analysti
JF-Expert Member
- Aug 24, 2009
- 731
- 614
Jana nilimsikiliza ofisa mwingine wa TCU akiongea ITV, na leo yupo huyu anaitwa Fabian Mahundu. Ukiwasikiliza hawa maofisa maongezi yao yanaonesha kuwa, tunahama kwenye mfumo wa udahili uliokuwa bora, wenye ufanisi mkubwa na madhubuti, na tunahamia kwenye mfumo ambao ni crude, inefficient na utakaokuwa na changamoto nyingi.
Mimi ni mdau wa elimu, nafahamu wanachojaribu kukiaminisha kwa uma hawa jamaa ni upotoshwaji uliokithiri. Wametumwa hapo kutetea interests za vyuo vya kibabaishaji vilivyoanzishwa vichochoroni huku wakijineemesha kwa rushwa kubwa kuanzia uanzishwaji wake hadi kuwahakikishia rundo la wanafunzi.
Kwa jinsi wanavyoongea hawa jamaa, ipo dhahiri kuwa wapo tayari kuhujumu mfumo huu mpya, ili uonekane haufai na ikiwezekana turejee mfumo wa zamani. Naomba, nitoe wito kwa waziri Ndalichako, awabadilishe vitengo hawa jamaa, wasijihusishe kabisa na process za udahili.
Lakini pia, maongezi yao ni insurbodination kwa Rais ambae aliongea publicly kuwa huo mfumo ulikuwa misused.