Huyu Ridhiwani ninani???

Huyu Ridhiwani ninani???

Status
Not open for further replies.
Kikwete ni fisadi penda usipende. Usitufanye sisi wajinga. Mali za Ridhwani zinajulikana. Bongo ni nchi ndogo, hakuna siri. Kila kiongozi wa Tanzania lazima atajitarisha na ataitajirisha familia yake. Kuanzia Mwinyi, Mkapa, na sasa Kikwete. Na kiongozi atakayefuata naye atafanya hilo hilo. Atajineemesha yeye na familia yake. Watanzania wataendelea kutaabika.

Wewe usemae Kikwete fisadi, leta ushahidi kama hauna kaa kimya. Mali usemazo za Ridhwani leta ushahidi wacha porojo.

Nyinyi ndio wale hata nzi mkubwa mnasema wa kizungu huyo. Kushindwa kwakokimaisha utafute sababu kwa mwengine.

Jiulize walioweza wamewezaje wewe umeachwa mkiani? jibu ni simpo, ni kwa ujinga wako, ni kwa uvivu wako, ni kwa kungoja kwako ufanyiwe.
 
Wacha upunguani. Hiyo TAKUKURU imepewa meno na Kikwete, walikuwa na uwezo wa kuchunguza mawaziri au mawaziri wa zamani? wakati wa Kikwete tumeona mpaka kina Mramba wakifungwa. Upo hapo ulipo.

Na wakikutikana na hatia kesi ni mahakamani. Hilo la kufikishwa tu TAKUKURU ni hatua moja nzuri sana na Serikali ya Kikwete inabidi isifiwe.

PCCB kama kweli wanameno mbona kesi nyingi sana huisha kinyemela hasa zile zenye mkono wa Rais? yasemwayo kuwa dogo riz anamiriki ukwasi mkubwa na utitiri wa miradi na majumba yaotayo kama uyoga ni ya kweli kabisa! hiyo operating capital kubwa namna hii kaipata wapi? mabilioni haya kayakopa benki gani na kwa sifa zipi kama sio mgongo wa ofsi ya babayake?
we kikongwe FF acha akiri za kijuha ilewa kuwa huwatendei haki watz na usiniambie kuwa vijisenti upewavyo kwa kuwatetea hawa wadharimu watakula hadi vitukuu vyako!
 
Naona una usingizi hujui hata unachoandika,Mramba kafungwa lini wakati kesi yake inapigwa danadana?kuhuisu TAKUKURU fuatilia maoni ya Mkurugenzi wa TAKUKURU kwenye tume ya katiba alisema nini kuhusu uhuru wa taasisi anyoiongoza,acha kudanganya watanzania wenzako.Tatizo mnasoma elimu ahera sana alafu mnataka madaraka.Na penye milioni 600,Maige kandanganya?kanusha.

Wewe ndiye uliye usingizini hujui kuwa Mramba kaachiwa kwa dhamana ambayo ni haki na sheria kwa kila mtu anaetimiza?

Huo ni usingizi tena wa pono. Mchana kweupe , wewe umelala.

Hilo la TAKUKURU waachie TAKUKURU wafanye uchunguzi wao, kufikishwa mawaziri au mawaziri wa zamani kuchunguzwa na TAKUKURU tena kinaga ubaga, hiyo ni hatua kubwa sana na inabidi Kikwete asifiwe kwa hilo, ameweza.

Maige akidanganya au asidanganye wewe umejuwaje? umekuwa mtabiri?

Hiyo elimu yetu wewe achana nayo, wewe jibu hoja hapa usitake kuyafanya haya yakawa ya kidini ambayo ndio chuki zako zote za Kikwete. Huyo huyo wa "elimu ahera" ndiye Rais wako na amefanya vyema kuliko wa sunday school Nyerere na Mkapa.

Wewe si bure, itakuwa ni mwanafunzi wa Father Kit Cunningham wa Soni.
 
Wewe usemae Kikwete fisadi, leta ushahidi kama hauna kaa kimya. Mali usemazo za Ridhwani leta ushahidi wacha porojo.

Nyinyi ndio wale hata nzi mkubwa mnasema wa kizungu huyo. Kushindwa kwakokimaisha utafute sababu kwa mwengine.

Jiulize walioweza wamewezaje wewe umeachwa mkiani? jibu ni simpo, ni kwa ujinga wako, ni kwa uvivu wako, ni kwa kungoja kwako ufanyiwe.

Kikwete na ridhiwani ni mafisadi papa, na lowassa anawatamani kweli kweli. Ngoja apate cheo chake 2015 ndiyo mtamjua.
 
Ukweli kujulikana hata mtandaoni ni mchakato au harakati nzuri.unajua wazungu wao waona mbali sanaaa.kuzipa masharti nchi za dunia ya tatu juu ya uhuru wa kujieleza ulikuwa ni msaada tosha sana kwetu.kwani tuna utamaduni wa kusifiana kila kitu,watu wanazikwa wakiwa hai na bado wanashukuru.

Wengi tunajua ukweli lakini tumeshafanya nini? Na hata kama watu wanaojua wakiongezeka ndiyo watafanya nini? Kura zao wanapata kule vijijini ambako watu hawajui mtandao ni kitu gani. Yaani taifa linaburuzwa tuu. Wakikuona unapiga sana kelele jua kabisa watakufanyia kitu kibaya.
 
PCCB kama kweli wanameno mbona kesi nyingi sana huisha kinyemela hasa zile zenye mkono wa Rais? yasemwayo kuwa dogo riz anamiriki ukwasi mkubwa na utitiri wa miradi na majumba yaotayo kama uyoga ni ya kweli kabisa! hiyo operating capital kubwa namna hii kaipata wapi? mabilioni haya kayakopa benki gani na kwa sifa zipi kama sio mgongo wa ofsi ya babayake?
we kikongwe FF acha akiri za kijuha ilewa kuwa huwatendei haki watz na usiniambie kuwa vijisenti upewavyo kwa kuwatetea hawa wadharimu watakula hadi vitukuu vyako!

Toka Kikwete kaanzisha TAKUKURU tunaona kesi nyingi za rushwa kuliko wakati wowote ule mahakamani, tumeona mawaziri na waliokuwa mawaziri wakifikishwa mahakamani. Uliyaona hayo kabla ya TAKUKURU.

Usisahahu ni nani aliyoianzisha TAKUKURU na usisahau ni nani aliyoipa meno, na bado meno hayatoshi na inaendelea kuboreshwa. Usifikiri taasisi kama hiyo inaanzishwa leo na kuwa na sheria zote mikononi mwake leo, uozo uliokuwepo kwa miaka 44 kabla ya Kikwete si rahisi kutatua kwa siku moja. Lakini kazi zake na mafanikio yake wenye macho tunayaona:

Statistics as from 2005 to October 2013 translate as follows:

  1. 49,853 Allegations were received since 2005 to OctoberNot all the allegations being reported are related to corruption.
  2. Number of administrative actions taken against public servants proven to be inclined to take bribes and other corrupt behavior since 2005 to October 2013 is 816 Public Servants.
  3. Number of new cases filed into courts since the new Act (PCCA, 2007) became operational are 1,557 cases.
  4. Number of convictions against corrupt offenders in courts since 2005 to October 2013 are 378.
  5. Money recovered by PCCB for the period 2005 to October 2013 is to the tune of Tshs. 47,686,737,345/= Billions.
Source: Case Statistics

Uliyaona hayo kabla ya Kikwete?
 
Kikwete na ridhiwani ni mafisadi papa, na lowassa anawatamani kweli kweli. Ngoja apate cheo chake 2015 ndiyo mtamjua.

Fikra finyu.

Lowassa na Kikwete hawajajuana mitaani.
 
Wewe usemae Kikwete fisadi, leta ushahidi kama hauna kaa kimya. Mali usemazo za Ridhwani leta ushahidi wacha porojo.

Nyinyi ndio wale hata nzi mkubwa mnasema wa kizungu huyo. Kushindwa kwakokimaisha utafute sababu kwa mwengine.

Jiulize walioweza wamewezaje wewe umeachwa mkiani? jibu ni simpo, ni kwa ujinga wako, ni kwa uvivu wako, ni kwa kungoja kwako ufanyiwe.

Hujui maisha yangu kwa hiyo usi ASSume kama mimi maisha yamenishinda. Hakuna haja ya kutoka nje ya hoja na kuleta kashfa binafsi. Unasema tulete ushahidi. Ushahidi utapatikana tuu pale ambapo independent investigation itavyoanza kazi. Kama siyo wezi waruhusu third party investigation ifanye uchunguzi. Waangalie hizo biashara ambazo watu wanajua ni za Ridhwani, waangalie akaunti za benki zilizopo nje ya nchi. Kama ma organization mengi ya kimataifa yanafanya hizi kazi. Waje hapa wafanye uchunguzi walete ripoti tuisome ndiyo tujue kweli ni wasafi. Lakini kamwe hawawezi kukubali hilo kwa sababu wanajua wameshafanya maovu na ufisadi wa hali ya juu.
 
Watanzania wajinga kweli, zamani ilikuwa kila kitu kikubwa ni cha "kizungu", sasa kwa ule ule umbumbumbu ni cha "Rais" au "mtoto wa Rais".

Hivi kwa upuuzi kama huu mnategemea mtaendelea? mimi nasema "mawee".

Badala ya kutwa kukaa kusifia vya wanaume wenzenu na nyinyi ingieni wivu wa kufanya si kusengenya, wasengenyaji wakubwa nyie.

Duuuh FF una matusi...
 
you have 10% sio bure.
 
Ni mtoto wa raisi ambae hutoza 10% kama rushwa kwenye miradi mbalimbali ya serikali yenye ubia na wawakezaji kutoka nje
 
Wewe unaleta post ya kujua mwanaume mwenzako halafu iweje sijui unamuuongelea ridhi yupi wa mama said au yule wa kidinda kwanza jengo lipi unaloongelee stand ya somanda au bariadi mjini hebu dadavua kwanza ueleweke.

wewe unamjua rizi yupi?? niujinga kamatutaendelea kushabikia watu wanma hii,, badala ya kuhoji, wewe ukinyamaza leao watoto wako watakuuliza kesho na nilazima uwape majibu
 
Hapa morogoro kihonda kuna LI-ZIWANI anafanya kazi CAR WASH, nae ana ghorofa pale stand ya mabasi MSAMVU! mbona wako wengi!
 
Hivi yanayoandikwa humu yanaushahidi au ni kahawa, tende, haluahalua na kashata. Maana ninavyoona hata hii nyumba ninayoishi mtakuja kusema ni ya RIZ
 
Toka Kikwete kaanzisha TAKUKURU tunaona kesi nyingi za rushwa kuliko wakati wowote ule mahakamani, tumeona mawaziri na waliokuwa mawaziri wakifikishwa mahakamani. Uliyaona hayo kabla ya TAKUKURU.

Usisahahu ni nani aliyoianzisha TAKUKURU na usisahau ni nani aliyoipa meno, na bado meno hayatoshi na inaendelea kuboreshwa. Usifikiri taasisi kama hiyo inaanzishwa leo na kuwa na sheria zote mikononi mwake leo, uozo uliokuwepo kwa miaka 44 kabla ya Kikwete si rahisi kutatua kwa siku moja. Lakini kazi zake na mafanikio yake wenye macho tunayaona:

Statistics as from 2005 to October 2013 translate as follows:

  1. 49,853 Allegations were received since 2005 to OctoberNot all the allegations being reported are related to corruption.
  2. Number of administrative actions taken against public servants proven to be inclined to take bribes and other corrupt behavior since 2005 to October 2013 is 816 Public Servants.
  3. Number of new cases filed into courts since the new Act (PCCA, 2007) became operational are 1,557 cases.
  4. Number of convictions against corrupt offenders in courts since 2005 to October 2013 are 378.
  5. Money recovered by PCCB for the period 2005 to October 2013 is to the tune of Tshs. 47,686,737,345/= Billions.
Source: Case Statistics

Uliyaona hayo kabla ya Kikwete?

Na yeye mwenyewe angeleta watu wa nje wamu investigate ndiyo angetupa confidence kidogo. Kuwa investigate makarani na maofisa wa vyeo vya chini wanaokula rushwa mbuzi siyo kitu cha kujivunia. Afanye investigation ya hao ma big fish na ajianzie mwenyewe na familia yake.
 
Wacha upunguani. Hiyo TAKUKURU imepewa meno na Kikwete, walikuwa na uwezo wa kuchunguza mawaziri au mawaziri wa zamani? wakati wa Kikwete tumeona mpaka kina Mramba wakifungwa. Upo hapo ulipo.

Na wakikutikana na hatia kesi ni mahakamani. Hilo la kufikishwa tu TAKUKURU ni hatua moja nzuri sana na Serikali ya Kikwete inabidi isifiwe.

Mramba kafungwa lini?hiyo Takukuru ni kiini macho tu mana kama Dr Hoseah mwenyewe anasema kama angekua na mamlaka thn angefanya makubwa ila nguvu zote ziko juu na huwezi kumchunguza au kumhukumu aliekuteua kushika wadhifa flani
 
Watanzania wajinga kweli, zamani ilikuwa kila kitu kikubwa ni cha "kizungu", sasa kwa ule ule umbumbumbu ni cha "Rais" au "mtoto wa Rais".

Hivi kwa upuuzi kama huu mnategemea mtaendelea? mimi nasema "mawee".

Badala ya kutwa kukaa kusifia vya wanaume wenzenu na nyinyi ingieni wivu wa kufanya si kusengenya, wasengenyaji wakubwa nyie.

n'a ww ni fisadi kuleni mali ya umma mkijua hakuna mwisho endeleeni kujitanua kwa kuwafanya watanzania mambulula. ss haturidhiki iweje leo kila kitu ni cha watoto wa viongozi Mpaka magari ya taka no yenu uda yenu kitaeleweka tu.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom