Huyu Pastor Hananja adhibitiwe. Ataleta maangamizi

Cashman

JF-Expert Member
Jun 8, 2018
2,293
3,965
Huyu mtu anajitambulisha kama pastor mstaafu na amekuwa maarufu sana kwenye media.

Jana kuna jamaa mmoja aliyesikia moja ya mafunzo yake kuhusiana na mahusiano ya mapenzi na ndoa.
Alimsikia akisema kina mama wenye umri wa miaka zaidi ya 40 wanapenda sana vijana wadogo kama ambavyo wanaume wenye umri mkubwa wanavyopenda vibinti.

Sasa jamaa analalamika sana mkewe sasa hivi kawa mkali na hamjali na wala hana hamu ya kufanya naye tendo la ndoa.Alivyosikia kauli hizi tena zinatoka kwa mtumishi anayejiita wa Mungu, aliamini hadi kufikia kumtilia mashaka mke wake kuwa huenda ana tembea na wavulana wadogo.Jamaa alisema hali hii ikiendelea,atamgawanya mkewe vipande viwili.Hahitaji kuwa na ushahidi zaidi ya hicho anachofanyiwa na mkewe.

Sasa nimeandika hivi,na kuomba huyu Mzee (Pastor) adhibitiwe,kwa kuwa analeta hofu katika ndoa za watu.Ujumbe wake hauna matumaini zaidi ya kuleta taharuki.Huyu jamaa akimchinja mkewe kwa hisia tu kwa vile amesikia kutoka kwa Mchungaji ,hamuoni hiyo ni hatari sana?

Nimesikia matukio ya mauaji yameongezeka sana hasa yanayohusiana na wivu wa mapenzi.Na Waziri akatoa rai kwa viongozi wa dini wawasaidie wananchi.Itakuwaje kwa wachungaji kama hawa wanaochochea taharuki kama hizi?

Kwa uelewa wangu mdogo, akina mama wanapofikia umri wa utu uzima,huwa wana kipindi cha mpito kutoka katika siku zao za kila mwezi kuingia kipindi ambacho hawaoni tena siku zao(menopause),huwa wanapata dalili za kuwa wenye wasi wasi,hasira,kutojisikia kushiriki tendo la ndoa,kutokana na mabadiliko ya homoni( post menopausal syndrome)Hali hii isipotibiwa huweza hata kusababisha ndoa kuvunjika.
Sasa watu hawa wasio na elimu ya kutosha wakiachwa tu waendelee na mafunzo yao yasiyo na tafiti,yanayotolewa tu kama hadithi za kizee,wanaweza kuleta balaa sana katika jamii kwa vile jamii yetu bado inawaamoni sana viongozi wanaojiita watumishi wa Mungu
 
Ili adhibitiwe yakupasa ulete ushahidi wa sauti ama video,maana hivi hivi wataamini vipi kama wewe sio Mkewe/dogo dogo wa mkewe ama una chuki nae binafsi?!!
 
Huyo mtumishi inawezekana anafanya utafiti kupitia waumini wake wanapoomba ushauri,kufanyiwa maombi na kutoa shuhuda.
Watumishi mbali na mapungufu ya kibinadamu wanajua mengi kuhusu jamii.

Kama hajafumaniwa asihukumiwe
 
Nimetoa kama tahadhari na nimetimiza wajibu wangu kama binadamu.

Mimi ni mmoja wa watu ninaoguswa sana na mauaji ya wanandoa kwa vile naamini kuna masuluhisho mengi mbadala.
Ili adhibitiwe yakupasa ulete ushahidi wa sauti ama video,maana hivi hivi wataamini vipi kama wewe sio Mkewe/dogo dogo wa mkewe ama una chuki nae binafsi?!!
 
Utafiti wake hautoshi kabisa na utaleta majanga kwa wana ndoa.
Huyo mtumishi inawezekana anafanya utafiti kupitia waumini wake wanapoomba ushauri,kufanyiwa maombi na kutoa shuhuda.
Watumishi mbali na mapungufu ya kibinadamu wanajua mengi kuhusu jamii.

Kama hajafumaniwa asihukumiwe
 
Sijaona kosa la pastor hapo.Kwani ni uongo kwamba wamama wanapenda viben ten na wababa wanapenda vibinti vidogo?

Zaidi sn naona km wewe ndy pastor au umekuja kumtangaza maana me naliikia Hilo jina
 
Mimi ni whistle blower,nimeleta uzi huu kwa vile Waziri wa mambo ya ndani ametoa rai kwa viongozi wa dini wasaidie hii hali ya wimbi la mauaji ya jinsi hii yasiwepo kwa wao kutoa mafundisho watu wawe na hofu ya Mungu.
Ila kwa mafundisho kama hayo (ya mke kupenda vijana wadogo) kutolewa na pastor ,sioni kama viongozi wa jinsi hii watakuwa msaada
Ili adhibitiwe yakupasa ulete ushahidi wa sauti ama video,maana hivi hivi wataamini vipi kama wewe sio Mkewe/dogo dogo wa mkewe ama una chuki nae binafsi?!!
 
Huyu mtumishi safi sana. Ukisikiliza mahubiri yake utatamani tuwe na watu kama hawa kama 50 hivi. Anabadili sana fikra za vijana na maisha kwa ujumla.
 
Wewe ni mmoja wa watu wenye akili nyepesi sana.
Nitafute hela ipi?Wanaotafuta hela watakufa wanatafuta.Mimi hela inanitafuta yenyewe.Hiyo level ya tafuta hela ni level za wavulana.
Kuwa kidogo ili uongee vitu vya akili
Umuue mke wako Kwa Sababu ya shimo lisilo Jaa Wacha uchizi wewe tafuta Hela Kula bata
 
Bahati mbaya sijamsikia sana.
Anaweza kuwa na mengi mazuri lakini akaharibu iwapo ataongea sana bila kuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya mahusiano
Huyu mtumishi safi sana. Ukisikiliza mahubiri yake utatamani tuwe na watu kama hawa kama 50 hivi. Anabadili sana fikra za vijana na maisha kwa ujumla.
 
Bahati mbaya sijamsikia sana.
Anaweza kuwa na mengi mazuri lakini akaharibu iwapo ataongea sana bila kuwa na elimu ya kutosha kuhusiana na masuala ya mahusiano
Mengi anayoongea ni kweli na ameyashuhudia kwa waumini wake waliokuwa wanakuja kuomba ushauri kanisani. Ameoa akiwa na 40 years, kwahiyo anajua anachoongea. Jaribu kusikiliza mafundisho yake utakuja kunishukuru.
 
Mimi kuna huyo wa Mbezi anajiita somebody Musa sijui mtume sijui kitu gani ana banda lake pale Msuguri yupo shemeji yangu nimeowa mdogo wake nasikia ananitangaza kwenye familia yao kwamba eti mtume wake amemwambia kwamba mimi ni mchukua misukule na tena ni freemason na hii ni baada ya kukataa kumkopesha mumewe hela ya mtaji so akenda kupiga ramli kwa huyo nabii ikaonekana bora hizo pesa sikuwapa eti ni za msukule.

Haya maneno ameniambia mke wangu na ni baada ya huyo dada yake kumuita kumuonya kuhusu mimi,hawa watu wanavuruga sana jamii sasa hivi na ukweli wanawake ndiyo victims wao kila wanaloambiwa wanabeba kama lilivyo na kama una mke akaenda kwa hawa wapumbavu hesabu huna ndoa wanawajaza ujinga ujinga ujinga!!!
 
Luh! Hii hatari sana.
Mimi kuna huyo wa Mbezi anajiita somebody Musa sijui mtume sijui kitu gani ana banda lake pale Msuguri yupo shemeji yangu nimeowa mdogo wake nasikia ananitangaza kwenye familia yao kwamba eti mtume wake amemwambia kwamba mimi ni mchukua misukule na tena ni freemason na hii ni baada ya kukataa kumkopesha mumewe hela ya mtaji so akenda kupiga ramli kwa huyo nabii ikaonekana bora hizo pesa sikuwapa eti ni za msukule.

Haya maneno ameniambia mke wangu na ni baada ya huyo dada yake kumuita kumuonya kuhusu mimi,hawa watu wanavuruga sana jamii sasa hivi na ukweli wanawake ndiyo victims wao kila wanaloambiwa wanabeba kama lilivyo na kama una mke akaenda kwa hawa wapumbavu hesabu huna ndoa wanawajaza ujinga ujinga ujinga!!!
 
Wewe ni mmoja wa watu wenye akili nyepesi sana.
Nitafute hela ipi?Wanaotafuta hela watakufa wanatafuta.Mimi hela inanitafuta yenyewe.Hiyo level ya tafuta hela ni level za wavulana.
Kuwa kidogo ili uongee vitu vya akili

Hiyo statement yako Ume quote from the book Rich Dad Poor Dad by Robert Kiyosaki ila kiuhalisia wewe haupo hivyo unavyo sema.

Ungekuwa Na Hela hizo usinge sumbuliwa Na mwanamke kiasi cha kutaka kuuondoa uhai wake halafu Maisha yako yote yaliyo baki ukayamalizie gerezani.

Motivation Speakers wameisha kuharibu tayari cause u take them serious ndio maana unataka kununua mkeo Kwa Sababu umesikia MTU anaongelea tabia hizo . So sad
 
Mkuu unachokisema kiko sahihi sana ingawa watu wameanza kutoa comment za kukukejeli. Kwa nchi za wenzetu mtu yoyote huwezi tu kuibuka na kuanza ku comment kwenye jambo ambalo hana utaalamu nalo, ndo maana kwa wenzetu waandishi huita wataalamu wa eneo husika kutoa mitazamo yao endapo kuna jambo ambalo limetokea kwenye jamii na wangehitaji kupata ufafanuzi au mitazamo ya kitaalamu......sasa hapa kwetu mtu yoyote hasa pia hufanywa na wanasiasa ambao huwa wanatolea uafafanuzi maswala ambayo kimsingi yanatakiwa yaongelewe na wataalamu husika.
 
Mengi anayoongea ni kweli na ameyashuhudia kwa waumini wake waliokuwa wanakuja kuomba ushauri kanisani. Ameoa akiwa na 40 years, kwahiyo anajua anachoongea. Jaribu kusikiliza mafundisho yake utakuja kunishukuru.
Tatizo hawa watu wenu wanawafundisha watu ujinga na wanaweza kuwa wana points ila watu weupe vichwani hasa wanawake wakisikia chochote kutoka kwao bila kuchuja wanakiingiza kwenye circle ya maisha ya kawaida mwisho wanagombanisha ndugu.

Naandika haya nikiwa najua maana imenitokea,kama wanajihisi wanajua kitu waingie madarasani wasome ili wajue namna bora ya kuwasilisha hoja zao but kienyeji kienyeji hivi hawatawafikisha popote ninyi mnaowaamini.
 
Duh pole sana mkuu
 
Back
Top Bottom