Huyu ni mdudu Tandu? ana madhara gani?

Baada ya King Kong kunipa jina nimecheki Google.

Wanasema wanasaidia kuua wadudu wengine kama mende na kwamba wanapokuuma unaweza pata maumivu ila yanaisha ndani ya siku mbili.

Wanasema specie hii ya wadogo hawana sumu ya kukuua!

Wanadai ni vizuri kuwaacha, unajua tena mambo ya mabeberu. Kumbe Wajapan wanawafuga kama pets.
Unaposema mabeberu unamaana huwa wanakumendea?
 
Huyo ni tandu. Anasumu kali sana.
Anapenda sana nyumba zenye uchafu.
Nyumba yako inaelekea ni chafu sana na kuna makorokoro mengi kama viatu vya zamani visivyo tumiwa nk.
Mwanamke gani wewe mchafu hivyo na huoni aibu ya kuanika uchafu wako.
Wanaume utaishia kukutana nao gesti na sahau ndoa kama huyajirekebisha.
we jamaa wew...panic ya nini mkuu....ni ushauri tu kaomba mkuu...isiwe ugomviii....hahahaahahahah
 
Usiue ovyo Viumbe hai, tambua kuwa kila kiumbe ana haki ya kuishi. Endapo kiumbe kaingia kwenye himaya yako usimdhuru bali mtoe na kumweka kwenye mazingira wezeshi ya yeye kuishi, ama la muite AFISA MALIASILI WA HALMASHAURI ndizo kazi zao za Uhifadhi. Zingatia ushauri huu ili tusitokomeze baadhi ya Viumbe. Nowdays hata kumuona kobe imekuwa nadra, mijusi, vippepeo, nyigu nk hiii yote ni kutokana na Elimu duni ya Viumbe tuliyonayo hasa Kuwaua viumbe pasipo kuwa na matumizi nao. Utakuta Watoto wanaua panzi, mijusi, ndege nk with no reason. Wizara husika imelala fofoooooo.

Hivi vipepeo waliishiaga wapi au na wenyewe tuliwauza sana nje kinyemela?

Ukitembelea nchi nyingine unaona ndege wazuri wanaishi kwa amani tu, wanapendezesha sana mazingira, sisi kunguru tu wamebaki angani wanakula mapapai yetu.

Hao wote hatukuwaua, tumewauza!
 
ni tandu.... ana tabia kama za nyoka kwamba ukipishana naye na yeye anapishana na wewe..... anakula wadudu wadogowadgo na anapenda sehemu zenye joto...... hana sumu ya kuua lakini maumivu ni makali...... WAPO AINA NYINGI.... KUNA WAKUBWA AMBAO AKIKUOTEA UNAKUFA.
Mkuu unamfahamj swila au unamsikia? Swila akiingia ndani usiku hua anatafuta njia kwa kugonga gonga yaani kama ni jikoni basi utakuta kagonga masufuria hadi vikombe

Sent using unknown device
 
Hivi vipepeo waliishiaga wapi au na wenyewe tuliwauza sana nje kinyemela?

Ukitembelea nchi nyingine unaona ndege wazuri wanaishi kwa amani tu, wanapendezesha sana mazingira, sisi kunguru tu wamebaki angani wanakula mapapai yetu.

Hao wote hatukuwaua, tumewauza!
😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Kila baada ya wiki kadhaa, nimekuwa nakumbana na mdudu huyu ndani ya nyumba. Uzuri mara zote nimekuwa namuwahi kumuua kabla hajanigusa.

Kuna mtu alikuwepo nymbani siku moja wakati anatokea akaniambia ana sumu kali.

Naomba nijue jina lake na mengine muhimu ninayotakiwa kujua.

View attachment 1048752
Vitu vichache nilivyoona kuhusu huyu mdudu:
  1. Ana kichwa kigumu sana. Unaweza kumpiga na kiatu hata mara nne bado akawa hai.
  2. Anatembea kwa kasi sana. Huyu wa kwenye picha ni kwamba nilikuwa tu kwenye alert ila alikuwa anakuja kwangu kwa kasi.
  3. Akiwa anatembea kwenye corridor, anatembea kwenye corner kabisa iwe ngumu kumpiga.
  4. Hauwezi kumkuta ametulia tu. Usipomuwahi anaweza kupotelea kwenye makochi huko.
Wewe umesoma arts itakuwa halafu utakuwa sio mtz

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyo ni tandu. Anasumu kali sana.
Anapenda sana nyumba zenye uchafu.
Nyumba yako inaelekea ni chafu sana na kuna makorokoro mengi kama viatu vya zamani visivyo tumiwa nk.
Mwanamke gani wewe mchafu hivyo na huoni aibu ya kuanika uchafu wako.
Wanaume utaishia kukutana nao gesti na sahau ndoa kama huyajirekebisha.
#Weee ungemwambia tu huyo ni mdudu gani.. Hayo ya Uchafu achana nayo.... #

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vizuri sana.
Usiue ovyo Viumbe hai, tambua kuwa kila kiumbe ana haki ya kuishi. Endapo kiumbe kaingia kwenye himaya yako usimdhuru bali mtoe na kumweka kwenye mazingira wezeshi ya yeye kuishi, ama la muite AFISA MALIASILI WA HALMASHAURI ndizo kazi zao za Uhifadhi. Zingatia ushauri huu ili tusitokomeze baadhi ya Viumbe. Nowdays hata kumuona kobe imekuwa nadra, mijusi, vippepeo, nyigu nk hiii yote ni kutokana na Elimu duni ya Viumbe tuliyonayo hasa Kuwaua viumbe pasipo kuwa na matumizi nao. Utakuta Watoto wanaua panzi, mijusi, ndege nk with no reason. Wizara husika imelala fofoooooo.
Ila huyo afisa maliasili umuite aje achukue mende, mjusi au huyo tandu nadhani na yeye atakuona ni zuzu.

Nakushauri anzisha zoo ya viumbe hao na tangaza mtu yeyote anayekutana na design hiyo ya mifugo akupigie simu ukaichukue na ukaiweke kwa zoo yako.

Utakuwa umefanya jambo la mbolea na kuongeza mapato na kulipa kodi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom