TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,563
Wakati sisi mashabiki wa Almasi tukisumbua kwenye mitandao ya kijamii tukiamini tumeitawala Afrika kufuatia colabo ya msanii wetu kipenzi na Neyo, msanii ambaye kwa sasa ni 'zilipendwa' kule nchini Marekani kule Nigeria msanii Wizz Kid amezidi kutunyima pumzi na kutukatisha tamaa,mara ya kwanza tulisikia eti ameshirikishwa na Chris Brown katika wimbo wake mmoja hivi ambao unasumbua sana katika billboards charts, mara tukasikia eti Wiz Kid yupo na Chris Brown katika ziara ya pamoja ya kimuziki kule Ulaya wakifanya show pamoja jukwaani.
Hata akili zetu hazijatulia kufuatia msanii wetu kipenzi Almasi kuikosa tuzo ya muziki ya B.E.T mara safari hii tunasikia eti Wizz Kid 'The Star Boy' ametoa singo mpya iitwayo 'SHABBA' akiwashirikisha akina Chris Brown,Trey Songz na French Montana wakati msanii wetu na sisi mashabiki wake tumekuwa tukisumbua juu ya singo mpya iliyowashirikisha P-Square ambao ni wasanii wengine 'zilipendwa' kwa kule nchini Nigeria.
Aah kwa kweli nimekata tamaa kabisa kama kweli sisi Team Almasi tunaitawala Afrika, kweli tuna safari ndefu sana kuitwa wafalme wa Afrika.