miundombinu nk. Lakini kwa masikini wao huwa neema, ndio sababu kuna watu kwenye migomo au maandamano huingia kwenye maduka ya watu na kujichukulia wanachoweza kuchukua au kufanya matukio yoyote ya kujinufaisha kwa muda husika
Kutokana na matajiri kuwa na vitu vingi vya kupoteza, hasa ukichukulia hao wenye viwanda vya uzalishaji ni lazima wa-freeze kwa muda kupima upepo ili kama kutatokea tafrani wasiwe na hasara kubwa
Hii imeonekana kwa viwanda hivyo kwa kuacha kuzalisha ili kuepuka hasara kubwa ambayo ingeweza kutokea kama kungekuwa na machafuko kama migomo, maandamano na mapigano yasiyoisha
Kutokana na hatua hiyo uzalishaji ulionekana kuwa chini huku uhitaji ukiwa bado uko juu, hali hii ili-push bei kwa haraka na kufikia kiwango hiko ambacho isingekuwa rahisi kupanda kawaida ndani ya wiki mbili
Hili linatosha kuonesha athari za machafuko ya kisiasa kiuzalishaji na kimaendeleo kwenye taifa lolote