Huyu ofisa wa udahili TCU, Fabian Mahundu anapotosha umma kwa maslahi ya nani?

Offliner User please niweke sawa hapa ukimaliza Bsc hautasoma tena Bongomovie, naona kama kuna cha kujifunza hapa!
HAHAHA NILIMAANISHA: baada ya kumaliza Bachelor yangu TZ, niliapa kutosoma tena TZ...... Na hilo lilitimia! [HASHTAG]#pole[/HASHTAG] kwa usumbufu Norton82
 
Uko sahihi. Lakini,mfumo wa TCU ulidahili wanafunzi wenye ufaulu mdogo kwenye kozi zinazohitaji ufaulu mkubwa. Kozi husika,na hata vyuo vikuu husika,zikashuka kiheshima.
Hapana Mkuu. Waliokuwa wanadahili wanafunzi ni admission officers wa Chuo husika. Wao ndiyo wanachagua wenyewe kisha hutoa majina TCU.

Kibaya tu ninachokiona kwa CAS, walikuwa wanatoa nafasi kwa vyup fulani wachague wanafunzi fasta ili wapewe japo kidogo kwa vyuo ambavyo kwa namna fulani visingepata wanafunzi.
 
Hao lazima walikuwa wanapata chao, muhimu waondolewe hapo na kuahamishiwa kwingine kabisaaaaa. Hata kuchunguzwa kama wana shares kwenye hivyo vyuo.

Mfumo huu mpya ni mzuri na unatumika kwenye nchi nyingi pia kupitia taasisi kama hiyo ya TCU nchini.

Serikali bado ina kazi kubwa ya kuondoa na kusimamishwa wala rushwa kwa kweli na wavivu.
 
Jana nilimsikiliza ofisa mwingine wa TCU akiongea ITV, na leo yupo huyu anaitwa Fabian Mahundu. Ukiwasikiliza hawa maofisa maongezi yao yanaonesha kuwa, tunahama kwenye mfumo wa udahili uliokuwa bora, wenye ufanisi mkubwa na madhubuti, na tunahamia kwenye mfumo ambao ni crude, inefficient na utakaokuwa na changamoto nyingi.

Mimi ni mdau wa elimu, nafahamu wanachojaribu kukiaminisha kwa uma hawa jamaa ni upotoshwaji uliokithiri. Wametumwa hapo kutetea interests za vyuo vya kibabaishaji vilivyoanzishwa vichochoroni huku wakijineemesha kwa rushwa kubwa kuanzia uanzishwaji wake hadi kuwahakikishia rundo la wanafunzi.

Kwa jinsi wanavyoongea hawa jamaa, ipo dhahiri kuwa wapo tayari kuhujumu mfumo huu mpya, ili uonekane haufai na ikiwezekana turejee mfumo wa zamani. Naomba, nitoe wito kwa waziri Ndalichako, awabadilishe vitengo hawa jamaa, wasijihusishe kabisa na process za udahili.

Lakini pia, maongezi yao ni insurbodination kwa Rais ambae aliongea publicly kuwa huo mfumo ulikuwa misused.

Hawa dawa yao ni kutumia staili kama ile aliyoitumia Charles Keenja alivyofanya miaka ya huko nyuma kwenye uongozi wa jiji la Dar es Salaam. Halafu mimi nashangaa, huko nyuma hatukuwa na TCU, je vyuo vyetu vilikuwa havidahili wanafunzi?
 
Hujaongea substance of your malalamiko. wanasemaje, eleza. wanatetea CAS au huu wa kutuma vyuoni applications
Pili, achana na mambo ya rais, rais huyu usimuone kama infallible... , he can make mistakes and always they make mistakes because of abuse of power, they make a lot of mistakes, tena silly ones!
Hapa ndio tunapokuja na hisia za ajabu. Inaelekea kuna watu hawa amini hili au hawataki kabisa kuliamini. Wengine wanashindwa kujadii wazo wanasema ni directive. Cha ajabu ni hawa TCU kama wamesha lipitisha na kutangaza sioni sababu ya wao kuanza kulipinga (assuming ni kweli) sasa hivi, watu walilizungumzia hili kwa kirefu baada tu ya raisi kulisema huo ndio ungekuwa wakati wao kuzungumza. Sasa wanatakiwa waje na damage control tactics na sivinginevyo.
 
Mi naona mfumo wa TCU uko vizuri maana mtu unaomba vyuo unavyopenda. Cha muhimu cha kuboresha ni mtu ukikosa vile ulivyoviomba wasilete huruma ya kukupangia kwingine wakuache nyumbani mpaka mwaka ujao
 
Hili ndilo muhimu zaidi kwa mwanafunzi kuzingatia.

Ukifaulu vizuri huna hata haja ya kuapply vyuo viwili, chuo kimoja tu kingetosha. Tatizo ni huu ufaulu hafifu.
Ufaulu hafifu utakuwepo siku zote. Biological, environmental and socio economic variation ni kawaida katika maisha ya binadamu. Hivyo tuje na mifumo ambayo itawapa maombaji wenye ufaulu unaotakiwaa vyuo vinavyotoa elimu yenye viwango vilivyo pitishwa.
 
Hivi advance level mbona tunachagua shule na Necta wanatupangia? Basi na Necta waache watu waende shule tu wanazozitaka. Kwa hili presidaa kachemka. Sasa ngoja watumie hela kuapply kila chuo uone gharama kama hazitazidi mpaka waanze kulalamika
 
Uko sahihi. Lakini,mfumo wa TCU ulidahili wanafunzi wenye ufaulu mdogo kwenye kozi zinazohitaji ufaulu mkubwa. Kozi husika,na hata vyuo vikuu husika,zikashuka kiheshima.
Kivipi kwa mfano wakati cut off points zipo pale. Au nyie mmekurupukia wapi? Mnaujua kweli mfumo?
 
  • Thanks
Reactions: kdc
Mi naona mfumo wa TCU uko vizuri maana mtu unaomba vyuo unavyopenda. Cha muhimu cha kuboresha ni mtu ukikosa vile ulivyoviomba wasilete huruma ya kukupangia kwingine wakuache nyumbani mpaka mwaka ujao[/QUOTE]
Nina wasi wasi watafanya hivyo mwaka huu-tuwe wavumilivu hayo yakitokea, watapata walivyotaka wenye ufaulu unaostahili lakini kiasi kikubwa kinaweza kuachwa hewani.
 
Hivi advance level mbona tunachagua shule na Necta wanatupangia? Basi na Necta waache watu waende shule tu wanazozitaka. Kwa hili presidaa kachemka. Sasa ngoja watumie hela kuapply kila chuo uone gharama kama hazitazidi mpaka waanze kulalamika
NECTA ndio wa kwanza kutangaza utumiaji wa kuomba vyuo moja kwa moja (ukiacha program za afya na elimu za vyuo vya serikali-sijui kwa nini?).
 
Badala ya kwenda mbele tunarudi nyuma hatua 1000 na tunajipongeza.... Huu ni uwendawazimu
 
  • Thanks
Reactions: kdc
Hivi mkuu ww unadhani ni kwamba TCu hawayajua mapungufu au? watu wana mipango yao bana achana nao.
Sirikali we iache fanya shughuli zako.
 
TCU ilifanya vizuri sana kuharmonise. Ilipunguza kwa kiasi kikubwa application fees ambayo ninaona sasa mwanafunzi atatumia mpaka laki 3 kufanya application. Hata hivyo TCU kama chombo cha usimamizi kinachofanya monitoring and Evaluation ya vyuo, haikutakiwa kufanya hii kazi. Maana kuna vyuo vingine vingine vililetewa wanafunzi wasiofaa na kwa sababu vinahitaji ada vimewapokea tu. TCU imeshindwa sasa kuvisimamia vyuo na kuangalia ubora wa wanafunzi na walimu kwa sababu yenyewe imekuwa sehemu ya tatizo la kuleta wanafunzi wasio na sifa. Kwa sasa hakuna monitoring ya vyuo maana TCU kwa kiasi kikubwa ilijiingiza kwenye uendeshaji.
Pia walisaidia kuaminimize errors ulikuwa mfumo ambao unaendana na kasi ya mabadiliko ya dunia kwa matumizi ya digit
 
Kama alikosa nafasi MUHAS ni juu yake,labda alichelewa kuapply kwasababu jinsi unavyowai kuapply ndio jinsi chance ya kupata nafasi kwenye chuo husika inavyokua kubwa.
Mfano MUHAS wana idadi yao ya wanafunzi wanaowahitaji na kutokana na wanafunzi wengi kuhitaji kusoma hiko chuo wana wai kuapply.
Kuna dogo mwaka juzi alichelewa kuapply UDSM akakosa nafasi wakati alikua ana div 2,sasa hivi anasoma Chuo kikuu cha Iringa lakini malengo yake yalikua ni kusoma UDSM.
Kama mtu unataka chuo fulani na una vigezo wahi kuapply utapata bila shida ila ukichelewa lazima ukose.
Wanaita first come first serve
 
Ufaulu hafifu utakuwepo siku zote. Biological, environmental and socio economic variation ni kawaida katika maisha ya binadamu. Hivyo tuje na mifumo ambayo itawapa maombaji wenye ufaulu unaotakiwaa vyuo vinavyotoa elimu yenye viwango vilivyo pitishwa.
Mabadiliko haya yaliyotangazwa na Rais ndio njia kuelekea huko.Vyuo visivyo na mvuto wacha vife tu.Kuendesha elimu kwa kuangalia "uwingi wa vyuo" na "uwingi wa wanafunzi" bila kuzingatia ubora kunaua elimu yetu.

Ni muhimu sana hii kuweka levels za vyuo ili kuwamotivate wanafunzi kusoma kwa bidii, kama Division 1 Point 5 kwa mfano akanyimwa Mhimbili na kupelekwa chuo cha hadhi ya chini,na wa division 2 akaenda Mhimbili, kesho kipi kitawamotivate wanafunzi wa PCB wanaotaka kusomea udaktari?

Wacha wanafunzi wenyewe wachague vyuo wanavyovitaka,kisha competition itaamua wenye marks za juu zaidi wasome vyuo gani. Hii itakuwa ni motivation factor kwa wanafunzi.

Na kwa vyuo, itaongeza ushindani zaidi ambao ni mzuri sana kama kweli tunajali ubora wa elimu yetu.
 
Back
Top Bottom