Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
- Thread starter
- #61
Huyo ni tandu. Kama umeshaoa basi nyumba yako ni chafu mwambia mkeo azidishe usafi. Na kama unaishi geto basi pangilia vizuri vitu vyake. Nyumba ikiwa safi uyo mdudu huwezi kumkuta
Nitakujibu wewe kuhusu suala hili la uchafu kwa sababu kidogo umeongea kwa staha, lakini ujumbe huu uwafikie wote waliokuwa wanadai nyumba yangu ni chafu!
Ni hivi, nyumba ni safi tena sana tu, unaweza hata kulia chakula sakafuni!
Kwa maelezo niliyosoma kuhusu huyu mdudu ni kwamba kwanza hata hawafuati vyakula kama mende, na kama ni hivyo wasingevikuta kwangu!
Ni kwamba mara nyingi hamna mtu nyumbani. Kinachoweza kuwa kinawaleta inawezekana ni giza, mara nyingi nyumba inakuwa kwenye giza. Ushauri wa jamaa mmoja kuhusu kufungua madirisha na mapazia nadhani kwa case yangu ndiyo inaweza kuwa suluhisho. Ila kwenye usafi, niko vizuri!