Huyu x ana nini?

Huyu x ana nini?

Habari zenu wanajamii...?
Mimi kuna linalonisumbua sana na nina amini humu nitapata ushauri, naombeni sana sana mnishauri kistaarabu kwa wale mliozoea kuharibu na kutukana kwa muda huu mnivumilie mwenzenu nina shida.
Mimi ni mwanamke na umri wangu nipo above 25.
Miaka kama 3 iliyopita niliwahi kuwa na mpenzi ambaye tunakalibiana umri ingawa yeye ni mkubwa wangu.
Tulidate kwa muda mrefu sana na napenda kuwa mkweli kuwa nilimpenda kweli pamoja na madhaifu yake yote.
Sijui kwa upande wake ila tuliachana baada ya yeye kuanza kushika pesa na kuamua kuniacha kwa kunisingizia kuwa napenda wanaume na vitu vingi ambavyo si kweli. Kesi ambayo ilifika mpaka kwa wazazi wake coz nilikua nikijulikana kwao.
Baada ya maumivu na kulia sana nikaona nimove on na maisha yangu.
Siku sina hili wala lile, dada yake akanipigia simu kuwa ana shida nami nikamsaidia bila kinyongo. Usiku wa siku hiyo jamaa akapata taarifa toka kwa dada yake ndipo akaamua kuja kuniomba msamaha sana kwa yote aliyofanya but anataka urafiki nami tuendelee kusaidiana na bla bla bla.
Binafsi sikuona haja ya kuweka kinyongo sababu kama mtu hajakupenda huwez kulazimisha hivyo tukawa marafiki ambao hatukuwa karibu kama zamani ila yeye akaendelea kustay in touch nami mara kwa mara.
Hatua ya kuongea kila mara ikaleta kushirikiana kwa karibu sana. Akanijulisha kuwa ana girl wake nami nikamuonyesha a man ninae date nae. Tukawa marafiki wa aina hiyo. Kila kitu ananishirikisha.
Kugombana kwetu ni kawaida sana. Kila mara tunagombana kwa vitu vidogo vidogo. Mfano baada ya utambulisho mwenzangu alinikasirikia sielewi hata sababu.
But hivi karibuni nimeshangazwa na ugomvi mmoja ambao binafsi sielewi kabisa kwa nini unatokea. Akitu kimoja.
Katika story tunazoongeaga, uwa pia tunakumbuka vituko vya zamani na kukumbusha na kucheka. Ila leo nilimuuliza mwenzangu " Wakati tunadate kipindi kile, ivi ulikuwa unanidanganya au ulinipenda kweli?"
Nilipouliza swali hilo mwenzangu alipata hasira na kubadilika ghafla, binafsi sioni hata haja ya kukasirika. Nimeona ni kama swali la kawaida sana, naombeni ushauri kama kuna lolote ninalokosea au hilo swali sikupaswa kuuliza?
Tafuta "Y"
 
Nyie mnataka kupasha kiporo . Mmeachana muda mrefu, kuna maswali ambayo si ya kuuliza maana yanakusha ya nyuma.

Ni vizur kila mtu akatulia. Zake.. la si hivyo mkiendelea.. mtakumbushia tu
 
Kipyenga cha kuanzisha boli hakijapulizwa tayari 4-0 haya ukipewa mimba uje ufungue uzi tena uulize sijui umeingiaje
 
Inawezekana kabisa jamaa kukuacha hakukusinhizia ni tabia yako
 
Mistake ulioifanya ni kuruhusu kuendelea kua na mawasiliano naye japo hamko kikaribu mawasiliano n mawasiliano tu

Unaweza ku move on completely na hata usiwe na mawasiliano na ex wako huku ukiwa huna kinyongo pia na maisha yakaenda

Achana na yeye na why akuumize kichwa?? Fine kakasirika haikua na haya ya kujali hivo mana tayar inaleta taswira halisi bado anaishi moyoni mwako

Focus na mahusiano yako mapya, achana na ex ameshakua ana example of what you shudnt have in future
 
Jibu hapo ulikuwa nalo tayari ndio maana alikuacha, hakukuwa na haja ya kumuuliza yeye
 
He is your x, what u care about? Move on bhana, anza kukaa mbali nae naona anaanza kurudi moyoni mwako, kama akikasirika unaanza kuwaza basi we utakuwa mtumwa yaani moyo wako utawatumikia mabwana wawili. Kama amekasirika we kaa kimya fanya yako ye si ndo alijileta kwako. Thamini zaidi mahusiano uliyonayo sasa maana huyo wa sasa akigundua ukaribu huu na x wako hakika atakuacha maana kukumbushia ni kitu cha dakika 1 tu hasa mkiwa eneo faragha. Muache! Angalia ulipo sasa! Fanya yako! "Aliyeshika jembe tayari kulima huku anaangalia nyuma hafai katika ufalme wa mbingu"
 
Wakati tunadate kipindi kile, ivi ulikuwa unanidanganya au ulinipenda kweli?"
Nilipouliza swali hilo mwenzangu alipata hasira na kubadilika ghafla, binafsi sioni hata haja ya kukasirika. Nimeona ni kama swali la kawaida sana, naombeni ushauri kama kuna lolote ninalokosea au hilo swali sikupaswa kuuliza?

Swali lako inawezekana likawa na shida na inawezekana lisiwe na shida. Inategemeana na nyie wawili.
Ila dada shida wala sio hilo swali lako.
Shida ni kwamba, ingetakiwa ufungue uzi kama kuna issue huielewi kati yako na mpenzio wa sasa.
Hiyo tu ndo shida!
 
Matatizo ya Kuwa idle haya. Jishughulishe hata kwa kuuza karanga mtaani mkuu
 
Kuendelea kuwasiliana na ex wako ni kama kutembea na muwa kama mkongojo ipo siku utautafuna tu.....
 
Sasa hapa unataka msaada gani? We mpe tu kwani kuna shida gani kama bado una mpenda. !!
 
Back
Top Bottom